Monday, July 13, 2015

KAMBI YA JESHI YAPOROMOKA YAUA 23

Takriban wanajeshi 23 wa Urusi wameuawa karibu na mji wa Omsk ulioko Siberia baada ya jengo la kambi ya kijeshi kuporomoka.

Wanajeshi wengine 19 waliokolewa kutoka kwa vifusi vya jengo hilo.
Mwanajeshi mmoja aliyeokolewa ameileza runinga ya Urusi kwamba wanajeshi walikuwa wamelala wakati wa ajali hiyo.

Picha za televisheni zilionyesha sehemu ya jengo hilo la ghorofa nne likiwa limeharibika kabisa huku wanajeshi wakishirikiana kuondosha vifusi.

Mwandishi wa BBC Moscow amesema inadhaniwa kwamba ukarabati duni uliofanyika mwaka jana ndio uliosababisha kuporomoka kwa jengo hilo. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

MAN CITY YAKUBALI KUMUUZA STERLING KWA LIVERPOOL


Raheem Sterling
Klabu ya Manchester City ya Uingereza imekubaliana na wapinzani wao Liverpool dau la pauni milioni £49 kumsajili mshambulizi Raheem Sterling.
Uhamisho wa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa unategemea makubaliano baina yao na vipimo vya afya. Sterling alikuwa ameomba kundoka Anfield kabla ya klabu hiyo kukataa dau mbili za Man City mwezi Juni.

Mshambulizi huyo atakuwa mchezaji aliyegharimu pesa nyingi zaidi raia wa Uingereza baada yake kukatalia mbali mshahara wa pauni laki moja kwa juma kutoka Liverpool.
Sterling aliyejiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 15 kutoka QPR mwezi februari mwaka wa 2010 yuko katika kandarasi inayokamilika mwaka wa 2017. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

VAN PERSIE ATUA UTURUKI


Van Persie akipokelewa Uturuki
Mashabiki wa manchester United wengi walijua kuwa Van Persie anaondoka kuelekea Fenabashe lakini kwa mtoto mdogo mwingereza wa miaka minne Louis Diamond hakufahamu kuwa kipenzi chake Robin Van Persie anaondoka mpaka pale alipoambiwa na wazazi wake kwamba mpachika magoli Robin alikuwa tayari kuelekea uturuki. 

Hivi sasa waturuki wameanzisha kampeni ya kuchangishana pesa ili mtoto huyo ambaye video yake imesambaa mitandaoni na kutizamwa na watu wengi aletwe Uturuki kumshuhudia mchezaji huyo. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

Friday, July 10, 2015

MAPINDUZI MENGINE YAANDALIWA BURUNDI

Rais Pierre Nkurunziza
Mmoja wa viongozi katika mapinduzi yaliyozimwa nchini Burundi hivi karibuni ya kumpindua Rais Piere Nkurunziza ameiambia BBC kuwa waasi wao wamekuwa wakiwapa mafunzo polisi na askari kwa ajili ya jaribio jingine la kumwondoa rais Pierre Nkurunziza.

Akiwa uhamishoni Generali Leornard Ngenda Kumana amekanusha kuwa walisaidia na mataifa ya nje. Wamekuwa wakimshutumu Rais Nkurunziza kuwa kusababisha vurugu kaati ya jamii ya wahutu na watutsi na kuwapa silaha wapiginaji wa vijana waoiunga mkono serikali ambao wanaonekana wengi ni kutoka jamii ya wahutu.

Zaidi ya watu laki moja wamekimbia nchi hiyo wakihofia vurugu wakati wa uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Wanaompinga wanasema hatua ya kugombea urais kwa muhula wa tatu kwa rais huyo ni kinyume cha katiba. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

KIKWETE: "NILIACHA KUANGALIA MPIRA ILI NISIONEKANE NINA MKOSI"


Raisi Kikwete akipeana mkono wa mchezaji wa zamani wa Real Madrid walipoitembelea Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema aliacha kwenda uwanjani kuiangalia timu ya taifa Stars kwa kuwa alionekana kuitia mkosi wa kufungwa timu hiyo kila ilipocheza.

Akiongea wakati wa kuvunja bunge na kuwaaga wabunge, Rais Kikwete alisema zamani alihudhuria sana mechi za Stars na baada ya kuonaa inafungwa mara kwa mara, aliamua kuacha kwenda uwanjani .

“Mwanzoni nilikuwa navaa hadi jezi kuishangilia timu yetu ilipokuwa inafanya vizuri, tulipoanza kufungwa fungwa wakasema mzee unaitia timu mkosi, nikaamua kuacha”, alisema Rais Kikwete huku akicheka katika hali ya mzaha.

Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

FIFA YATAJA VIWANGO VYA UBORA, TANZANIA YASHUKA

Tanzania na Uganda zimeshuka katika viwango ya FIFA vilivyotolewa Alhamis huku Kenya, Sudan na Rwanda zikipanda.

Uganda, ambayo ilikuwa nafasi ya 71, imeshuka nafasi mbili na sasa ni ya 73 wakati Tanzania, imeshuka nafasi 12 na sasa ni ya 139.

Licha ya kushuka, Uganda, ambayo hivi karibuni imeitoa Tanzania katika kugombania nafasi ya kucheza fainali za CHAN mwakani nchini Rwanda, ndio nchi iliyo juu katika viwango vya FIFA kwa nchi za Afrika ya Mashariki.

Kushuka kwa Tanzania kunatokana na kufungwa na Uganda 4-1 katika michuano ya CHAN na kufungwa na Misri 3-0 katika mechi ya kwanza ya kugombania kufuzu kucheza fainali za AFCON.
Kenya imepanda nafasi saba na sasa ni ya 116 katika viwango hivyo ya Dunia. Rwanda ipo nafasi ya 78, ikipanda nafasi 16 wakati Sudan ikiwa nafasi ya 90, ikipanda nafasi 18. Burkina Faso (72), Botswana (120) na Comoros (187).

Algeria ndio timu inayoongoza katika viwango vya FIFA kwa Afrika ikiwa nafasi ya 19. Timu ya Agentina, licha ya kufungwa na Chile katika fainali za Copa America, imepanda na kuwa timu ya kwanza katika viwango va FIFA, ikiitoa Ujerumani. Tano bora za viwango vya FIFA ni Argentina, Germany, Belgium, Colombia na Uholanzi.

Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

Monday, July 06, 2015

RUTO "KENYA HAITARUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA"

Naibu rais wa Kenya Mh. William Ruto ameonya kuwa ndoa za jinsia moja ni haramu na kuwa hazitawahi kuruhusiwa nchini humo.

Ruto amechukua msimamo huo mkali siku chache tu kabla ya ziara wa Marekani Barrack Obama nchini Kenya.

Friday, June 26, 2015

KAFULILA AKOMALIA MABEHEWA FEKI

Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila.

MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR Mageuzi) ameitaka Serikali kuwasilisha bungeni taarifa ya kashfa ya ununuzi wa mabehewa feki katika Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kusababisha hasara ya Sh bilioni 230. 

Baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni jana, mbunge huyo alisimama kuomba muongoza wa Spika kwamba kutokana na unyeti wa jambo hilo, ikiwa ni pamoja na madai kwamba Kampuni iliyopewa zabuni ya kuagiza mabehewa hayo haikuwa na uwezo huo, kwa nini suala hilo lisipelekwe bungeni kujadiliwa.

WATOTO WALIWA NA FISI

Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.

Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala.

AL-SHABAAB YASHAMBULIA KITUO CHA AMISOM

Kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom. 

Takriban watu 30 wamepoteza maisha yao baada ya shambulizi la kigaidi katika kituo cha kijeshi cha wanajeshi wa kimatifa wa kulinda amani nchini Somalia Amisom.

Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga aliendesha gari lake moja kwa moja hadi kwenye lango kuu la kituo hicho .

Kituo hicho kiko katika eneo la Leego, barabara kuu inayounganisha mji mku wa Mogadishu na Baidoa.

BURUNDI KUENDELEA NA RATIBA YA UCHAGUZI

Gervais Rufyikiri aliyekuwa makamu wa rais wa Burundi amekimbilia Ubelgiji. 

Serikali ya Burundi imesema haitashiriki katika mazungumzo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakilenga kupunguza hali ya uhasama uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenye utata.

MKWASA AWAOMBA MASHABIKI WA SIMBA WASIMZOMEE

Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Taifa Stars, Charles Mkwasa.

KOCHA mpya wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amewataka mashabiki wa Simba kutomzomea pindi watakapomuona kwenye mazoezi au mechi, kwa vile atakuwa pale kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya wachezaji wake wa timu ya taifa. 

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mkwasa alisema mashabiki wanatakiwa kufahamu kuwa yeye ni kocha wa taifa, hivyo atakuwa akitembelea katika mechi za timu mbalimbali kuangalia wachezaji na maendeleo ya wale wanaocheza timu ya taifa.

“Mashabiki wa Simba mnaponiona kwenye mechi zenu msinikimbize kwa mawe mkadhani kuwa nimekuja kwa ajili ya Yanga, nitakuwa na utaratibu wa kutembelea timu kuangalia wachezaji, mnajua kazi ya kocha wa taifa ndio hiyo,” alisema Mkwasa ambaye pia ni Kocha Msaidizi wa Yanga.

TAMBWE AIPANIA KAGAME

Amissi Tambwe

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe amesema anategemea kufanya vizuri zaidi katika michuano ijayo ya Kagame kuisaidia timu kuchukua taji katika michuano hiyo itakayofanyika nchini kuanzia mwezi ujao. 

Tambwe, ambaye aliwahi kufanya vizuri katika michuano hiyo iliyofanyika Sudan miaka miwili iliyopita kwa kuibuka mfungaji bora, aliliambia gazeti hili kuwa anajipanga kufanya vizuri zaidi.

Mchezaji huyo aliibuliwa na Simba katika michuano hiyo wakati akiichezea Vital’O ya Burundi iliyochukua ubingwa wakati huo, kutokana na kuisaidia timu yake kwa kiasi kikubwa na kufanya vizuri.

ENGLAND YATETEA WACHEZAJI CHIPUKIZI

Timu ya England U21 katika moja ya michezo yao ya michuano ya Ulaya

England imefanya uamuzi sahihi kuwaondoa katika michuano ya ubingwa wa Ulaya kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 21, baadhi ya wachezaji wake ambao wanacheza ligi kuu ya nchi hiyo, amesema mkurugenzi wa chama cha soka wa maendeleo ya wachezaji Dan Ashworth.

Timu ya England chini ya kocha Gareth Southgate ilifuzu kucheza hatua ya makundi kwa kwenda Jamhuri ya Czech. "Tulifanya uamuzi na nautetea ," Ashworth amemwambia mwandishi mwandamizi wa BBC wa habari za mpira wa miguu Ian Dennis. 

"Timu za vijana zipo kusaidia kuwakuza wachezaji na kuwapa uzoefu kuingia katika timu ya wakubwa." Mchezaji wa ushambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, kiungo wa Everton Ross Barkley, viungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Jack Wilshere na mlinzi wa Manchester United Phil Jones ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakihitajika katika timu hiyo, lakini hawakuitwa.

England, ambayo ilikuwa na wachezaji wa ligi kuu, akiwemo mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, mlinzi wa Everton John Stones na mshambuliaji mpya wa Liverpool Danny Ings, ilipoteza kwa Ureno 1-0 , wakaifunga Sweden kwa idadi kama hiyo lakini ilipoteza 3-1 kwa Italia.

Wednesday, June 24, 2015

WAZIRI GHASIA, KAFULILA WATOFAUTIANA BUNGENI

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila 

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia jana walitofautiana bungeni kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Hadija Nyembo.

Tukio hilo lilitokea baada ya swali la nyongeza la mbunge huyo, aliyetaka kujua msimamo wa serikali kuhusu Nyembo aliyedai kutoa kauli ya kutaka Wabembe waende kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) iliyosababaisha Wabembe kukamatwa na kupelekwa ubalozini, ambapo ubalozi wa DRC , uliwakataa na kusababisha wanyanyasike kwa karibu wiki mbili. 

Pia Mbunge huyo alidai Mkuu huyo wa Wilaya aliondolewa wilayani Chato akihusishwa na ufisadi wa mbolea yenye thamani ya Sh bilioni 1.5 na kwamba sasa ana kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Chato, hivyo serikali haioni aibu kuwa na Mkuu wa Wilaya wa aina hiyo, ambaye anashitakiwa na serikali yenyewe.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...