Rais wa Gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow.
Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''.
Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.