Monday, July 08, 2013

RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AWAASA WAISLAMU NCHINI

 

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amewataka Waislamu wote nchini kuishi na Watanzania wenzao katika misingi ya kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana, kama Uislamu ulivyofundisha.

Dk Shein aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa msikiti wa Masjid Taqwa, uliopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam, katika hotuba ilyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji MakameKatika hotuba hiyo ya ufunguzi wa msikiti huo, Dk Shein alisema kuwa ni wajibu kwa Waislamu kufanya kila jitihada katika kuilinda amani na utulivu alioubariki Mwenyezi Mungu hapa Tanzania. 

Alisema kuwa kuna kila sababu kwa Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanaweza kufanya ibada zao katika mkusanyiko mkubwa kama huo wa ufunguzi wa msikiti bila ya hofu, woga wala bughudha ya namna yoyote.Dk Shein alipongeza jitihada zinazochukuliwa na wasimamizi wa msikiti huo katika kuimarisha na kuitunza historia yake tangu ulipoanzishwa mnamo mwaka 1927, ambapo historia hiyo inadhihirisha kuwa msikiti huo ni miongoni mwa misikiti mikongwe katika Jiji la Dar es Salaam.

MKE WA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA, MAMA ANNA MKAPA AMETENGWA...!!!

MAMA ANNA MKAPA.

MKUTANO wa wake za marais uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wazito, akiwemo Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush na Mkewe, Laura, umeacha kitendawili kizito kuhusu mke wa Rais wa zamani, Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa. Imebainika kuwa katika mkutano huo, ambao mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma alikuwa ni mwenyeji wao, Mama Anna Mkapa hakuhudhuria, lakini pia imeonyesha wazi kwamba hakupewa fursa kulingana na hadhi yake. 

Mkutano huo wa Kimataifa ulifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, Juni 2-3 mwaka huu, uliozungumzia nafasi ya wanawake kuinuka kimaendeleo, ukizihusisha taasisi zinazoendeshwa na wake wa marais, wakiwemo wale wastaafu.



HAKEEM NA FATIMA WAAGA SHINDANO LA BBA USIKU WA LEO; MWANAMZIKI WA KIBONGO ATUMBUIZA

 Ikiwa leo ni siku ya 42 ndani ya jumba la BBA,kama inavyokuwaga siku zote kila jumapili huwa ni eviction day yaan lazma mshirik hata mmoja aage mashindano
Mwanadada Fatima kutoka Malawi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuaga mashindano ya BBA kwa usiku wa leo.Mshiriki mwenzake kutoka Malawi  Natasha hakuamini kilichotea na kuanza kulia huku Fatima akimwambia Natasha  "No drama, no drama. It's not about you, chill out "kasha akaagana na wenziwe na kutoka nje ya jumba la BBA. 
  Hakeem kutokea nchini Zimbabwe nae ameyaaga mashindano usiku wa leo huku akiwa haamini kabisa kile kilichotokea kutokana na utani aliokuwa akiwatania wenzake kwamba wanatoka leo.Na cha zaidi amemuacha mchumba wake CLEO katika wakat wa majonzi.
 .Usiku wa leo ndania ya BBA ulipambwa na msanii mahiri kutoka TANZANIA aitwaye WAKAZI aliyeimba nyimbo zake WEEKEND na TOUCH.
Live Show: Wakazi sizzles on stage

HIZI NDIYO SABABU ZA MH ZITTO KABWE KUTOSHIRIKI TAMASHA LA MATUMAINI


Kupitia account yake ya facebook Mh. Zitto Kabwe amepost hotuba hii akielezea kushindwa kwake kufika katika tamasha la siku ya matumaini.
POST YAKE AMEANZA KWA KUANDIKA HIVI.

Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji.


TAMASHA LA MATUMAINI

Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka. Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.


Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.

