Wednesday, June 11, 2014

UMRI WA KUISHI WAONGEZEKA...!!!

Wastani wa umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kutoka miaka 50 kwa sensa iliyofanywa mwaka 1988 hadi kufikia miaka 61 kwa sensa ya mwaka 2012.
Akiwasilisha taarifa za msingi za kidemografia, kijamii na kiuchumi kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini hapa jana, mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa alisema wanawake wanaishi umri mrefu zaidi kuliko wanaume.
“Matokeo haya yameendelea kuonyesha wastani wa umri wa kuishi kwa wanawake ni miaka 63 ambao ni mkubwa zaidi ukilinganisha na wanaume ambao ni miaka 60. Tunaamini ongezeko hilo limetokana na kukua kwa uchumi na kupungua kwa umaskini wa kipato.”
Akizungumzia kuhusu matokeo ya awali ya uzazi kwa sensa ya mwaka 2012, alisema inaashiria kupungua kwa kiwango cha uzazi kutoka wastani wa watoto 6.5 mwaka 1988 hadi kufikia watoto 5.2.
“Hii inaweza kuwa imesababishwa kuongezeka kwa umri wa kuolewa katika umri wa kuanzia miaka 22 wakati wanaume wamebainika kuwa huoa kuanzia miaka 24 na kuendelea,” alisema.
Alisisitiza kuwa inawezekana matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango na kuongezeka kwa kiwango cha elimu kwa wanawake ni sababu zinazowafanya waishi zaidi. Akizindua taarifa hiyo, Rais Jakaya Kikwete aliwapongezawalioshiriki kukusanya taarifa hizo na kuzichanganua, akieleza kwamba ni miongoni mwa shughuli ngumu kwa kuwa kuna udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Taarifa hizi zimechambuliwa vyema na zitasaidia kupanga masuala ya maendeleo. Idadi yetu inazidi kuongezeka pia. Mwaka 2012 tulikuwa milioni 44, pengine hadi mwaka 2016 tutakuwa milioni 48,” alisema.
Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...