Tuesday, March 20, 2018
Monday, March 19, 2018
PICHA ZA RAIS MAGUFULI AKIENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
Sehemu ya Viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
Viongozi wa wa taasisi mbali mbali katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
Ujumbe wa Umoja wa nchi za Ulaya (EU) katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz
Sunday, March 18, 2018
RAIS MWANAMKE PEKEE AFRIKA AJIUZULU
Rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim.
AMEENAH Gurib-Fakim rais wa Mauritius amejiuzulu urais baada ya kuelekezewa tuhuma za ufisadi kwa kutumia kadi ya malipo; awali alisema hatajiuzulu.
Baada ya kung’atuka madarakani kwa rais Sirleaf Johnson wa Liberia, huyu ndiye alikuwa mhimili wa wanawake Afrika kujishikilia kwa kusema "tuna Rais mwanamke" lakini sasa madai ya ufisadi yanaelekea kumtega.
Amehusishwa na kashfa ya kutumia kadi ya benki ambayo alikuwa amekabidhiwa na wahisani ya kufadhili ununuzi wa misaada kwa raia wake kujifaa yeye mwenyewe.
Kitita alichokigeuza kuwa chake ndani ya kadi hiyo kinasemwa kuwa makumi ya maelfu ya dola za Kimarekani.
Alijitetea kuwa hakufanya lolote baya na kwamba amerejesha pesa ambazo amedaiwa kujifaa nazo, hivyo basi kuweka swali wazi kuhusu "utarejesha nini ikiwa hukuiba".
Gurib-Fakim akiwa ni mwanasayansi tajika, alipaa hadi uongozi wa Mauritius mwaka wa 2015, ingawa ni wadhifa ambao hauna mamlaka yale ya viongozi wengine wa Afrika. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz
Monday, March 12, 2018
CHAMA TAWALA NCHINI CHINA CHAIDHINISHA 'RAIS WA MAISHA'
Chama tawala cha National People's Congress nchini China, kimeidhinisha marekebisho ya kipengee cha katiba, ya kufutilia mbali uongozi wa mihula miwili kwa Rais wa nchi hiyo.
Hatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023 na kuendelea kuongoza kwa kipindi kisichojulikana.
Wakosoaji wameonya kuhusiana na hatari ya kuondoa muda wa mihula miwili ya uongozi wa Rais, ambayo ililetwa na Deng Xiaoping mwaka 1982.
Friday, March 09, 2018
TRUMP AKUBALI MUALIKO WA KUKUTANA NA RAIS WA KOREA KASKAZINI
Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu, na hivyo kuweka historia kufuatia kuwa kutokuwepo rais wa Marekani ambaye amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini.
Hata hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa, na pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim Jong Un laini bado vikwazo vitasalia pale pale.
Tangazo hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un, limetolewa na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini.
KENYATTA, ODINGA WAKUTANA IKULU, WAKUBALIANA JAMBO
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo Raila Odinga katika ofisi yake Jumba la Harambee, Nairobi.
Mkutano huo umefanyika muda mfupi kabla ya Bw Kenyatta kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson.
Marekani imekuwa ikihimiza kufanyika kwa mazungumzo na mashauriano kutatua mzozo wa kisiasa uliokumba taifa hilo baada ya uchaguzi uliojaa utata mwaka jana.
Mkutano huo umefanyika muda mfupi kabla ya Bw Kenyatta kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson.
Marekani imekuwa ikihimiza kufanyika kwa mazungumzo na mashauriano kutatua mzozo wa kisiasa uliokumba taifa hilo baada ya uchaguzi uliojaa utata mwaka jana.
Thursday, February 22, 2018
MAANDAMANO YAWAPONZA CHADEMA, MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AWALIMA BARUA NZITO...!!!
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii leo Februari 22, 2018, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema barua hiyo ya msajili waliipokea jana na wanapaswa kuijibu kabla ya Februari 25, 2018.
Sunday, February 18, 2018
MTULIA, DR. MOLLEL WAREJEA BUNGENI UPYA
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni amemtangaza mgombea wa CCM, Mtulia Maulid kuwa Mbunge mteule wa jimbo hilo.
Mgombea
huyo ameongoza kwa kura 30, 247 akifuatiwa na Mwalimu Salum wa CHADEMA
kwa kura 12,353, Rajab Salum wa CUF kwa kura 1,943 na Ally Abdallah wa
ADA-Tapea mwenye kura 97.
“Nashukuru waliojitokeza kufanya
haki yao ya kidemokrasia, pia nawashukuru Tume ya Uchaguzi kwa umakini
waliouonesha kuhakikisha tumefanya uchaguzi na kumaliza salama,
kushindwa ndio kawaida ya ushindani.” Mtulia Maulid
Mkoani Kilimanjaro, NEC imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi katika jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake, Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.
Mkoani Kilimanjaro, NEC imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi katika jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake, Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.
WAZIRI NCHEMBA AAGIZA WAKIMBIZI WA BURUNDI 32,000 KURUDISHWA KWAO
Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza UNHCR kuwaondoa wakimbizi 32,000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.
Waziri Dr Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ikishaagiza vifungwe mala moja.
Dr Mwigulu amesema shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR wao wanafanya kazi masaa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini kwao.
Friday, February 16, 2018
HII HAPA LYRICS YA WIMBO MPYA WA PAPII KOCHA
Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz tu-follow instagram @jambotz. YouTube channel @jambotz.
NIGERIA WAZINDUA NDEGE ISIYO NA RUBANI
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amezindua ndege inayojiendesha yenyewe bila ya rubani ambayo ni ya kwanza kutengenezwa nchini humo.
Kifaa hicho kilichotengenezwa na Taasisi ya Teknolojia ya jeshi la anga la Nigeria, kitatumika kupambana na wapiganaji pamoja na majambazi.
Mipango ya jeshi la nchi hiyo ni kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi na pia uwezekano wa kuvisafirisha katika nchi nyingine.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na kitisho cha usalama, ikiwemo wapiganaji wa kiislamu walioko kaskazini mwa nchi hiyo, wapiganaji walioko katika eneo lenye utajiri wa mafuta, kusini mwa nchi na mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la kati mwa nchi hiyo
Thursday, February 15, 2018
RAIS WA AFRIKA KUSINI AJIUZULU...!!!
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake.
Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.
Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.
ZARI AMMWAGA DIAMOND SIKU YA WAPENDANAO
Katika siku ya wapendanao, jana Februari 14, 2018, Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady ametangaza kuvunja rasmi mahusiano yake ya kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kupitia ukurasa wake wa Instagaram, Zari amefunguka kuwa kilichompelekea kufanya hivyo ni kutokana na Diamond kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao huku akibainisha kuwa kuachana katika mahusiano ya kimapenzi hakutaathiri uhusiano wao kama wazazi.
Diamond ambaye alianza mahusiano na Zari takribani miaka mitano iliyopita baada ya kuachana na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu, amezaa na Zari watoto wawili ambao ni Tiffah na Nilan huku pia akitajwa kuchepuka jambo ambalo limepelekea akazaa mtoto mwingine na mwanamitindo Hamissa Mobeto.
Mbali na Mobeto, Diamond amekuwa akihusishwa kurudiana na Wema ambapo hivi karibuni walionekana kugandana kwenye hafla ya kutambulishwa kwa msanii Mbosso kwenye lebo ya WCB Wasafi.
Bado haijathibitika moja kwa moja iwapo kweli wameachana ama ni kiki kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanya.
Subscribe to:
Posts (Atom)