Saturday, November 22, 2014
CHAMA TAWALA ZAMBIA WAMTIMUA KAIMU RAIS CHAMANI
Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu wa katiba.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho.''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya chama,'' amesema Malozo Sichone.
Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi utakapofanyika tarehe 20 Januari.
Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MTOTO ALIYEKUFA KWA AJALI AZIKWA UGANDA
Shughuli
za mazishi ya mtoto wa miaka miwili zimefanyika nchini Uganda, mtoto
ambaye kifo chake kimezua ghadhabu baada ya mtoto huyo kugongwa na gari
la halmashauri ya jiji la Kampala ,baada ya mama yake kukamatwa akiuza
matunda kinyume cha sheria.
Familia ya Ryan Ssemaganda na
wanasiasa wa upinzani walitishia kutomzika mtoto huyo mpaka maofisa hao
watakapo wajibika kwa kitendo hicho.Mwili wake ulichukuliwa wakati
wakiandamana kuelekea bungeni siku ya alhamisi.Raia wa Uganda wanaona kuwa halmashauri hiyo inatumia nguvu nyingi kupambana na wachuuzi wa mitaani.
Mama wa mtoto Ryan alikamatwa siku ya jumatatu baada ya kukutwa akiuza matunda huku akiwa hana leseni.
Siku iliyofuata, Bibi wa mtoto huyo alimpeleka katika Ofisi za Mamlaka ya mji wa Kampala ambako mama mtoto alikuwa akishiliwa , nia ilikua kumpa mama mtoto ili amnyonyeshe.
Maafisa wa Ofisi hiyo walikataa na wakati wakijadiliana kuhusu hilo, mtoto alichoropoka kutoka kwa mama yake na kugongwa na gari linalomilikiwa na Mamlaka hiyo.
Siku ya Alhamisi polisi ilizuia kupelekwa kwa mwili katika Bunge, wakisisitiza mwili huo uzikwe ili marehemu apumzike kwa amani, na kuwataka waepuka jambo hilo kushughulikiwa kisiasa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MECHI ZA LIGI KUU UINGEREZA LEO JUMAMOSI
Mechi za Ligi kuu ya Uingereza siku ya jumamosi
Chelsea v West Brom18:00
Everton v West Ham18:00
Leicester v Sunderland18:00
Man City v Swansea18:00
Newcastle v QPR18:00
Stoke v Burnley18:00
Arsenaly v Man Utd 20:30
Mechi zote kuchezwa saa za Afrika Mashariki. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
WENGER: TULIJARIBU KUMSAJILI MESSI
Mkufunzi
wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kuwa kilabu hiyo
ilijaribu kumsajili nyota wa kilabu ya barcelona Lionel Messi kama
mpango wa kutaka kuwanyakua wachezaji watatu wachanga wa kilabu hiyo.
Messi alikuwa na miaka 15 wakati huo na mwenzake Gerrad Pique pamoja na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Cess fabregas.Wenger:''Tulitaka kumchukua Fabregas,Messi na Pique,lakini tukafanikiwa kumpata Fabregas pekee''.
Fabregas aliichezea kilabu ya Arsenal kwa miaka minane kabla ya kurudi Barcelona ,huku Pique akijiunga na Manchester United mwaka 2004.
Messi mwenye umri wa miaka 27,ameichezea timu ya Barcelona kwa muda wote na kuisadia kushinda mataji sita ya La liga pamoja na kombe la vilabu bingwa mara tatu baada ya mpango wa kujiunga na Arsenal kugonga mwamba.
Hatahivyo ,Wenger amepinga madai kwamba mpango huo ulifeli kutokana na makaazi ya Messi na familia yake.
Mchezaji huyo wa timu ya Argentina pia angelazimika kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza.
Wenger aliongezea:''Nadhani Messi mwenyewe hakutaka kujiunga nasi''. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Friday, November 21, 2014
NDERAKINDO AMKANA SAMUEL SITTA
Wakati Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akisema ofisi yake
imewakutanisha na kumaliza mgogoro baina ya wabunge wawili wa Bunge la
Afrika Mashariki (Eala), mmoja wa wabunge hao, Dk Nderakindo Kessy
amesema hakuna kitu kama hicho.
Dk Kessy jana aliripotiwa na vyombo vya habari
akidai kupigwa na mbunge mwenzake, Shy-Rose Bhanji, akisema
alisababishiwa maumivu makali, lakini likapingwa na Sitta. Jana, sakata hilo lilitinga bungeni na Serikali ikitakiwa kutoa maelezo kwa nini wabunge wa Tanzania wanafanya mambo ya ajabu.
Akijibu swali hilo, Waziri Sitta alisema ilitokea
bahati mbaya Bhanji kupitia CCM akamgonga Dk Kessy (NCCR-Mageuzi) na kwa
kuwa mbunge huyo wa chama tawala alikuwa na haraka kwenda kuwahi gari,
hakusimama, hivyo baadhi ya wabunge wa Uganda wakamshauri Dk Kessy
kwenda kuripoti tukio hilo polisi. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
NAPE: WAPUUZENI WAPINZANI
Wananchi wametakiwa
kupuuza kauli alizodai kuwa za wapinzani za kuwataka wasishiriki kupiga
kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Desemba,
mwaka huu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema hayo juzi alipozungumza na wakazi wa Nchingwea mkoani Lindi.
Alisema ni marufuku kwa vyama vya upinzani kuzuia wananchi kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayempenda
“Tumepata taarifa kuna wapinzani wameanza
kuwatisha wananchi wasiende kupiga kura siku ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa,” alidai Nape.
