Juhudi za uokoji zinaendelea
siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao
elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika
maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa
wa karibu mita kumi kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja
kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo TzSunday, May 04, 2014
Saturday, May 03, 2014
MWENGE WA UHURU WAWASHWA RASMI JANA MKOANI KAGERA,TAYARI KUKIMBIZWA KATIKA WILAYA 127
Makamu
wa Rais wa, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa
Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa
Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo. Mwenge huo unatarajia kuitimisha
mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu
wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa
mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kuuwasha rasmi wakati wa Sherehe
za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini
Bukoba Mkoa wa Kagera jana. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
ABSALOM KIBANDA AFUNGUKA NDANI YAMAANDIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI
Baadhi ya waandishi wa habari na
wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano
la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari
Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari
nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na
kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
Kibanda aliyasema hayo
jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya
maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza
kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na
kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili
unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.
“Baadhi ya wahariri
huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa
uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu
moja kwa moja,” alisema Kibanda.
Aliongeza kwa kusema
kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na
kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa
kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea
kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
POLISI NIGERIA WAOMBA PICHA ZA WANAFUNZI
Polisi nchini Nigeria wamewataka wazazi wa wanafunzi wasichana zaidi ya 200 waliotekwa kuwasilisha picha za mabinti hao.
Wasichana hao walichukuliwa na watu wanaoshukiwa
kuwa wanamgambo wa Kiislam kutoka shuleni kwao katika jimbo la Borno
zaidi ya wiki mbili zilizopita.Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
WATU 30 WAFA KWA MOTO VITANI UKRAINE
Polisi wa Ukraine wanasema kuwa
zaidi watu 30 wameuawa katika moto ulioanza baada ya makabiliano kati ya
vikosi vya wanamgambo wanaounga mkono Urusi na wafuasi wa serikali
katika mji wa kusini magharibi wa Odessa.
Haijulikani ni nini kilichosababisha moto huo
katika jengo la chama cha wafanyikazi ,huku ripoti zikiarifu kwamba
pande zote mbili zilikuwa zikitumia mabomu ya petroli."Waziri wa mpito wa Mambo ya Ndani nchini Ukraine Arsen Avakov amesema kuwa harakati za serikali kudhibiti mji wa mashariki wa Sloviansk uliopo mashriki mwa Ukraine zinaendelea na kwamba vikosi vyake vimeliteka jengo la Televisheni karibu na Kromartosk." Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Friday, May 02, 2014
JK: MISHAHARA ITAPANDA NA KUPUNGUZWA KODI
Rais
Jakaya Kikwete akiangua kicheko wakati walimu (juu), walipokuwa wakipita
kwa maandamano, huku wakiimba ‘Shemeji mshahara bado’ wakati wa sherehe
za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) zilizofanyika Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam jana. Walimu walimwita shemeji kwa kuwa mkewe, Salma ni
mwalimu kitaaluma. Picha na Silvan Kiwale.
Dar/mikoani. Rais
Jakaya Kikwete ametoa ahadi mbili za kuwafurahisha wafanyakazi. Kwanza
ametangaza nia ya kuongeza mishahara yao na pili, kupunguza kodi
inayokatwa kwenye mishahara hiyo mambo ambayo ameahidi kutekelezwa
katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi
karibuni.
Akizungumza
kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika
kitaifa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema anatambua kuwa
wafanyakazi wana hamu ya kujua Serikali itasema nini kuhusu masilahi
yao.
Alisema
malalamiko ya wafanyakazi wengi ni kutaka kuona kima cha chini cha
mshahara kinaongezwa huku kodi kwenye mishahara (Paye), ikipungua.
“Mimi na
wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo,
tumethibitisha miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Huku
akishangiliwa na wafanyakazi waliofurika katika Uwanja wa Uhuru, Rais
Kikwete alisema: “Najua kuwa nyongeza tuliyotoa mwaka jana si kubwa kama
wafanyakazi walivyotaka iwe... hata mimi nisingependa iwe hivyo.”
