Friday, August 02, 2013

YANGA KUKIPIGA NA MTIBWA JUMAPILI HII



Afisa Habari wa timu ya Yanga SC, Baraka Kizuguto akiongea na wanahabari leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es Salaam.

Mweka Hazina kutoka DRFA, Ally Hassan, akifafanua jambo juu ya maandalizi ya mechi hiyo.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua matukio kwenye kikao hicho.



TIMU za Yanga SC na Mtibwa SC zinatarajia kumenyana vikali Jumapili hii katika mchezo wa kirafiki ambao utakuwa na lengo la kujipima nguvu na kutambulisha baadhi ya wachezaji wao wapya waliyosajiliwa kwenye vilabu vyote viwili.



Akizungumza na waandishi wa habari leo, Afisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema kwamba Yanga itashuka katika Uwanja wa Taifa Jumapili hii kwa ajili ya kujipima uwezo wao na kutoa fursa ya kuwatambua wachezaji wake wapya na wale waliokuwa katika timu ya Taifa. “Mchezo wa Jumapili hii utakuwa ni muhimu sana kwa timu yetu kwani utatuwezesha kutambua zaidi na pia utatoa fursa kwa wachezaji wetu wapya kuonekana kwa mashabiki wa timu yetu”, alisema Kizuguto (HABARI PICHA:MUSA MATEJA/GPL)

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...