Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa
Umoja wa Afrika uliofanyika Ehiopia umetaka mahakama ya kimataifa ya
makosa ya jinai (ICC) huko The Hague icheleweshe kesi ya Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya, iliyopangwa kuanza kusikilizwa Novemba mwaka huu.
AU pia wamekubaliana azimio
linaloeleza kuwa hakuna kiongozi mkuu wa taifa la Afrika aliyeko
madarakani atakayefikishwa katika mahakama hiyo.
Wakati viongozi wa Kenya na Sudan
wakikabiliwa na kesi huko ICC, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa
wakilalamika kwa muda mrefu kuwa mahakama hiyo inafanya upendeleo na
kuwaonea kwa makusudi.
AU ilijadili uwezekano wa nchi wanachama kujitoa, lakini wazo hilo halikuungwa mkono kiasi cha kutosha.
Wanasiasa na wanadiplomasia waandamizi
akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan wamekosoa
mpango wa kujitoa kutoka ICC. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Kucheleweshwa
Viongozi hao wa AU, waliokutana Addis Ababa, walikubaliana kuwawekea kinga ya kutoshitakiwa kiongozi yoyote wa taifa la Afrika.
Pia wameitaka Kenya iandike barua kwa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiga kuomba ucheleweshwaji wa kesi
katika mahakama ya ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anakabiliwa
na mashtaka ya jinai.