Wednesday, July 17, 2013
HIKI NDICHO KILICHOIMALIZA TAIFA STARS DHIDI YA UGANDA...!!!
Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars, Mrisho Ngassa (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Uganda, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za CHAN 2014. Uganda ilishinda 1-0. Picha na Michael Matemanga.
KIWANGO cha chini kilichoonyeshwa na wachezaji wa Taifa Stars juzi dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, kimewavunja moyo baadhi ya wapenzi wa soka hapa nchini na kujikuta wakipoteza matumaini ya kuiona timu hiyo ikifuzu kushiriki katika fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
amewataka kuwa wavumilivu kwani lolote linaweza kutokea katika mechi ya
marudiano itakayofanyika nchini Uganda wiki mbili zijazo.
“Suala ni kwamba tulitengeneza nafasi tukashindwa
kuzitumia, katika mechi ya marudiano tunatakiwa kutengeneza nafasi na
kuzitumia kwani mpira ni magoli,” alisema kocha Poulsen.
MMOJA AFA NA WENGINE WANNE WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA BODABODA HANDENI
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi, Handeni
Dereva
mmoja wa Bodaboda amefariki dunia papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa
kwenye ajali baada ya pikipiki mbili kugongana usukani kwa usukani huko
kwenye eneo la Mzundu wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP Constantine Massawe, amemtaja Dereva huyo
wa Bodaboda kuwa ni Ismail Mhando(30), mkazi wa Kabuku wilayani Handeni. Amesema
kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mzundu wilayani Handeni
mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo katika uchunguzi wa awali wa tukio
hili Polisi walibaini kuwa imesababishwa na mwendo kasi kwa kila mmoja
na kutokuwa makini barabarani.
CHADEMA YATUPA KOMBORA JIPYA TENA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanikiwa kunasa siri za mipango ya hujuma zilizokuwa zimeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne za Jiji la Arusha, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika, zimebainisha kuwa CHADEMA katika uchaguzi huo kilifanikiwa kushinda kata hizo baada ya kuvunja ngome ya CCM iliyok
uwa ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
Kwa mujibu wa habari hizo, mipango karibu yote iliyokuwa ikifanywa na CCM, ikiwemo halali na haramu, ilivuja na kufika mikononi mwa wapinzani wao ndani ya muda mfupi hata kabla ya utekelezaji.
Imedaiwa kwamba baadhi ya watu waliokuwa katika kambi ya CCM, waliamua kwa siri kufichua mipango hiyo na kuifikisha kwa mahasimu wao kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa kushiriki katika mambo ya kidhalimu.
Habari zinasema maofisa kadhaa wa CCM ambao wamekuwa wakiratibu na kusimamia mipango karibu yote miovu dhidi ya wapinzani, waliamua kwenda kinyume na makubaliano hayo, na kwa njia ya siri wakafanikiwa kutoa mpango mzima hadharani.
Tuesday, July 16, 2013
ALICHOKIANDIKA RAY KUHUSU MAREHEMU KANUMBA....!!!
“Ni
siku ambayo nimesheherekea siku yangu ya kuzaliwa na ndugu zangu wa
karibu na wasanii wenzangu, ni siku ambayo nimekumbuka mambo mengi sana
katika maisha yangu, mara nyingi swahiba wangu marehemu Kanumba siku
kama ya leo ningekuwa naye katika sherehe kama hii, lakin ndio mambo ya
Mungu huwezi kulaumu kilichobaki ni kumuombea Mwenyezi Mungu ampumzishe
kwa amani Amen,” alisema The Greatest.
Katika sherehe hiyo iliyopambwa na vinywaji na malaji kibao
ilijumuisha wasanii nguli katika tasnia ya filamu kama Bonge la bwana,
JB, Maya, Odama, Chikoka na wasanii wengine kibao huku kukiwa na michezo
kadha wa kadhaa ni jambo jema kwa marafiki kukumbuka katika matukio
kama hayo.
MUGABE ATOA KALI YA MWAKA, ATAKA MASHOGA NA WASAGAJI WAPEANE MIMBA LA SIVYO JELAAAA...!!!
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametoa kali ya mwaka kwa kuwachimba mkwara Mashoga na Wasagaji kwamba wasipotiana mimba ni lazima atawafunga jela. Mubabe ametoa kali hiyo Ijumaa wakati akizindua kampeni za chama chake cha kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika mwezi. Isome taarifa nzima ya rais huyo mwenye umri mkubwa aliye madarakani duniani na ambaye wazungu wanambloo kwa misimamo yake isiyoyumba. |
DIAMOND AMBANA PREZZO PATAMU BAADA YA PREZZO KUMPIGIA SIMU NA KUOMBA MSAMAHA
Diamond Platnumz amesema Rapcellency Prezzo alimpigia simu hivi karibuni kumuomba msamaha kufuatia tweet za kumdiss alizoziandika wiki iliyopita, lakini hitmaker huyo wa Kesho amesema kama Prez ana nia ya kumuomba msamaha basi afanye hivyo hadharani kwenye mtandao wa Twitter.
Diamond
alikuwa akihojiwa mchana wa leo kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha
Radio Citizen ya nchini Kenya kinachoendeshwa na mtangazaji William Tuva.
Msanii huyo anayeongoza kwa kulipwa zaidi kwenye show nchini, amesema alishangazwa na kitendo hicho cha Prezzo kumdis kutokana na majigambo aliyoyatoa kabla ya show yao kwenye Tamasha la Matumaini mwanzoni mwa mwezi huu.
Msanii huyo anayeongoza kwa kulipwa zaidi kwenye show nchini, amesema alishangazwa na kitendo hicho cha Prezzo kumdis kutokana na majigambo aliyoyatoa kabla ya show yao kwenye Tamasha la Matumaini mwanzoni mwa mwezi huu.
WALIOSAJILIWA NA WALIOTEMWA KWENYE LIGI KUU
*********
Mosses
Oloya wa Uganda anayecheza soka la kulipwa nchini Vietnam anaweza akawa
ndiye mchezaji anayetikisa zaidi kwenye usajili wa soka la Bongo kwa
timu 14 zinazojiandaa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Oloya
anamudu vyema kucheza nafasi ya winga wa kushoto pamoja na kulia kama
ilivyokuwa kwa mfungaji hatari wa Simba, Emmanuel Okwi aliyetua klabu ya
Etoile du Sahel ya Tunisia Januari mwaka huu, baada ya kupata mafanikio
makubwa akiwa na Simba.
Monday, July 15, 2013
WEMA SEPETU: "SIACHI MKOROGO HADI MADUKA YAFUNGWE"
Wema katika pozi linaloonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika.
THE
big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu ametundika
mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika na kuweka
michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu kulikoni, alisema kuwa
hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe.
Baada
ya staa huyo wa filamu za ‘kikwetukwetu’ kuulizwa na kujibu hivyo
wikiendi iliyopita, alitundika picha nyingine kwenye ukurasa wake katika
mtandao wa kijamii wa BBM zikimuonesha akiwa nyumbani kwake,
Kijitonyama jijini Dar huku madhara ya mkorogo yakionekana waziwazi
kwenye mwili wake.
Baadhi
ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na wengine
kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo ndiyo
vimemfanya apasuke kiasi hicho.
BINTI KIZIWI ATUPWA JELA MIAKA MITANO BAADA YA KUNASWA NA MADAWA YA KULEVYA
Mtandao wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa biashara hiyo haramu.
Hivi
karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’
amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na
hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda
kortini mara moja Ijumaa iliyopita.
Wakati
Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa
ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’,
Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata
la ‘unga’.
Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa
Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya
kukutwa na madawa ya kulevya.
CHADEMA YAIBUKA KIDEDEA KATIKA MATOKEO YA UDIWANI KWA KUZOA KATA NNE, JIJINI ARUSHA
HOFU YAKIMBIZA
WAPIGA KURA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na ushindi mnono katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata nne za jijini Arusha.
Katika Kata ya Elerai, mgombea wa CHADEMA
Injinia Jeremia Mpinga alimbwaga Emanueli Laizer wa CCM kwa kura 1,715, dhidi ya
1,239.
Kata hiyo ilikuwa na wapiga kura 23,797
waliojiandikisha na vituo 55 vya kupigia kura, lakini idadi kubwa ya wananchi
hawakujitokeza.
Matokeo ya kura yalitangazwa chini ya ulinzi
mkali wa askari polisi zaidi ya 40 wenye silaha, na kupokelewa kwa shangwe kubwa
na wafuasi na mashabiki wa CHADEMA.
Katika Kata ya Kaloleni, mgombea wa CHADEMA,
Kessy Emmanuel Miliare alimshinda kwa mbali mgombea wa CCM kwa kura 1,470 dhidi
ya 530, wakati mgombea wa CUF ameambulia kura 275. waliojiandikisha 12,674
waliopiga kura 2,292. Kura halali ni 2,277 na zilizoharibika 15.
Akitangaza matokeo katika Kata ya Themi,
Msimamizi wa Uchaguzi, Editha Mboye alimtangaza mgombea udiwani wa CHADEMA,
Mallance Kinabo kuwa mshindi kwa kupata kura 678, akimwacha mbali mgombea wa CCM
Victor Mkolwe aliyepata kura 326, huku yule wa CUF, Lebora Ndervai akipata kura
313.
Kata ya Kimandolu, CHADEMA pia wameibuka na
ushindi mkubwa na kuiacha vibaya CCM.
Mgombea wa CHADEMA, Elishadai Ngowi amemshinda
mgombea wa CCM, Edina Sauli kwa kura 2,265, dhidi ya 1,169 za mpinzani
wake.
TAMKO LA RAIS NA AMIRI JESHI MKUU KUHUSU TUKIO LA KUUAWA KWA WANAJESHI 7 DARFUR|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa sana na tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa
vijana saba hodari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania waliokuwa wanalinda amani
katika eneo la Darfur, Sudan.
Kwa hakika, Rais amesikitishwa sana
na kitendo hicho ambako wanajeshi wengine 14 wa Tanzania wamejeruhiwa na waasi
wa Sudan na ametuma salamu za rambirambi za moyoni mwake kwa Jeshi la Wananchi
wa Tanzania na kwa familia za wafiwa wote.
Aidha, Rais Kikwete anaungana na
Watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za wafiwa
kuomboleza vifo vya vijana hao hodari wa Tanzania. Rais pia anaungana na
Watanzania wote kuwaombea wale walioumia katika tukio hilo waweze kupona haraka
na kuendelea na majukumu yao ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Katika salamu zake za rambirambi kwa
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis
Adolf Mwamunynge na familia za
wafiwa, Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu amesema:
“Sina maneno ya kutosha ya kuelezea
mshtuko, huzuni na masikitiko yangu makubwa kufuatia vifo vya vijana wetu hao
ambao wamepoteza maisha yao katika shughuli muhimu sana ya utekelezaji wa
majukumu ya Umoja wa Mataifa ya kulinda na kuleta amani katika eneo la dunia
ambako maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na
waassi.”
Rais Kikwete ameongeza kumwambia
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na familia za wafiwa ”Napenda kwa niaba ya Watanzania
wenzangu niwahakikishieni kwamba hakuna shaka kuwa vijana wetu hao tokea
walipokwenda Darfur Februari mwaka huu, na kwa hakika tokea Tanzania
ilipoanza kuchangia walinzi katika eneo hilo mwaka 2007, wamefanya kazi nzuri
sana, kazi iliyoongozwa na weledi wa hali ya juu na kazi ambayo imeiletea nchi
yetu heshima kubwa. Tutaendelea kuwaenzi kwa kujivunia kazi yao.”
Amesisitiza Mheshimiwa Rais Kikwete:
“Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu za rambirambi za dhati ya moyo
wangu kuomboleza vijana wetu hawa. Kupitia kwao, natuma salamu za rambirambi
kwa maofisa wakuu na maofisa wadogo pamoja na wapigaji wote wa Jeshi letu kwa
kupotelewa na wenzao. “
“Aidha, kupitia kwako, nawatuma
salamu zangu kwa wanafamilia za waliopotelewa na wapenzi wao na ndugu zao
katika tukio hilo. Wajulishe kuwa naungana nao katika kuomboleza. Wajue kuwa
uchungu wao ni uchungu wangu pia na wa Watanzania wote na kuwa kwa pamoja
tunamwomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki
kigumu. Vile vile kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze peponi roho za
marehemu. Amina.’
Kwa walioumia, Rais Kikwete
amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Naungana pia na Watanzania wenzangu katika
kuwapa pole nyingi walioumia katika tukio hilo tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu
wapone haraka na kuendelea na shughuli zao za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa
Mataifa.”
Vijana hao waliopoteza maisha yao na
walioumia, walikuwa sehemu ya askari 37 na ofisa mmoja ambao walikuwa
wanasindikiza msafara wa waangalizi wa kijeshi katika Darfur kutoka eneo la
Khorabeche kwenda Nyara waliposhambuliwa na waasi kiasi cha kilomita 20 kutoka
Khorabeche saa tatu asubuhi jana, Jumamosi, Julai 13, 2013.
Subscribe to:
Posts (Atom)