Monday, December 22, 2014
WAHITIMU 344 WA DARASA LA SABA HAWJUI KUSOMA NA KUANDIKA...!!!
Wanafunzi 344 waliomaliza darasa la saba
mwaka huu mkoani hapa wamebainika kuwa hawajui kusoma, kuandika na
kuhesabu. Ofisa elimu wa mkoa, Nestory Mloka alitoa taarifa hiyo juzi
katika kikao cha elimu kilichoitishwa kwa ajili ya kuchambua matokeo ya
mtihani wa darasa la saba na kuwapangia shule wahitimu waliofaulu.
Mloka alisema kati ya walihitimu hao ambao hawajui kusoma na kuandika, wavulana ni 163 na wasichana 181. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
KIKWETE "HATUWEZI KUENDELEA KWA KUTEGEMEA RAMLI"
Sehemu ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyoko Tengeru Arusha.
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa kamwe Tanzania, kama ilivyo nchi
nyingine yoyote duniani, haiwezi kuendelea kwa kutegemea mazingaombwe
ama ramli bila kuwekeza kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Aidha, ametaka Watanzania kuacha mwenendo wa kutumia ubishi wa
kisiasa kutafuta majawabu ya changamoto za maendeleo akisisitiza kuwa
majawabu ya maendeleo yatapatikana katika maendeleo ya sayansi na
teknolojia.
Amewataka Watanzania kuongeza kasi yao ya matumizi ya intaneti
akisema kuwa mfumo huo wa habari na mawasiliano ni chimbuko kubwa la
elimu ikiwemo elimu ya sayansi kuliko kutegemea kupata elimu hiyo katika
magazeti.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
MUME AMJERUHI MKEWE KWA SHOKA KISA WIVU WA MAPENZI
Mama
mwenye watoto watatu anapata matibabu hospitalini nchini Malaysia baada
ya mumewe kuvamia mikono yake na miguu nakumcharanga kwa shoka la
kucharangia nyama,na baadaye mwanamume huyo kujinyonga .
Mama huyo
anatajwa kama K Menaga,amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi
katika hospitali ya Kluang upande wa kusini mwa jimbo la Johor baada ya
shambulio hilo hatari lililotokea mapema mwezi huu.Ingawa taarifa kutoka hospitalini hapo zinaarifu kuwa mama huyo ameshatolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya hali yake kuendelea vyema,na amelazwa katika wodi ya wagonjwa wa kawaida.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
WAAMUZI 11 WA KITANZANIA KWENYE ORODHA YA FIFA
Shirikisho
la soka ulimwenguni FIFA limetoa orodha mpya ya waamuzi linaowatambua
,Kwenye orodha hiyo kuna jumla ya waamuzi 18 kutoka Tanzania,miongoni
mwa waamuzi hao waamuzi 11 wapya na 7 wa zamani.
Waamuzi wapya wa
kati kutoka Tanzania ni Mfaume Ali Nassor kutoka visiwani Zanzibar
pamoja na Martin Saanya kutoka Morogoro, pia wamo waamuzi watatu wa kike
ambao ni Florentina Zabron ,Jonesia Rukyaa pamoja na Sofia Ismail.Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wanaume ni Frank John Komba na Soud Idd Lila , kwa upande wa wanawake ni Kudura Omary Maurice,Hellen Joseph Mduma,Dalila Jafari Mtwana na Grace Mawala.
Waamuzi wa zamani wa Tanzania kwenye orodha ya FIFA ,kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni Nkongo na Waziri Sheha Waziri,kwa upande wa waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali,Fernand Chacha,John Longino Kanyenye ,Ali Kinduli na Samuel Hudson Mpenzu .
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
STERLING MWANASOKA BORA CHIPUKIZI
Mshambuliaji
kinda wa Liverpool, Raheem Sterling amekabidhiwa Tuzo ya Mwanasoka bora
chipukizi mwaka 2014 na Chama cha soka cha England FA.
