
Rais wa
mpito wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia, amejiuzulu
kufuatia shinikizo kali na kukosolewa kwa mwendo wake wa kujikokota
katika kusuluhisha mgogoro wa kidini unaotokota nchini humo.
Hatma ya Djotodia ilikuwa swala kuu katika ajenda ya mkutano wa viongozi wa kikanda kuhusu mzozo unaoendelea nchini humo. Taarifa zinazohusiana Afrika, Siasa
Mkutano huo ulifanyika nchini Chad huku maelfu wakiendelea kutoroka nchini humo kutokana na ghasia.
Maelfu ya watu waliandamana leo katika barabara za mji mkuu Bangui kumtaka Rais Djotodia, ajiuzulu.
Rais Djotodia amekosolewa vikali kwa
kukosa kumaliza mapigano ya kidini kati ya wakristo na waliokuwa waasi
waisilamu ambao walimsaidia kuingia mamlakani kwa njia ya mapinduzi
mwaka jana.
Baraza lote la mpito katika Jamuhuri
ya Afrika ya kati limekwenda nchini Chad ambako viongozi wa Afrika
wanakutana kujadili mzozo unaoendelea nchini humo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz