Diamond Platnumz amesema Rapcellency Prezzo alimpigia simu hivi karibuni kumuomba msamaha kufuatia tweet za kumdiss alizoziandika wiki iliyopita, lakini hitmaker huyo wa Kesho amesema kama Prez ana nia ya kumuomba msamaha basi afanye hivyo hadharani kwenye mtandao wa Twitter.
Diamond
alikuwa akihojiwa mchana wa leo kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha
Radio Citizen ya nchini Kenya kinachoendeshwa na mtangazaji William Tuva.
Msanii huyo anayeongoza kwa kulipwa zaidi kwenye show nchini, amesema alishangazwa na kitendo hicho cha Prezzo kumdis kutokana na majigambo aliyoyatoa kabla ya show yao kwenye Tamasha la Matumaini mwanzoni mwa mwezi huu.
Msanii huyo anayeongoza kwa kulipwa zaidi kwenye show nchini, amesema alishangazwa na kitendo hicho cha Prezzo kumdis kutokana na majigambo aliyoyatoa kabla ya show yao kwenye Tamasha la Matumaini mwanzoni mwa mwezi huu.
Amesema
haoni sababu ya Prezzo kuyachukulia vibaya majigambo hayo kwakuwa
hayakuhusiana na maisha ya kawaida bali ni ya kawaida kwa show za
kupambanishwa na kutolea mfano jinsia wacheza mieleka wnavyotambiana
kwenye mechi zao na kwamba kwenye maisha ya nje huwa hawana ugomvi.
“Sikujisikia vizuri kabisa, vitu vingi vimezungumzwa, kwanini anitukane, mimi sijazoea mambo hayo,” amesema Diamond.
“Tuache mambo ya zamani ya kutengeneza attention kupitia ugomvi, tutengeneze ngoma kali, haina haja ya kugombana.”
Diamond
ametoa ushauri kwa wasanii wote Afrika Mashariki kuwa wanatakiwa
kuungana ili kuupeleka juu muziki wake ili kwenda sawa na wanamuziki wa
Afrika Magharibi.
“Sikupenda kama binadamu wa kawaida, sikujisikia vizuri, East Africa hatuna muda wa kugombana.”
Aliongeza
kuwa majigambo ya wasanii kuhusu kuzidiana fedha hayana maana
yoyote.”Hakuna mwanamuziki mwenye hela East Africa, tufanye kazi nzuri
kuleta sifa kwenye nchi zetu.”
Hata
hivyo amesema licha ya kuumizwa na kitendo hicho cha Prezzo, hana
tatizo naye. Katika hatua nyingine, Diamond amesema yuko mbioni kufanya
ngoma na Jose Chameleone wa Uganda.
Big up:Bongo5
No comments:
Post a Comment