Tuesday, July 30, 2013

MHE. PANDU KIFICHO ALITAHADHARISHA BARAZA LA WAWAKILISHI KUWA MAKINI KUFANYA MAAMUZI YAKE

mr-pandu-ameir-kifichoNa Ali Issa-Maelezo Zanzibar 
Spika wa baraza la wakilishi Zanzibar Pandu ameir kificho amesema Baraza la wakilishi liwe na Tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo utekelezaji wake umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali kuja kuingia katika kitahanani kwa lile amblo kulitimizia Taifa mahitaji yake muhimu.
 
Hayo ameyasema  leo huko Baraza la wakilishi  wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura CCM  Hamza Hassan Juma wakati alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nnje uzuuliwe kwani una uwasokosesha mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.
 
Amesema si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo kuzuia kuku kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wa
kutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.
 
 “sivizuri kuzuia fungu hili na kukusema kuku wasiagiziwe kutoka nje bali tuwachie Serikali wakachunguze ukweli wa hilo na baadae watuleteeripoti,”alisema Spika.
Aidha ali sema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana wananchi wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio
lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...