Naibu Waziri wa viwanda nchini Libya
ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa ziarani mjini Sirte
Mashariki mwa Tripoli ambako alizaliwa.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema
kuwa watu wasiojulikana walimfyatulia risasi kadhaa Hassan al-Droui
karibu na soko rasmi mjini humo. Ni mauaji ya kwanza ya afisa wa serikali ya mpito ya Libya.
Libya imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu kuondolewa mamlakani kwa hayati Muammar Gaddafi mwezi Oktoba mwaka 2011. Sirte ilikuwa ngome ya mwisho ambako
mapigano yalitokea wakati wa harakati za mapinduzi ya Muamar Gaddafi
ambaye alikamatwa na kupigwa risasi akijaribu kujificha kutoka kwa
waasi.
Bwana al-Droui alikuwa mwanachama wa zamani wa baraza la mpito lililosimamia kipindi cha mpito baada ya Gadaffi kuuawa. Aliteuliwa kama naibu waziri na waziri
mkuu wa kwanza wa mpito na kuendelea kushikilia wadhifa huo hata baada
ya Ali Zeidan kuchukua mamlaka.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz