Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Bariadi kwenye Viwanja vya
Sabasaba. Adai wamechukizwa na viwanda vya nguo,nyuzi ,nyama na ajira.
-Asema misaada ya China ni ukombozi mkubwa unaowakera Chadema.
-Awataka kanda ya ziwa kuujua unafiki huo wa Chadema.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya Chadema kukerwa na hatua za Balozi wa China na serikali ya China kwa ujumla katika kushiriki katika hatua za kuwakwamua watanzania katika umasikini.

Nape alisema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Bariadi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM sabasaba Mkoani Simiyu. Alisema hoja kuwa ambayo imewakera na kuwasumbua Chadema ni hatua zinazochukuliwa hivi sasa kwa pamoja kati ya Serikali ya CCM na Serikali ya China ambayo hivi sasa inaelekea kuzaa matunda ya kutoa mwanya wa ajira zaidi ya elfu- 25 viwandani.