Sterling
alikabidhiwa tuzo hiyo kabla ya Mechi wa ligi kuu ya England kati ya
Liverpool dhidi ya Arsenal wakiwa uwanja wa nyumbani Anfield, ambapo
mechi hiyo imemalizika kwa sare ya goli 2-2.FA imekuwa na utaratibu wa kutoa tuzo ya Mwanasoka bora wa mwaka kwa wachezaji chipukizi wanaofanya vizuri katika mchezo wa soka.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Sunday, December 21, 2014
BIBI AMUUA MJUKUU WAKE KWA KUMTUPA NJE YA BASI
Mmoja wa abiria waliokuwamo kwenye basi hilo, Ebenezer Hans alilieleza gazeti hili kwamba mama huyo akiwa miongoni mwa abiria, alikuwa na mtoto wake mwenye umri unaokadiriwa miaka 14 na wajukuu wawili, ambao alikuwa akisafiri pamoja nao. PICHA|MAKTABA
Jeshi la Polisi
mkoani Singida, linamshikilia Nawaridi Saidi (45), mkazi wa Dar es
Salaam kwa tuhuma za kumtupa mjukuu wake Mayasa Meshack (6) kutoka ndani
ya gari wakati akisafiri kwenda Kigoma akitokea Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias
Sedoyeka alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 18, saa 2 usiku
katika Kijiji cha Igugumo, wilayani Iramba ambapo mama huyo akiwa kwenye
basi aina ya Scania, alifungua dirisha kutoka katika kiti alichokaa na
kumtupa Mayasa wakati basi likiwa katika mwendo.
“Mama alikuwa anaenda mkoani Kigoma kwa ajili ya
Sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya, aliambatana na mtoto wake mwingine
ambaye jina bado halijafahamika,” alisema Kamanda Sedoyeka. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
SERIKALI YAONYA DAFTARI LA WAPIGAKURA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mh. Willium Lukuvi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William
Lukuvi, ameonesha kutoridhishwa na utaratibu mbovu unaotumika
kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura, kutokana
na kuwa na mianya inayoweza kuingiza wasio raia wa Tanzania.
Lukuvi aliyasema hayo jana, wakati alipotembelea kituo cha Bunju A
kuangalia uandikishwaji wa wananchi kwa kutumia teknolojia mpya ya
Biometric Voter Registration (BVR).
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
MITAA 89 KURUDIA UCHAGUZI LEO DAR
Jumla ya mitaa 89 kutoka wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, leo zinatarajiwa kufanya uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka huu.
Moja ya kasoro hizo ni kuchanganywa kwa majina ya wagombea wa uenyekiti na wajumbe.
Manispaa ya Temeke ina mitaa 10, Kinondoni 16 na Ilala 63 .
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa manispaa ya
Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, ameingia kwenye mvutano mkubwa na Chama
cha Wananchi (CUF), kuhusu uamuzi wake wa kutaka uchaguzi urudiwe
katika Mtaa wa Mwinyimkuu huku ikidaiwa chama hicho kilishinda.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUSABABISHA KIFO CHA PUNDA...!!!
Mwanaume
mmoja nchini Hispania amefunguliwa mashtaka ya kutesa wanyama baada ya
kusababisha kifo cha punda aliyemuua wakati akimkalia kwa lengo la
kupiga nae picha.
Sabu ya kifo cha punda aliejulikana kwa jila na Platero inasemekana
ni uzito uliopitiliza wa mwanaume huyo na kusababisha kumpa maumivu
makali mnyama huyo hadi alipopoteza maisha baada ya siku tatu.
Picha hiyo iliwekwa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanaume
huyo mwenye umri wa miaka 38 akitabasamu huku akipiga picha na mnyama
huyo.
Baada ya siku mbili Punda huyo aliyekua akiugulia maumivu alishindwa
kusimama na baada ya uchunguzi wa Polisi aligundulika kuvunjika baadhi
ya viungo vyake kutokana na kubeba kitu kizito. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
POLISI WAWILI WAUAWA MAREKANI
Maafisa wawili wa polisi mjini New York Marekani wameuawa kwa kupigwa risasi walipokuwa ndani ya gari lao eneo la Brooklyn.
Kamishna
wa idara ya polisi mjini New York Bill Bratton amesema kuwa maafisa hao
walilengwa na kuuawa kutokana na sare walizokuwa wamevaa.Alisema kuwa awali mwanamume huyo alikuwa ameandika ujumbe wa kuwashutumu polisi kwenye mtandao wa kijamii baada ya kumfyatulia risasi na kumjeruhi vibaya mpenzi wake wa zamani .
Mauaji hayo ya polisi yanajiri wakati kunashuhudiwa ghadhabu kali kufuatia uamuzi wa hivi majuzi wa kutowafungulia mashtaka polisi wazungu waliohusika kwemye mauaji ya waamerika weusi.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
PLUIJM ATOA SIKU SABA (7) KUIBADILI YANGA
Kocha Hans Van Der Pluijm akiwa na Boniface Mkwasa katika moja ya mechi za Yanga Uwanja wa Taifa.
