ALIYEKUWA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Arcado Ntagazwa,
jana alijikuta akiangua kilio ndani ya kizimba, baada ya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu kutamka yeye na wenzake wawili wameachiwa huru.
Ntagazwa alitokwa na machozi, mbele ya Hakimu Mkazi, Geni Dudu, alipokuwa akisoma hukumu katika kesi ya kujipatia tisheti 5,000 na kofia 5,000 za kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mwaka 2009 kwa njia ya udanganyifu.
“Ukiangalia ushahidi hapakuwa na udanganyifu katika kuagiza kuchapwa kwa tisheti na kofia, waliamini wangeweza kulipa fedha hizi, ukiangalia uhalisia wa tisheti hazikuwa za kibishara… zilikuwa za kugawa bure kwa wananchi, zilikuwa kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa kupiga vita rushwa na ufisadi, zilikuwa kama mabango.
“Ni kweli washtakiwa walihujumiwa na kushindwa kulipia gharama za uchapishaji, tayari nina shaka hiyo inatosha sana kuwaona washtakiwa si wakosaji, shaka hata ikiwa ndogo kiasi gani manufaa yanakuwa kwa washtakiwa.
“Kutokana na ushahidi na vielelezo vilivyopo mahakamani, naona washtakiwa hawana kosa, wako huru, mlalamikaji akafungie kesi ya madai ili aweze kupata haki yake,” alisema Hakimu Dudu na kutamka washtakiwa wako huru.
Ntagazwa, alianza kujifuta machozi yaliyokuwa yakibubujika akiwa kizimbani na hata baada ya kushuka kizimbani aliendelea kububujikwa na machozi, huku akitembea taratibu mno kuelekea nje ya jengo la mahakama.
Hakimu Dudu kabla hajafikia uamuzi wa kuwaachia huru washtakiwa, alisema katika ushahidi hapakuwa na ubishi washtakiwa walichapisha tisheti na kofia, ushahidi huo unasapotiwa na vielelezo kwamba kampuni mbili zilikubaliana kuingia mkataba huo.
Alisema upande wa Jamhuri ulileta mashahidi watano mahakamani kuthibitisha mashtaka hayo na kuomba katika majumuisho ya mwisho, kwamba washtakiwa watiwe hatiani kwani waliweza kuthibitisha makosa yao bila kuacha shaka.