Wizara
ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imepiga marufuku majina hamsini
ambayo yapo kinyume na tamaduni pamoja na dini ambapo kuanzia sasa,
wazazi kutoka falme hiyo hawataruhusiwa tena kuwapa watoto wao.
Majina hayo ni kama Linda, Alice, Elaine au Binyamin (jina lenye
maana Benjamin) ambapo jina la Benjamin (Binyamin) kwa dini ya kiislamu
linaaminika kuwa jina la mtoto wa mtume Jacob, yaani Yacoub kwa dini.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Mengine katika orodha hiyo ambayo hayatoruhusiwa ni kwa sababu
yanaaminika kuwa yenye kufuru, yasiyo ya kiarabu na yasio ya kiislamu au
yenye kupingana na tamaduni na dini ya falme hiyo.
Sababu nyingine ni ya kigeni ama ya ughaibuni yakiwemo yenye maana ya
ufalme au ukubwa, cheo flani kama Sumuw (mtukufu), Malek (mfalme) na
Malika (Malkia).
Majina
mengine hayapo katika jamii hizi hivyo hakuna sababu zilizotolewa juu
yake, hii ni sehemu nyingine ya orodha yenyewe ambapo ni Malaak (angel),
Abdul Aati, Abdul Naser, Abdul Musleh, Binyamin (Arabic for Benjamin)
Naris, Yara, Sitav.
Mengine ni Loland, Tilaj, Barrah, Abdul Nabi, Abdul Rasool, Sumuw
(highness), Al Mamlaka (the kingdom), Malika (queen), Mamlaka (kingdom),
Tabarak (blessed), Nardeen, Sandy, Rama (Hindu god), Maline, Elaine,
Inar, Maliktina
Maya.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz