Tuesday, September 10, 2013
VILIO VYATAWALA MSIBA WA MSANII WA FILAMU
Mama mzazi wa Malisa akiwa na uso wa huzuni.
Dada wa marehemu (wa tatu kushoto) akilia kwa uchungu baada ya msanii
wa filamu, Chuchu Hansi (aliyeinamisha kichwa) kuingia na kuangua kilio.
Wasanii wakongwe wa filamu, Devotha Mbaga na Vanitha wakilia kwa uchungu.
Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni.
VILIO
vimetanda msibani kwa msanii wa filamu za Kibongo, Zuhura Maftah
‘Malisa’ aliyefariki dunia jana akiwa hospitali ya Hindu Manndal
alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa.
Msiba wa msanii huyo upo nyumbani kwa dada yake Mikocheni na mazishi yatafanyika kesho makaburi ya Kinondoni.(Habari/Picha: Gladness Mallya na Hamida Hassan / GPL)
SERIKALI YAMPONGEZA MZEE GURUMO
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi. Lilly Beleko kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akimkabidhi Mzee Muhidini Gurumo barua kama ishara ya Serikali kutambua mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki nchini pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi kazi hiyo, hivi karibuni nyumbani kwake Makuburi, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ya Mkurugenzi ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Bw. Addo Mwasongwe na kulia pembeni ya Mzee Gurumo ni Mkewe, Bibi. Pili Said Kitwana.
Nguli wa Muziki wa Dansi, Mzee Muhudini Gurumo (aliyevaa shati la drafti) akiwa na watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, walipomtembelea nyumbani kwake Makuburi Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Serikali kupitia Wizara hiyo ilimkabidhi barua rasmi Mzee huyo kutambua mchango wake katika tasnia ya Muziki na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo.
Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi Lilly Beleko, wa pili ni mke wa Mzee Gurumo, Bibi. Pili Said Kitwana na wa Pili Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara Upande wa Sanaa, Bibi. Joyce Hagu.
Picha zote na Concilia Niyibitanga
Monday, September 09, 2013
"WAHAMIAJI WALIOOLEWA RUKSA KUISHI NA WENZA WAO"
Serikali imesema wahamiaji haramu walioolewa na Watanzania wanaruhusiwa kubaki nchini, hawalazimiki kuvunja ndoa zao ingawa wanatakiwa kupata kibali maalumu kutoka Idara ya Uhamiaji.
Akizungumza mjini hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, alisema wahamiaji haramu walioolewa wanatakiwa kwenda Idara ya Uhamiaji kupata hati hizo.
Pia, alisema kwa mujibu wa sheria,
mhusika atapewa kibali alichokiita 'Independence Pass' kitakachomwezesha
kuendelea kuishi nchini na kwamba, kinyume chake itakuwa ni kuvunja
haki za binadamu.
Hata hivyo, Massawe alibainisha kuwa
lazima zoezi la kuondoa wahamiaji haramu lifanyike, kwani walioondoka
kwa hiari ni 11,601 na waliokadiriwa kuondoka ni kati ya 52,000 na
53,000, hivyo idadi kubwa bado wanaishi nchini.
Akizungumzia zoezi la kurudisha
wahamiaji haramu lililoanza rasmi Septemba 6, mikoa ya Kagera, Geita na
Kigoma, Mkuu Msaidizi wa Operesheni hiyo, Simon Sirro, alisema tayari
wamewakamata 1,851.
Pia, Sirro alisema ng'ombe 1,765, sare
za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na bunduki saba vimekamatwa na
kwamba, wahamiaji wanaokamatwa wanarudishwa kwa mujibu wa sheria kwa
kuzingatia haki za binadamu.
SERENA WILLIAMS AMCHAPA VICTORIA AZARENKA 7-5, 6-7 (6-8) 6-1 KATIKA FAINALI YA US OPEN
Serena
Williams amefanikiwa kulinda Heshima na Ubingwa wake Wa US OPEN mara
baada ya Kumshinda mpinzani wake Victoria Azarenka Kwa Miaka Miwili
Mfululizo
Azarenka Akilia Baada ya Kushindwa na Serena Kwa Miaka Miwili Mfululizo katika Mashindano ya US Open
"WENGI MASIKINI KWA SABABU HAWATUMII FURSA ZILIZOPO" MENGI
Mwenyekiti Wa Makampuni ya IPP Reginald Mengi
MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Reginald
Mengi amesema Watanzania wengi wanazidi kuwa masikini kwa sababu
hawazitumii fursa za utajiri uliopo nchini, hivyo kutaka vijana kuona
kwa macho fursa hizo ili waweze kujikwamua kutoka kwenye dimbwi hilo la
umasikini.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa
washindi watatu wa shindano la nini kifanyike kuzalisha ajira nyingi
hapa nchini aliloanzisha Mwenyekiti huyo wa IPP, Mengi alisema baada ya
Watanzania kupofushwa kuwa nchi yao ni masikini, wengi walibweteka na
kushindwa kuchangamkia fursa zilizopo hali ambayo imeifikisha nchi hapa
ilipo.
Alisema jambo la msingi kwa vijana wa
Tanzania ni kuibua mawazo ya shughuli gani atafanya badala ya kukimbilia
namna ya kupata mitaji, kwani wengi ambao wamekimbilia kutafuta mitaji
wamejikuta wanaipata mitaji hiyo, lakini wakashindwa namna ya kuitumia.
Washindi katika shindano hilo ambalo
limeanzishwa na Mengi lijulikanalo kama Tweet Bora ni Lilian Wilson wa
Chuo Kikuu cha Ardhi aliyepata Sh milioni moja, Susan Senga ambaye ni
mfanyabiashara ndogo alipata Sh 500,000 na Ombeni Kaaya ambaye ni
mjasiriamali kutoka Nzega, Tabora aliyekabidhiwa Sh 300,000.
UNYAMA WA KUSIKITISHA....!!! MKE AZALIA CHOONI NA KUUA KICHANGA...!!!
KWELI
dunia inakwenda ukingoni, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu,
amefanya kitendo cha kinyama baada ya kujifungua msalani na kukiua kichanga chake.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni maeneo ya Mazizini, Ukonga Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya mwanamke huyo ambaye jina lake halikupatikana kukitumbukiza kichanga hicho chooni.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo ni mkazi wa Ukonga Moshi Bar
alidaiwa kunywa dawa kwa ajili ya kuutoa ujauzito aliokuwa nao wa miezi
minane na baada ya kuona hali imebadilika alitoka nyumbani kwake Moshi
Bar na kukimbilia Ukonga Mazizini kwa ajili ya kutaka msaada kwa mama
yake mdogo.
JK AONJA NGUVU YA CHADEMA MWANZA ISHARA YA VIDOLE VIWILI, PEOPLES POWER YATAWALA
RAIS Jakaya Kikwete jana alipata wakati mgumu, baada ya kukutana
na nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza
katika ziara yake, huku Waziri wake wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, naye
akijikuta akizomewa mbele yake.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA.
Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA.
Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika.
MELI YA TANZANIA ILIYOBEBA MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA HUKO NCHINI ITALIA....!!!
MV Gold Star ikiungua baada ya kuchomwa moto na wasafirishaji wa madawa ya kulevya.
Moshi mkubwa ukitoka katika meli hiyo baada ya wahusika kujitosa majini.
Saturday, September 07, 2013
DAZ BABA ACHANGANYIKIWA NA KUWA KICHAA....WADAU WASEMA NI BANGI NA MADAWA YA KULEVYA
Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure Namba 8′ Daz Baba amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu.
Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii wenzake.
Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia mwandishi wetu jana akiwa mkoani Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili zote za mtu ambaye ni Kichaa na amekuwa mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya matukio ya ajabu.
MSIKITI WATEKETEA KWA MOTO MJINI DODOMA....MOTO WA JIKO WADAIWA KUWA CHANZO...!!!
Msikiti
mkubwa wa barabara ya saba mjini Dodoma umewaka moto mchana huu
ikiwa ni muda mfupi baada ya swala ya mchana kumalizika....
Akiongea kwa njia ya simu na Mwandishi wetu, mmoja wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni moto wa JIKO la wakazi wa ghorofa ya juu ya jengo la msikiti huo...
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, moto huo umefanikiwa kudhibitiwa na jeshi la zima moto na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha kutokana na
moto huo.
Akiongea kwa njia ya simu na Mwandishi wetu, mmoja wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni moto wa JIKO la wakazi wa ghorofa ya juu ya jengo la msikiti huo...
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, moto huo umefanikiwa kudhibitiwa na jeshi la zima moto na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha kutokana na
moto huo.
Picha ya maktaba: |
Friday, September 06, 2013
RAIS KIKWETE NA KAGAME WAMALIZA TOFAUTI ZAO NA KUKUBALIANA KUSHIRIKIANA KAMA ZAMANI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa
Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na
kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani.
Viongozi
hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika
kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa
Kampala, Uganda.
Katika
mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea
kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati
ya nchi hizo mbili.
Subscribe to:
Posts (Atom)