WAFUNGWA wa Gereza la Ruanda lililopo mjini Mbeya wameiomba ofisi ya Waziri wa Mambo ya ndani ya nchini kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya kikatili ya mahabusu wawili katika Gereza hilo.
Kupitia
barua ya Septemba 22,2012 ya wafungwa hao kwenda ofisi hiyo, imesema kuwa
kama si lengo la kupunguza ufanisi wa kazi za waziri wa Wizara hiyo basi ni
mikakati iliyoundwa kwa ajili ya kuchafua wizara nzima.
‘’Mhe.
Waziri, Uongozi wa Gereza hili la Ruanda umekabidhi Mamlaka ya utendaji wa
shughuli za gereza mikononi mwa kundi dogo la wafungwa wanne, kundi hilo
ujulikana kwa jina la Maumau’’ imesema barua hiyo yenye kurasa tatu.
Barua hiyo
imesema kuwa endapo mfungwa au mahabusu atahoji uhalali wa kundi hilo na kwa
bahati mbaya kundi hilo likitambua, uhai wa mtu huyo unakuwa mikononi mwa kundi
hilo la Maumau.
Imesema
mnamo July 11 mwaka 2012, kuna mahabusu aliuawa kwa kipigo baada ya kuhoji uhalali wa kundi hilo ambapo aliuawa kwa
kupigwa na mfungwa Biroka au Edo ambaye ni miongoni mwa kundi linalounda kundi
la Mau mau.
‘’Alipigwa
mbele ya Afisa usalama na uhai wake ulitoweka akiwa ndani ya Dispensary, mnamo
tarehe 30.08.2012 mwingine alipigwa na kuzimia na kutibiwa kwa siku saba katika
Dispensary’’imesema barua hiyo.
Imeeleza
kuwa Septemba 19 mwaka huu kundi la Maumau lilipata taarifa zisizosahihi kuwa wafungwa
na Mahabusu walitaka kugomea chakula ili kupinga vitendo vya kundi hilo ndipo
uongozi ukaamuru wafungwa wote na mahabusu kulala chini na kupigwa.
Wamewataja
wanaodaiwa kuuawa kuwa ni Jafari Mwaipopo aliyepigwa Septemba 19,2012 na kufa
Septemba 21,2012, Fadhili Ruvanda aliyepigwa July 1, 2012 na kufa July 14, 2012
na Robert Kigodi alivunjwa mkono na Nyapala mkuu msaidizi.
Nakala ya
barua hiyo imepelekwa kwa Kamishina mkuu wa Magereza Dar es Salaam, Mkuu wa
mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Magereza Mbeya na Mkuu wa gereza Ruanda ambapo wameomba
ofisi ya Waziri wa mambo ya ndani kuunda tume itakayofika gerezani hapo na
kukutana na wafungwa na mahabusu ili kuthibitisha tuhuma hizo.
Baadhi ya
mamlaka za Serikali zimekiri kupata nakala ya barua hiyo ambapo zimesema kuwa
hali hiyo ipo kila Gereza nchini kutokana na mfumo ulivyo.
Hata
hivyo baadhi ya wadau wa haki za binadamu wamependekeza kuwa endapo
tume hiyo itaundwa iundwe tume ya vyombo vya dola vinavyohusika na
uchunguzi wakiwemo wajumbe kutoka usalama wa taifa, Polisi na Takukuru
na si vingenevyo.
Na Kalulunga
Na Kalulunga
No comments:
Post a Comment