Friday, August 02, 2013

TCHANGIRAI: UCHAGUZI "KICHEKESHO KIKUBWA"

051 68151 
UCHAGUZI wa Rais nchini Zimbabwe ulikuwa ‘kichekesho kikubwa,’ Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema, akituhumu udanganyifu wa kura uliofanywa na kambi ya mpinzani wake Rais Robert Mugabe.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Tsvangirai alisema uupigaji kura wa Jumatano ulikuwa ‘upuuzi na si halali’.

Kundi kubwa la waangalizi mapema lilisema kufikia hadi watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.
Chama cha Bw Mugabe ambacho kinadai kushinda, kimekanusha tuhuma hizo kikisema upigaji kura ulikuwa shwari. (HM)


Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, alisemsa kwenye tathimini yao ya awali kuwa upigaji kura ulikuwa huru na haki.
Makundi mengine ya waangalizi yalisifia hali ya amani katika uchaguzi huo.

Kuhesabu kura ulianza kulianza usiku na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) ina siku tano za kutangaza nani mshindi katika uchaguzi huo.

YANGA KUKIPIGA NA MTIBWA JUMAPILI HII



Afisa Habari wa timu ya Yanga SC, Baraka Kizuguto akiongea na wanahabari leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es Salaam.

Mweka Hazina kutoka DRFA, Ally Hassan, akifafanua jambo juu ya maandalizi ya mechi hiyo.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua matukio kwenye kikao hicho.

URUGUAY KURUHUSU BANGI....!!!


Uruguay

1
Na BBC

Thursday, August 01, 2013

HII KALI: MWALIMU MKUU WA SHULE YA CHALINZE AHAMISHIA OFISI YAKE CHOONI...!!!


MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Chalinze Mzee, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Elias Kapama, yuko katika wakati mgumu baada ya kuhamishia ofisi yake kwenye vyoo vya wanafunzi kutokana na jengo la ofisi yake kuharibika vibaya.

Hatua ya kuhamia chooni ilitokana na mkuu huyo kutawaliwa na hofu ya ubovu wa ofisi yake, hivyo kushindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha unapotokea upepo au mvua.

Novemba 2012, Kapama alihamishia ofisi yake katika jengo la vyoo vya wanafunzi ambavyo havijaanza kutumika tangu ujenzi wake ukamilike mwaka 2011. Akizungumzia hali hiyo, Kapama alisema kuwa anajisikia vibaya kutumia chumba maalumu cha kubadilishia nguo cha wavulana katika choo hicho kutokana na kukosa msaada kutoka halmashauri ya wilaya hiyo.

MWANAUME AJIUA BAADA YA KUMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA NA KISU, KISA NI WIVU WA MAPENZI...!!!


                                 Linah Keza enzi za uhai wake
Jamii ya wauganda huko Uingereza wameaamka na habari za kusikitisha baada ya mwenzao aliyejulikana kwa jina la David Kikaawa kumuua mke wake Linah Keza.

Inasemekana kuwa David alimuua mke wake mida ya alfajiri baada ya kuhisi kuwa mke wake anatembea nje ya ndoa..

David alienda kujificha baada ya kumchoma mke wake na kisu hadi kufa. Baadae nae maiti yake(David) ilikutwa kwenye club 791,inayomilikiwa na kaka yake. Alijiua baada ya kumuua mke wak.

Wawili hao walikua wanaishi  kaskazini mwa London,amebaki mtoto wao wa kike mwenye miaka mitatu 
 
           Kushoto ni David,mtoto wao na Linah
                            

LIST YA WASANII, PRODUCERS NA WATU WA MEDIA 166 WALIOALIKWA NA RAIS KIKWETE KUFUTURU IKULU LEO


JK mtu wa watu
1

HUYU NDIYE BINTI ALIEFARIKI KWA KISA KILICHOANZIA FACEBOOK, FAMILIA YAKE KUISHITAKI FACEBOOK?


7

Kampuni ya mtandao wa kijamii wa facebook imezungumza baada ya tukio la yule msichana aliejiua kutokana na kisa ambacho kilianzia facebook January 2013.
1
Kumbe Chanzo ni picha ambayo ilikua inamuonyesha mrembo huyu wa Italia Carolina akiwa amelewa, aliiweka kwenye page yake ya facebook ambapo mpenzi wake wa zamani kwa kushirikiana na marafiki walianza kumtolea maneno machafu Carolina, walimtukana hivyo yeye na mdogo wake wa kike wakaamua kuripoti facebook lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Kwenye mji wa Italia wa Novarra ndio tukio lilitokea kupitia facebook na likaingia mpaka kwenye maisha ya Carolina ambapo bila yeye kujua, tukio liliendelea kuwa kubwa na kutishia kuwa kubwa kumshinda.

MWANAJESHI AMGONGA RAIA BAADA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KATIKA MATAA YA KUONGOZEA MAGARI ENEO LA TAZARA DAR ES SALAAM



Gari lililomgonga raia likipita katika upande wa kulia zinakotokea gari za Buguruni,Ubungo,baada ya dereva kukiuka sheria za usalama barabarani.

 Raia aliyegongwa akiwa hoi baada ya kugongwa na dereva wa gari la Jeshi akipepewa na askari Jeshi.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 1, 2013

DSC 0051 066d6
DSC 0052 9dfcf

JUMA KASEJA APATA DILI KUBWA KONGO...!!!

Mlinda mlango wa Taifa Stars Juma Kaseja
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Juma Kaseja amesema kwamba amefanya mazungumzo tu na wakala wa klabu ya St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini bado hajaingia Mkataba na klabu hiyo ya Lubumbashi.

Akizungumza jana mchana, Kaseja amesema kwamba mtu aliyejitambulisha kwake kama wakala wa Lupopo alimfuata wakafanya mazungumzo na kufikia makubalino juu ya dau la usajili, mshahara na mambo mengine ya msingi.

Hata hivyo, kipa huyo namba moja Tanzania amesema kwamba baada ya mazungumzo hayo na maafikiano, wakala huyo amepeleka majibu Lupopo ambao wakiafiki ndipo masuala ya Mkataba yatafuatia.

MUSWADA WA SUALA LA KODI YA SIM CARD KURUDISHWA BUNGENI AGOSTI

Waziri wa Fedha, , Dk. William Mgimwa amenukuliwa kwenye magazeti ya NIPASHE na HabariLeo matoleo ya leo akisema kuwa Serikali sasa imekubali kuwa kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na hivyo inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioazisha kodi hiyo wenye mkutano wa Bunge mwishoni mwa mwezi wa Agosti kwa mjadala zaidi na ufumbuzi kutoka kwa Wabunge.

Wiki iliyopita Rais Jakaya Kikwete alikutana na Wizara hiyo, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wajumbe wa MOAT (Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Simu -  TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel)  Ikulu kusikia pamoja na mambo mengine, kuondolewa kwa kodi ya simu kutakavyokwaza maendeleao ya sekta ya mawasiliano na kuwataka MOAT kutoa mapendekezo ya jinsi serikali itapata kiasi cha Sh. bilioni 178 zilizopangwa kupatikana katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2013/14 kutokana na kodi ya simu.

VYAKULA VYA MAFUTA NI CHANZO CHA KUKUKOSESHA USINGIZI

baga

Tumekuwa tukipokea maoni toka kwa watu wengi juu ya matatizo ya kukosa usingizi, ingawa kuna sababu nyingi zinazoweza kukufanya ukose usingizi kama magonjwa nk, ila mlo nao ni moja ya sababu hizo.Na moja ya vyakula hivi ni vile vyenye mafuta (fat) mengi kama burger, chipsi nk. Tafiti zinaonesha kuwa, vyakula hivi sio tu hukufanya uongezeke uzito bali pia huabiri mfumo wa kulala.

Tafiti zinaendelea kuwa, vyakula hivi vizito huamsha mfumo wa usagaji vyakula (digestion system) na kuifanya ianze kufanya kazi, hii hukupelekea mwili wako kuwa hai na pia hukufanya mara nyingi kujisikia kwenda haja hivyo kukukosesha usingizi. 
Hivyo basi epuka kula mlo wenye wanga mwingi wakati wa usiku au angalau kwa masaa mawili kabla ya kwenda kulala.

Wednesday, July 31, 2013

MWANASHERIA KUISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU KRISTO...!!

dola
Maajabu mengi sana hugundulika duniani kila siku , lakini kuna kila uwezekano kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee . Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu Kristo .
Mwanasheria huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Jesus-Christ-Wallpapers-3Mwanasheria huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia yoyote ya kustahili adhabu hiyo . 

Dola Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua Bwana Yesu .

FAHAMU KWANINI UNATAKIWA KUZIFANYA NDIZI KUWA SEHEMU YA MAISHA YAKO.


banana-amazing-fruit-and-cureNdizi ni tunda ambalo limezoeleka kwa watu wengi , linapatikana karibu kila mahali . Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa tunda hili mwilini mwako . Taarif aifuatayo itabadilisha mtazamo wako kwa tunda hili na utafahamu kwanini hupaswi kulichukulia poa hata siku moja .

Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako , sukari hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya Sucrose , Fructose na Glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na Fibre muhimu ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu inayohitajika mwilini mwako .

Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika 90 ambazo ni sawa na saa moja na nusu . Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu kabla na baada ya mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya mashindano katika mchezo husika .
Nishati si faida pekee inayokuja kwenye tunda la ndizi , tunda hili lina faida nyingine ambayo ni kuusaidia mwili wako kupambana na kujikinga na maradhi  kadhaa.

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU MWAKA WA MASOMO 2013/2014 HAYA HAPA



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr Shukuru kawambwa. 
---
Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.

Kati ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A) na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.Wanafunzi 363 wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.
---

MAELEKEZO MUHIMU:

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 15/08/2013.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...