Saturday, January 07, 2017

NANA AKUFO ADDO AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA GHANA

Nana Akufo-Addo akila kiapo wakati akiapishwa 
 
Viongozi kadha wa Afrika leo wamekusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za kutawazwa rais mpya, Nana Akufo Addo.

Maelfu ya wageni walialikwa kwenye sherehe katika Medani ya Uhuru mjini Accra. Bwana Akufo Addo, aliyewahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu, alimshinda Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Madaraka yanakabidhiwa kwa kiongozi mwengine kwa salama, jambo linaloonekana kuwa mfano mwema wa demokrasi Afrika ambako katika baadhi ya nchi, viongozi hawataki kun'gatuka.

Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani. Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...