Wednesday, December 31, 2014

YANGA, SIMBA, AZAM KUUMANA KOMBE LA MAPINDUZI

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeahirisha mechi za raundi ya tisa na kumi za timu nne zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na kuziruhusu kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza kesho hadi Januari 13, 2015 Zanzibar.

Timu za Tanzania bara zitakazoshiriki ni mabingwa watetezi Azam FC, Simba, Yanga na Mtibwa Sugar.
Awali, kabla ya TFF kushindwa kuthibitishiwa uwepo wa mashindano hayo kutokana na viongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kupelekana mahakamani, timu zilikuwa zikiendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi za raundi ya tisa zilizokuwa zifanyike Jumamosi ijayo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MZUNGU WA SIMBA AMETUA ASUBUHI HII KUMRITHI PHIRI


IMG-20141231-WA0000
KOCHA mpya wa Simba sc, Mserbia Goran Kapunovic amewasili asubuhi ya leo majira ya saa 1:00 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Goran ametua kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways na baada ya kuwasili amesema amekuja kufanya kazi na sivinginevyo.
Hata hivyo kocha huyo anayerithi mikoba ya Patrick Phiri amesema atazungumza mengi baada ya kumalizana na viongozi na kuanza kazi yake.
Goran anatarajia kuiongoza Simba kwa mara ya kwanza katika mechi za kombe la Mapinduzi linaloanza kutimua vumbi kesho januari mosi mwakani. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

BOSI UEFA AISHAURI FIFA KURUHUSU KADI NYEUPE UWANJANI

Soccer - Michel Platini File Photo

Rais wa UEFA Michel Platini amesisitiza mpango wake wa kuanza matumizi ya ‘Kadi Nyeupe’ itakayowafanya wachezaji watolewe nje kwa muda kisha kurejeshwa baadaye. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 59 alitoa wazo hilo kwa mara ya kwanza Oktoba lakini likapingwa na Rais wa FIFA Sepp Blatter.
Hata hivyo, Platini ameshikilia msimamo wake katika mkutano wa tisa wa kimataifa wa michezo unaofanyika Dubai.
“Kadi nyeupe ni kitu kipya. Inahusiana na tabia ya wachezaji wa soka. Kujiangusha na kujifanya kuumia, kupinga maamuzi ndani ya uwanja, haya hayakubaliki kwa watu wanaopenda mchezo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Monday, December 29, 2014

MGOMBEA URAIS ATABIRIWA KIFO

 
Maalim Hassan Hussein (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaama jana.

Maalim Hassan Hussein, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, marehemu Sheikh Yahya Hussein, ametabiri mambo 18 yatakayotokea mwakani, likiwamo la kufariki ghafla kwa kiongozi mmoja mzee ambaye yumo kwenye mbio za urais mwakani.

Hussein alisema jana kuwa kiongozi huyo atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali. Akitangaza utabiri wa mwakani, alisema: “Kiongozi huyo atakufa wakati akipelekwa hospitalini.”

Alisema pia mwandishi mmoja mashuhuri nchini atakufa kifo chenye utata kitakachoitesa Serikali na familia yake katika kutafuta sababu za kifo chake. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

NYARANDU AJITOSA KUWANIA URAIS 2015

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akisalimiana na wananchi wake katika uwanja wa Ilongero Singida Vijijini, baada ya kumaliza kuhutubia jana. (Na Mpigapicha Wetu).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu

MBIO za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimechukua sura mpya baada ya jana Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kutangaza rasmi nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka kesho.
Nyalandu anaungana na makada wengine wa CCM wakiwemo mawaziri waandamizi katika serikali ya Rais Kikwete, mawaziri wakuu wastaafu na hata wabunge waliotangaza nia au kutajwatajwa kwa nafasi hiyo, hivyo kuongeza joto la urais ndani ya CCM.
Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wake kwenye uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Ilongero Wilaya ya Singida Vijijini jana, Nyalandu mmoja wa waziri vijana, alisema muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MTOTO WA MIEZI MITATU MWATHIRIKA DAWA ZA KULEVYA

 
Zena akiwa na mtoto wake. Mwanamke huyo na wataalamu wa tiba wanathibitisha kuwa mama mwenye uraibu anayenyonyesha anaweza kumwathiri mtoto.

Mtoto mwenye umri wa miezi mitatu, mkazi wa Buza, Dar es Salaam amebainika kuwa mwathirika wa dawa za kulevya.
Damu na mkojo vya mtoto huyo (jina tunalihifadhi) vilichukuliwa na kupimwa katika maabara ya Hospitali ya Mwananyamala na baada ya saa mbili, majibu yalitoka na kuthibitisha kwamba alikuwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroini.
Taarifa za kitabibu zinaonyesha kuwa kuwapo kwa heroini mwilini mwa mtu, huweza kuonekana katika mkojo ndani ya siku mbili hadi nne iwapo dawa hizo zilitumiwa na mhusika kwa kati ya saa mbili hadi tano.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...