Waziri wa Fedha, , Dk. William Mgimwa amenukuliwa kwenye magazeti ya NIPASHE na HabariLeo matoleo
ya leo akisema kuwa Serikali sasa imekubali kuwa kodi mpya ya laini ya
simu ni mgogoro na hivyo inakusudia kurejesha muswada wa sheria
ulioazisha kodi hiyo wenye mkutano wa Bunge mwishoni mwa mwezi wa Agosti
kwa mjadala zaidi na ufumbuzi kutoka kwa Wabunge.
Wiki
iliyopita Rais Jakaya Kikwete alikutana na Wizara hiyo, Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wajumbe wa MOAT (Chama cha
Wamiliki wa Kampuni za Simu - TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel)
Ikulu kusikia pamoja na mambo mengine, kuondolewa kwa kodi ya simu
kutakavyokwaza maendeleao ya sekta ya mawasiliano na kuwataka MOAT kutoa
mapendekezo ya jinsi serikali itapata kiasi cha Sh. bilioni 178
zilizopangwa kupatikana katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa
2013/14 kutokana na kodi ya simu.