
Alama Kante afanyiwa upasuaji
Mwimbaji huyo Alama Kante, ambaye ni raia wa Guinea anayeishi Ufaransa alipewa dawa za kumfanya asihisi uchungu wakati upasuaji huo ukiendelea. Kante alikua na hofu kuhusu kupoteza sauti yake kutokana na upasuaji huo lakini daktari wake akapendekeza aimbe huku akipasuliwa ikiwa ni mara ya kwanza hatua kama hiyo kuwahi kuchukuliwa kote duniani.
Profesa Giles Dhonneur, aliyeongoza upasuaji huo katika hospitali ya Henri Mondor hospital, ameonyesha video ya mwanamziki huyo akiimba huku naye akiendelea na upasuaji. Ameelezea matuamani kuwa mambo yatakuwa sawa.
Amesema ni uchungu sana kufanya upasuaji kama huo bila kutumia dawa ya kumfanya mgonjwa asihisi uchungu lakini mbinu na dawa aliyotumia ilimuwezesha Kante kuhimili bila matatizo yoyote.
Kante ambaye amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na alipoamka na kuzungumza tena madkatari na wauguzi walifurahi sana kutimiza lengo lao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz





Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisistiza jambo wakati akizungumza na msanii
wa kizazi kipya Nasib Abdul “Diamond” ikulu ndogo mjini Dodoma wakati
chakula cha usiku alichowaandalia wasanii walioshiriki katika tamasha la
Uzalendo na Uzinduzi wa Video ya wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika uwanja wa michezo wa
Jamhuri mjini Dodoma jumamosi.Kulia ni mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani
Kikwete.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na msanii wa kizazi kipya 


