Sunday, July 07, 2013

BABU CHA MIAKA 92 AFUNGA NDOA NA BINTI ALIYEMZIDI MIAKA 70...!!!

 
Musali Mohammed al-Mujamaie (kulia) akiwa na mkewe, Muna Mukhlif al-Juburi.
Mkulima mmoja nchini Irak mwenye miaka 92 amemuoa mwanamke waliyetofautiana miaka 70 katika ndoa tatu kwa mpigo sambamba na wajukuu zake wa kiume wawili.

Musali Mohammed al-Mujamaie alimuoa mke mwenye umri wa miaka 22, Muna Mukhlif al-Juburi katika sherehe iliyodumu kwa masaa manne.

Wajukuu zake wa kiume, wenye umri wa miaka 16 na 17, nao walifunga ndoa kwenye sherehe hiyo iliyofanyika kaskazini mwa Baghdad Alhamisi iliyopita, kwa mujibu wa ripoti.

Mzee Mujamaie alisema kwenye siku hiyo maalum alikuwa akisubiria kwa muda mrefu kutokana na harusi za wajukuu zake kuwa zinaahirishwa mara kadhaa ili aweze kuunganisha na sherehe yake.

TBS YAPIGA MARUFUKU UUZWAJI WA MAFUTA YA KUPIKIA YA 'OKI'.....WADAI YANA MADHARA KIAFYA.

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/OKI.jpg 
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limebaini kuwa mafuta ya kula aina ya Oki na Viking yaliyoenea sokoni nchini, yamebainika kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Kwa mujibu wa TBS, vipimo vyote vitatu vilivyotumika kuyapima kuonyesha ubora, vimefeli na vimeonyesha mafuta hayo kuharibika kwa haraka tangu yalipotengenezwa na mpaka leo.
Pamoja na Oki, mafuta mengine yenye walakini ni Asma, Vikingi, Partiner na Premier Gold ambayo huuzwa kwa dumu lenye ujazo wa lita 20 kwa bei ya kuanzia Sh 38,000 hadi 45,000, wakati bei ya mafuta ya kula yanayotengenezwa nchini kwa ujazo huo huuzwa kati ya Sh. 52,000 na Sh.55,000.

Baada ya kupimwa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga, anasema ilithibitika kuwa mafuta ya Oki yanayozalishwa Malaysia na kupakiwa Singapore hayana ubora.
Alisema mafuta hayo yametengenezwa 2011 na kuonyesha mwisho wa kutumika ni Oktoba mwaka huu. Msasalaga alisema walipoyachunguza wamebaini hayana namba ya ufuatiliaji wakati suala hilo ni la muhimu kuwekwa.
Isitoshe, wawalipoyapima kutoka kipimo kimoja kwenda kingine, majibu yake yalishindwa na kuzidi kuonyesha mafuta hayo kuharibika kila walipoyapima.
Alisema kuna vipimo vya maabara ukipima vinaeleza mafuta kama yanafaa kutumika lakini kipimo hicho hakikufanikiwa.NA TALK BONGO

LUCY KOMBA NA IRENE UWOYA NDANI YA BIFU ZITO, KISA NDIKUMANA...!!!

 
MWANAFUNZI na mwalimu wake katika sanaa, Irene Uwoya na Lucy Komba wameingia katika bifu zito chanzo kikidaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumzunguka mwanafunzi wake kwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Lucy ambaye ndiye mwalimu wa Uwoya kisanaa, imedaiwa kuwa amemzunguka Uwoya kwa mumewe, Ndiku kwa kisingizio cha kucheza naye filamu iliyofahamika kwa jina la Kwa nini Nisimuoe?
 