“Hizi ni salamu kwa wapinzani wenye mpango huo kuwa hatutawaacha, lazima tutawashughulikia.”
Alisema kupiga kura ni haki ya kila mwananchi,
hivyo kitendo cha kuzuia watu ni sawa na kubaka demokrasia, jambo ambalo
CCM haitalivumilia.
Nape alisema CCM imejipanga vizuri na kwamba ina uhakika wa kushinda kwa kishindo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
POLISI WABAKAJI WAONGEZEWA ADHABU
Polisi
wawili nchini Tunisia walioshitakiwa kwa kumbaka mwanamke ndani ya gari
la polisi, wameongezewa adhabu katika kesi iliyowashtua wengi.
Maafisa hao walifungwa jela mwezi Machi huku kukiwa na malalamiko kwamba adhabu hiyo haitoshi.Hukumu hiyo, iliongezwa hadi miaka 15 Alhamisi baada ya rufaa kuwasilishwa mahakamani na mwathiriwa wa kitendo hicho cha unyama Meriem Ben Mohamed.
Wakili wake alitaja hatua ya mahakama kuwoangeza adhabu watuhumiwa kama jambo zuri, na pia kusifu ambavyo kesi za ubakaji zinashughulikiwa nchini Tunisia.
Aliambia shirika la habari la AFP, kwamba ameridhishwa na adhabu hiyo.
"lakini bado haitoshi, kwa maoni yangu kwa tendo la kukera kama hilo,'' aliongeza kusema wakili huyo.
Meriem Ben Mohamed alishambuliwa mwaka 2012 na maafisa wa polisi waliosimamisha gari lake alimokuwa na mpenzi wake mjini Tunis. Alikuwa na umri wa miaka 27.
Watuhumiwa walikanusha mashitaka wakisema kuwa waliwapata wawili hao wakiwa wanashirki tendo la ndoa ndani ya gari lao.
Maafisa wa polisi walijaribu kuwashitaki Meriam na mpenzi wake kwa kosa la kukosa maadili lakini maandamano yalifanywa kupinga hatua kama hiyo huku wengi wakiwatetea wawili hao.
Ilisababisha Rais wa Tunisia kumsamehe Meriam na mpenzi wake.
Afisaa mwingine wa tatu aliyejaribu kuwatoza hongo wawili hao, atatumikia kifungo cha miaka miwili alichokuwa amepewa.
Ripoti iliyotolewa na mtaalamu wa kisaikolojia ilisema kuwa yote yaliyotokea yalimsababisha Meriam kusongwa na mawazo.
Kesi hii inatokea wakati ambapo kumekuwa na shinikizo kali kwa serikali kuzingatia haki za wanawake kufuatia kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali.
Na BBC
MKANYAGANO HATARI WAWAUA 11 ZIMBABWE
Watu 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufnayika katika uwanja wa soka.
Polisi wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano
huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani
humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter
Magaya.
Mhubiri huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza.
Baadhi ya walioshuhudia mkanyagano huo wanatuhumu polisi kwa kufunga
baadhi ya milngo ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka
kupitia mlango mmoja tu.
Hata hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.
Bwana Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and
Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya kutokea
vifo hivyo alihuzunika sana. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
RONALDO AOSHA VYOMBO BAADA YA KUSHINDWA
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
ADEBAYOR ADAI MAMAAKE NI MCHAWI
Mshambuliaji
wa kilabu ya Totenham nchini Uingereza Emmanuel Adebayor amekosana na
mamaake kwa madai kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.
Duru
zimearifu kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku
dadaake Adebayor akiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor
ndiye aliyemfukuza.Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.
'' Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na dadaangu wamekuwa wakijaribu kuniroga''aliwauliza maripota.Mchezo wa Adebayor katika kilabu ya Tottenham umeathirika katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita huku Tottenham ikidaiwa kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji huyo katika dirisha la uhamisho mnamo mwezi January kufuatia kushuka kwa mchezo wake.
Thursday, November 20, 2014
OBAMA KUTANGAZA MABADILIKO YA UHAMIAJI
Ikulu
ya Marekani imesema Rais Obama atatumia muda ambao watazamaji wa
televisheni nchini humo wanaangalia zaidi matangazo siku ya Alhamisi
kutangaza mabadiliko makubwa ya mfumo wa uhamiaji wa nchi hiyo.
Inatarajiwa
kuwa Rais Obama atasema kuwa atatumia madaraka yake aliyopewa kikatiba
kuzuia wahamiaji wapatao milioni tano kurejeshwa makwao na badala yake
wapatiwe vibali vya kufanya kazi nchini humo.Rais Obama amesema hayo katika video iliyotumwa katika ukurasa wa facebook kabla ya hotuba yake.Tangu kuingia madaraka Obama amekuwa akipigania baadhi ya mabadiliko ikiwemo huduma ya utoaji wa huduma za afya kwa mfumo wa bima ya afya. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
BINTI AJINASUA NA NDOA YA MWANAMGAMBO
Mwanamke
mmoja raia wa Uholanzi amewasili nchini Uturuki baada ya safari
iliyojaa hatari nchini Syria kwa ajili ya kumchukua binti yake aliyekua
mjini Raqqa, mji unaokaliwa na waasi wa Islamic State.
Monique
alikwenda Uturuki mara ya kwanza baada ya binti yake aitwae Aicha
kusafiri kwenda Syria kuoana na mmoja wa wanamgambo wa kundi hilo mwenye
asili ya Uholanzi na Uturuki.Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la IS.
Aicha ,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na IS.Raia wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria Mwezi Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)