SIMBA
SC imelazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Matokeo hayo yatapokewa kwa furaha na mahasimu, Yanga ambao sasa wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa pointi sita kuelekea mechi nne za mwisho. Kwa sare hiyo ya 0-0, Azam FC inafikisha pointi 59, wakati Simba sasa inakuwa na pointi 58, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 65 baada ya timu zote kucheza mechi 26.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mathew Akrama wa Mwanza, aliyesaidiwa na washika vibendera Abdallah Mrisho wa Pwani na Omar Kambangwa wa Dar es Salaam hakukuwa na mashambulizi ya kusisimua na timu zote zilionekana kucheza kwa tahadari kupita kiasi, hivyo kuufanya mchezo upooze.