*********
Mosses
Oloya wa Uganda anayecheza soka la kulipwa nchini Vietnam anaweza akawa
ndiye mchezaji anayetikisa zaidi kwenye usajili wa soka la Bongo kwa
timu 14 zinazojiandaa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Oloya
anamudu vyema kucheza nafasi ya winga wa kushoto pamoja na kulia kama
ilivyokuwa kwa mfungaji hatari wa Simba, Emmanuel Okwi aliyetua klabu ya
Etoile du Sahel ya Tunisia Januari mwaka huu, baada ya kupata mafanikio
makubwa akiwa na Simba.
Nyota
Oloya yupo sokoni, anawindwa na klabu zote kubwa, Simba na Yanga. Oloya
amekuwa akibeba vichwa tofauti kwenye magazeti mbalimbali nchini.
Ufuatao ni baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa katika klabu za Ligi Kuu nchini na wachezaji waliotemwa na klabu hizo:
Prisons Mbeya
Wapya: Wilbert Mweta (Simba), Ibrahim Mamba (Oljoro).
Walioondoka:
David Abdallah (Mbeya City), Sino Agustino (Simba), Elias Maguri (Ruvu
Shooting), Misango Magai, Emmanuel Gabriel na Henri Mwalugala
(wameachwa).
Mbeya City
Wapya: David Abdallah (Prisons), Paul Nonga (Oljoro).
Walioachwa:
kipa Amani Simba. Pia kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi
anasema,”nafikiri nitafute baada ya wiki moja nitakuwa na jibu zuri la
kukujibu zaidi.”
Coastal Union
Wapya:
Haruna Moshi, Juma Nyosso (Simba), Said Rubawa, Marcus Ndahel (Oljoro),
Crispin Odulla (Bandari, Kenya), Keneth Masumbuko (Polisi Moro) na
Abdullah Othman (Jamhuri ya Pemba).
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment