Tuesday, July 16, 2013

VAN PERSIE AJIUNGA NA UNITED ZIARANI, ROONEY ABAKI NJIA PANDA BAADA YA MOYES KUSISITIZA KUMSAJILI FABREGAS

Straight into the action: Robin van Persie warms up alongside United coach Phil Neville in Sydney, hours after arriving for the second leg of the club's pre-season tour
Karudi kazini: Robin van Persie amerudi na kujiunga na Manchester United katika ziara yao Sydney
Robin van Persie in training with Manchester United in Sydney
Robin van Persie (right) trains with Phil Neville during Manchester United's pre-season tour to Australia
Doubts: Yet again, question marks over Rooney's future have risen again
Maisha ya Rooney ya baadaye katika klabu yake ya United bado haijulikani
David Moyes at United's match against Singha All-Stars 
Moyes amesema atamhitaji Rooney endapo tu Robin Van Persie atakuwa majeruhi
Late arrival: Robin van Persie turns up at Manchester United's Sydney hotel 
Robin van Persie akiwasili kujiunga na Manchester United katika hoteli Sydney
Clash: Chelsea boss Jose Mourinho admitted he likes Rooney, but Moyes says he is not for sale 
Moyes ameweka wazi kuwa msimu ujao bado jembe lake, ARV litatumika kutetea ubingwa wao, na Rooney atasubiri mpaka akipata majeraha
Clash: Chelsea boss Jose Mourinho admitted he likes Rooney, but Moyes says he is not for sale
Meneno hayo ya busara kwa upande wa pili: Wakati Moyes akisema hayo, bosi wa Chelsea, Jose Mourinho ameweka wazi nia yake ya kumhitaji Rooney, lakini Moyes alitangaza kuwa nyota huyo hauzwi
*******
Kocha wa Mabingwa wa soka nchini England, Manchester United, David Moyes ameweka wazi mpango wake wa kutafuta kiungo mshambuliaji mpya, huku akithibitisha kuwa mshambuliaji wake hatari, raia wa Uholanzi, Robin Van Persie atakuwa mshambulaiji wake namba moja msimu ujao na kuleta hofu kubwa juu ya hatima ya baadaye ya Wayne Mark Rooney, dimbani Old Trafford. 
Inafahamika kuwa Moyes anataka kumleta kiungo mshambuliaji wa FC Barcelona, Cesc Fabregas mwenye uwezo na ujuzi wa hali ya juu kumudu nafasi yake na kama dili litafanikiwa basi nafasi ya Rooney itakuwa mahali pabaya sana. 
Katika mfumo wa kocha mpya wa United, inafahamika wazi kuwa nyota raia wa Japan, Shinji Kagawa, atatumika kama namba kumi nyuma ya Robin Van Persie, hivyo hali hiyo kumshangaza Rooney wapi atacheza.
Lakini katika mahojiano aliyofanya Asia, Moyes alisema bado anatamani kumbakisha Rooney, ambaye amerejea England baada ya kupata majereha ya nyama za paja. Pia alisisitiza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, bado ana umuhimu mkubwa sana katika kikosi chake.
Hata hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Manchester United, Ed Woodward alisisitiza kuwa klabu hiyo haina mpango wa haraka kuzungumza na Rooney juu ya kuongeza mkataba wake kwani bado ana miaka miwili zaidi, lakini nyota huyo anaonekana kuwa na nia ya dhati kutaka kuihama klabu hiyo.
Wakati huo huo Jembe la United, Robin Van Persie limewashawasili kujiunga na wenzao katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini England ambapo United watakuwa wanatetea taji lao walilotwaa msimu uliopita.
Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...