Tuesday, January 07, 2014

LIONEL MESSI KUNG'OKA BARCELONA KWA EURO 400 MILIONI

JEURI ya pesa. Ndicho unachoweza kusema baada ya klabu tajiri Ulaya, Paris Saint-Germain na Manchester City kudaiwa kuwa zipo tayari kumng'oa, Lionel Messi, kutoka Barcelona kwa gharama yoyote ile.
Wakati ikiwekwa wazi kwamba thamani ya supastaa huyo wa Kiargentina ni Euro 400 milioni, klabu hizo zinazomilikiwa na matajiri wenye pesa ndefu, zimesema zipo tayari.
Ripoti zinabainisha kwamba uamuzi wa kumfanyia tathmini Messi ili kufahamu thamani yake halisi, umefanywa mahususi na klabu hizo ili kufahamu itawagharimu kiasi gani ili kuipata saini yake. Kwa mtazamo wa kawaida anaonekana mchezaji huyo ni kama hanunuliki.
Kwa mujibu wa tathmini hiyo iliyofanywa na klabu tatu za Ulaya zenye pesa za kutosha, staa huyo wa Barcelona na mshindi mara nne wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (Ballon d'Or), thamani yake ya sasa inazidi kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake kwamba anaweza kuuzwa kwa Euro 250 milioni.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Profesa Gerardo Molina, aliyeandika ripoti kuhusu thamani ya mwanasoka huyo, alisema: "Kuna klabu zinazothaminishwa na serikali (zimeripotiwa kuwa PSG na Man City) zinajiandaa kulipa Euro 400 milioni kwa ajili ya Lionel Messi.
"Kuna klabu tatu za Ulaya zilituuliza sisi tufanye tathmini ya thamani ya mchezaji huyo ili kufahamu ni kiwango gani kinahitajika kumnasa Messi. Hatuwezi kuzitaja klabu hizo, lakini kitu ambacho zinataka ni kumhamisha Messi."
Molina aliongeza: "Messi soko lake ni mara tano ya Cristiano Ronaldo. Kwa tathmini iliyofanywa, Ronaldo thamani yake ni kati ya Euro 150 milioni na Euro 160 milioni. Mkataba wa Messi una kipengele cha Euro 250 milioni, lakini kiwango hicho hakikutazama thamani yake halisi.
"Kwa sasa hakuna mchezaji mwingine duniani mwenye thamani kubwa kuliko Messi. Kwa uchunguzi uliofanywa kwenye soka la usajili kwa miaka mitano, Messi thamani yake ni zaidi ya Euro 400 milioni."
Staa huyo juzi Jumapili alikuwa jukwaani wakati klabu yake ilipomenyana na Elche kwenye mchezo wa Ligi Kuu Hispania na Barcelona kushinda mabao 4-0, Alexis Sanchez akifunga 'Hat-Trick' kuisaidia timu hiyo kuendelea kuongoza msimamo wa ligi hiyo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...