Rais Magufuli alivyokutana na Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo
Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara
Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha
Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko
Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa
Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo
kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa
wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya
Viwanda. Tangaza biashara yako hapa. Pia like
page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote
kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu
ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya
biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.
Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni
chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya
kutengeneza faida tu.
''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na
viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili
ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili ''
amesema Rais Magufuli.
Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia
kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa
shilingi bilioni 43 kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu
ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote,
Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa
amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya
Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya
mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.
Katika kuthibitisha hilo, tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori
mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la
kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la
kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya
kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.
Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya
kazi na Serikali ya Tanzania na kamwe hana nia yoyote ya kufunga
kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana
mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini
kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu
ya Tano.
Katika hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi
ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Singida.
Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye
anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt.
Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa
Itifaki).
Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment