Mkuu wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ameunga
mkono maandamano ya kupinga mabadiliko katika ya sheria ya uchaguzi
ambayo imezua siku tatu za maandamano.
Kadinali laurent Monsengwo ameitaka mamlaka kwa maneno yake mwenyewe kusitisha mauaji ya raia wake. Amewataka waandamanaji kuweka amani.
Makundi ya haki za kibinaadamu yamesema kuwa zaidi ya watu 40 wamefariki katika ghasia hizo.
Vyama
vya upinzani vinasema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa ililenga
kuchelewesha uchaguzi ili rais Joseph Kabila aendelee kuwa mamlakani
baada ya kipindi chake cha utawala kuisha mwaka ujao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.