HII NDIO TAARIFA RASMI YA YANGA KUHUSU USAJILI WA DOMAYO NA KAVUMBAGU
Uongozi
wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi
wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake
Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC
zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani
walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga
kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba
ramba.
Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama
kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika
wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio
watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu
zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao
tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba
yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao
2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni
waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya
kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo
yote ya msingi kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya
usajili wa wachezaji wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la
Bagamoyo linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
HAMAD RASHID KUGOMBEA URAIS 2015
Mbunge
wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed amesema anapanga kujitosa kwenye
kinyang’anyiro cha urais katika Uchaguzi Mkuu mwakani.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu hivi karibuni mjini Dodoma, Hamad Rashid
alisema: “Kama Mwenyezi Mungu akinijalia uhai na uzima mwakani,
ninatarajia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais ama wa Muungano au
wa Zanzibar.
“Ila sijaamua kama ni Bara au Zanzibar; kama ni chama cha CUF au kingine, hayo yote yatakuja baadaye,” alisema Hamad Rashid.
Mohamed
ambaye ana mgogoro mahakamani na chama chake cha CUF, ametoa kauli hiyo
wakati tayari viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), CUF
kikiwamo wanajipanga kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi
ujao.
Mbali na
CUF, vyama vingine vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi na Chadema ambavyo
pia vinakusudia kusimamisha mgombea mmoja kwa nafasi za ubunge na
udiwani, lengo likiwa kukabiliana na nguvu ya chama tawala, CCM.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
WATU 19 WAUAWA KATIKA MLIPUKO NIGERIA
Maafisa nchini Nigeria wanasema
kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi
katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya
kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60
walijeruhiwa vibaya lakini sitaka kati yao wametibiwa na kuruhusiwa
kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari sita yameharibiwa katika mlipuko
huo.Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa. Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja
Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Lakini shambulizi la bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Saturday, April 26, 2014
MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
Umati wa watu waliohudhuria
maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yanayoendelea hivi sasa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,
maonyesho haya yanajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo maonyesho.
Maadhimisho haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoaka mataifa
mbalimbali (Picha na Awadhi Ibrahim)
G7 YAZIDI KUIBANA URUSI...!!!
Viongozi wa nchi Saba tajiri kwa
viwanda duniani G7 wamekubaliana kuongeza vikwazo zaidi kwa Urusi
ambapo wamesema imezidi kuifanya Ukraine isitawalike.
Ikulu ya White House ya Marekani imesema
wataanza kuweka vikwazo hivyo haraka iwezekanavyo kuanzia siku ya
jumatatu na wanatarajia kulenga biashara za binafsi na ambazo zina
uhusiano na Rais Vladimir Putin wa Urusi.Wametoa wito kwa Urusi kuacha mipango yake kijeshi ya siri kwenye mpaka na Ukraine.
Kwa upande mwingine viongozi hao wa nchi saba tajiri duniani wameisifu Ukraine kwa jinsi walivyojizuia kwa kupanda na wapiganaji waasi.
Serikali ya Ukraine imesema inahofia kuwa Urusi ina mipango ya kuivamia. Hata hivyo Urusi imesema nchi za magharibi zina mipango ya kuteka kuitawala nchi yao.
HAKUNA KATIBA BILA UKAWA...!!!
Na Hudugu Ng'amilo
MWANASIASA
mkongwe na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Kingunge Ngombale –
Mwiru, amesema makada wenzake wanaomshambulia aliyekuwa Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, wanakitukana Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema
kumtukana au kumshambulia Jaji Warioba, au wajumbe wengine wa tume hiyo
ni sawa na kukitukana Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongoza serikali.
Kingunge
alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akichangia sura ya kwanza na ya
sita ya rasimu ya Katiba, ambapo alisema wanaomshambulia Jaji Warioba
wanaonyesha utovu wa adabu, kwa kuwa chama kina maadili na adabu katika
kushughulikia masuala mbalimbali.
"Mimi
sitakubali hata kidogo wajumbe watumie msimamo wa chama kumshambulia
Warioba au wajumbe wengine wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, si
halali kumshambulia Warioba au mjumbe yeyote yule binafsi.
Subscribe to:
Posts (Atom)