Naibu waziri wa Afya
Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala akiwa anazungumza na
waandishi wa habari wanawake kuhusu tatizo la Saratani ya shingo ya Kizazi,
katika Ukumbi wa Olasiti Lodge Jijini Arusha, aliyepo kushoto kwake ni
Dkt. Mathew Kasumuni kutoka hospital ya Mountmeru iliyopo jijini Arusha.
Waandishi wa habari
wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya
jamii wazee jinsia na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala, Aliyepo kushoto kwake ni
Dkt. Mwanahamis Ghembe kutoka Mountmeru Hospital.
Naibu
waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la
ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV
vinavyosababisha Saratani ya mlango wa kizazi.
Kigwangala
amesema wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango
wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila kinga,huambukizwa
kwa kujaamiana. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
Kigwangala
amesema kuwa kati ya wanawake 100,000 wanawake 50.9% wanaweza kupata
saratani ya Shingo ya kizazi,na kati ya hao asilimia 37.5% wanapoteza maisha
hivyo serikali imeanza kutekeleza utafiti wa mradi ambao utahusisha wasichana
wenye umri kati ya miaka 9-14 katika wilaya ya Moshi na utakapokamilika
wataanza utoaji wa chanjo hiyo kwa nchi nzima,amewataka kutokufanya ngono
mapema.
Amesema
kuwa Saratani ya mlango wa kizazi haionyeshi dalili wala maumivu yeyote amesema
mgonjwa anaweza akawa nao kuanzia miaka 10-15 bila kujitambua huku dalili
zikiwa zinakwenda taratibu sana.
Kwa
upande wake Dkt. Mathew Kasumuni kutoka hospital ya mount Meru amesema kuwa
dalili za Sratani ya Mlango kizazi ni kutokwa na damu bila mpangilio,kutokwa na
majimaji yenye harufu kali,amewataka wanawake watakapoziona dalili hizo wawahi
hospitali mapema kabla tatizo halijawa kubwa.
Aidha
Masumuni amesema kuwa unaweza kujikinga ili usipate saratani ya mlango wa
kizazi kwa kupima saratani ya mlango wa kizazi mapema, kupunguza idadi ya kuzaa
watoto wengi,kupunguza idadi ya wpenzi wengi,ukifanya ngono watumie kinga.
Sambamba
na hayo Dkt. Mwanahamisi Lyinga amesema kuwa zipo njia kuu tatu za kupima
saratani ya mlango wa kizazi mabazo ni pamoja na kutumia Darubini, Upimaji wa(
DNA)wa kirusi,pamoja na Via utambuzi wa kuona kwa kutumia Siki.
Kwa
upande wake Sr. Noela Lyinga ambaye ni muuguzi katika hospitali ya Mountmeru
ametoa elimu kwa wanawake wawe wanajikagua matiti yao kila wanapomaliza
mzunguko wao wa hedhi kila mara ili kuona kama yapo mabadiliko katika matiti
yao ambayo yanaweza kuleta saratani ya matiti.
Lyinga
amewataka wanawake mara wanapoona dalili yeyote ambayo siyo ya kawaida
katika matiti yao wasisite wawahi hospitali mapema wakafanyiwe uchunguzi na
vipimo ili kama utagundulika ugonjwa waweze kupatiwa matibabu kwa haraka zaidi. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
Na Woinde
Shizza Arusha.
No comments:
Post a Comment