BAADA ya kupewa mkataba wa mwaka moja na nusu kukinoa kikosi cha
Yanga kocha Hans van der Pluijm ameomba siku saba kuibadili timu hiyo.
Pluijm alisema atahakikisha anatoa mbinu zake zote alizokuwa nazo za
ukocha ili aweze kuipa mafanikio timu hiyo msimu huu ikiwemo kutwaa
ubingwa wa Tanzania bara.
Pluijm aliyetua Yanga kwa mara ya pili akichukua nafasi ya Mbrazil
Marcio Maximo alisema kwa kuanza atatumia siku saba kwa ajili ya
kubadilisha mfumo na kasi ya wachezaji ili waweze kushinda mchezo wao wa
Ligi Kuu dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa
Desemba 28.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
U.S.A YAITAKA KOREA KASKAZINI KUILIPA SONY
Marekani imezitaka China na nchi zingine kuthibitisha kuwa Korea
Kaskazini ilihusika na uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony
Pictures.
Marekani inasema kuwa Korea Kaskazini ni lazima ikiri kuwa ilihusika na iilipe Kampuni ya Sony kutokana na hasara ambayo imepataKorea Kaskazini imeyataja madai hayo ya Marekani kuwa ya uongo.
Wataalamu wanasema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa Korea Kaskazini ilihusika.
Lakini mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini anasema kuwa kampuni ya Sony Pictures nchini Marekani na wakuu wake nchini Japan watahitajika kuamua iwapo wataonyesha filamu ya uchesi yenye utata ya rais wa Korea Kazkazini Kim Jong-un. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na BBC
WAPIGA KURA WAHOFIA EBOLA LIBERIA
Idadi ndogo ya wapiga kura imeripotiwa kwenye kura ya kuwachagua maseneta nchini Liberia.
Kura
hiyo ilikuwa imeahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa
ebola na huenda hofu ya ugojwa huo iliosababisha watu kukosa kufika kwa
vituo vya kupigia kura.Wapiga kura walishauriwa kusimama umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine walipokuwa wakipanga milolongo kupiga kura baada ya viwango vyao vya joto kuchukuliwa na maafisa wa afya.
Kwenye taifa jirani la Guinea waandamanaji waliwazuia wafanyikazi wa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF kuweka kituo cha ebola kusini mwa nchi hiyo.
Polisi wanasema kuwa mahema yalichomwa na wafanyikazi wakafukuzwa na megenge ya vijana.
Jamii kwenye sehemu zingine za magharibi mwa afrika zilipinga jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zikihofia kuwa huenda zikapata maambukizi kutoka kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za afya. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na BBC
MOHAMMED ALI ALAZWA HOSPITALINI
Aliyekuwa bingwa wa ndondi ulimwenguni Mohammed Ali amelazwa hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya mapafu.
Ali ambaye ana umri wa miaka 72 na ambaye ana ugua ugonjwa wa Parkinson anadaiwa kuwa katika hali imara .Msemaji wake amesema kuwa ugonjwa huo uligunduliwa mapema.
Hatahivyo hakutoa maelezo zaidi na kutaka haki ya faragha ya familia ya bondia huyo mkwongwe kuheshimiwa.
Ali alipataikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984,miaka mitatu baada ya kuustafu katika masumbwi.
Alionekana hadharani katika sherehe moja mnamo mwezi Septemba nyumbani kwake Louisville Marekani wakati wa kutoa tuzo za kibinaadamu za bondia huyo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
REAL MADRID NDIO CLUB BINGWA DUNIANI
Kilabu
ya Real Madrid imeshinda taji lao la nne mwaka 2014 baada ya kuwashinda
mabingwa wa Marekani Kusini kutoka Argentina San Lorenzo katika fainali
la za kilabu bingwa duniani zilizochezwa nchini Morrocco.
Mabingwa
hao wa kombe la kilabu bingwa barani ulaya,Copa Del Rey na mabingwa wa
Super Cup barani Ulaya walianza kufunga kupitia kichwa cha Sergio Ramos.Makosa ya mlinda lango wa Lorenzo yaliihakikisha ushindi Real madrid baada ya Gareth Bale kuongeza bao la pili.
Real madrid hawakutatizwa na mabingwa hao wa Marekani kusini na hivyobasi kuongeza rekodi yao ya ushindi katika mecho zote kufikia 22.
Ushindi huo pia ni wa kwanza wa kilabu hiyo Bernabeu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Subscribe to:
Posts (Atom)