SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza kubomoa jengo la iliyokuwa
Klabu Bilicanas na ofisi za Free Media inayomiliki gazeti la Tanzania
Daima zinazomilikiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, lililopo makutano ya barabara
ya Mkwepu na Indira Gandhi lenye kitalu namba 725-726/24 na hati namba
C. T No. 186018/15 and C. T No. 186018/10.
Ubomoaji huo ulioanza jana unafanyika wakati Mbowe ameingia katika mgogoro na NHC baada ya kampuni ya udalali ya Poster and General Traders kumtolea vyombo nje mwanzoni mwa Septemba, mwaka jana kwa kudaiwa Sh bilioni 1.2 ambayo ni deni la pango ya miaka 20.

Gazeti hili lilishuhudia ubomoaji huo ukiwa katika hatua za awali na baadhi ya vijana walionekana wakianza kuondoa vioo na vigae vilivyoezekwa katika jengo hilo wakiwa chini ya usimamizi wa walinzi.
Hata hivyo, walipoulizwa watu waliokuwa wakisimamia katika eneo hilo walidai kuwa ubomoaji huo ni wa kawaida na ulipangwa kufanyika muda mrefu na endapo waandishi watahitaji maelezo wawasiliane na uogozi wa NHC.