“Kimenuka! Lucy Komba amemhadaa Ndiku, akazuga kuigiza naye filamu moja ndipo walipozama kwenye ukaribu kwelikweli.
“Mbaya zaidi filamu yenyewe wameigiza wahusika wawili tu (Lucy na Ndiku) mwanzo mwisho kule Tegeta. Sasa wewe unafikiri kuna nini hapo kama siyo mapenzi?’’ kilihoji chanzo hicho makini.
Baada ya paparazi wetu kuyanasa madai hayo, Jumatano iliyopita alimtafuta Uwoya kwa njia ya simu ambapo alipopewa taarifa hizo, alionesha kushtuka na kuchanganyikiwa mumewe kuigiza filamu moja na Lucy, alikata simu kisha baadaye akampigia paparazi yeye.
“Kuna wakati nilikuwa namtafuta Ndiku sijui alipo kumbe alikuwa na Lucy, sawa lakini kama Lucy ameamua kunifundisha mimi na sasa amemfundisha mume wangu sawa, tupo hapa!”
Paparazi wetu alihamishia majeshi kwa kumtwangia ‘mtuhumiwa’, Lucy ambaye alitiririka kama ifuatavyo:
 
“Nilijua Uwoya akisikia itakuwa ni balaa maana siku za nyuma niliwahi kumshutumu kutoka na mzazi mwenzangu (Patrick Mbasha) lakini mimi nipo tayari kwa lolote!”
Lucy Komba ndiye aliyemuingiza Uwoya kwenye sanaa baada ya kumchezesha Filamu ya Yolanda ambayo ndiyo iliyomtambulisha vyema staa huyo kisha kuliteka soko la sinema Bongo.

SERIKALI YA AFRIKA YA KUSINI YAKANA MZEE NELSON MANDELA KUWA HANA FAHAMU

Former South Africa's President Nelson Mandela is pictured during an interview with the media at is house in Qunu, South Africa,18 July 2008. Mandela, the anti-apartheid icon spend his 90th birthday at home in Qunu with his family, and the whole village is celebrating EPA/THEMBA HADEBE

SERIKALI ya Afrika Kusini imekanusha taarifa kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, hana fahamu zake tena kama inavyoelezwa katika nyaraka za mahakama zilizowasilishwa mnamo 26.06.2013. 

Kifungu kinachoelezea hali mbaya ya Mandela kilitumika katika nyaraka za mahakama zilizowasilishwa na jamaa wa familia ya Mandela, kwa mujibu wa wakili aliyenukuliwa na vyombo vya habari. Ofisi ya rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ilisema madaktari wanakana rais huyo wa zamani amepoteza kabisa fahamu na hali hiyo haitabadilika. 
Zuma alisema jana mchana baada ya kumtembelea hospitalini kuwa Madiba anapewa matibabu ya hali ya juu na timu ya madaktari bingwa waliobobea katika taaluma ya utabibu, ambao wako kando ya kitanda chake hospitalini kila wakati.
Nyaraka za mahakama zilizopatikana na shirika la habari la AFP zinaonyesha madaktari wanaomtibu Mandela walisema hana fahamu na kuishauri familia wiki moja iliyopita iruhusu mashine zinazomsaidia kuishi zizimwe ili apumzike.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 7, 2013

.



.
.

MFANYABIAS​HARA MWENYE ASILI YA KIARABU MBARONI KWA KUMBAKA TAHIRA


Na Cresensia Kapinga,Songea.
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikiria mfanyabiashara mmoja Jamali Nassoro (67) mwenye asili ya kiarabu mkazi wa eneo la Making'inda katika manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito wa mimba ya miezi 5 msichana mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kuwa na ugonjwa wa utindio wa ubongo(TAILA) ambaye jina lake tunalo limehifadhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma George Chiposi alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiarabu limetokea hivi karibuni baada ya wazazi wa msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo tofauti kimaumbile na kuchukuwa jukumu la kwenda kumpima ambako vipimo vilionesha kuwa ni mjamzito wa miezi 5.

Chiposi alisema kuwa wazazi wa msichana huyo baada ya kubaini mtoto wao ni mjamzito walimuhoji ili kujuwa ni nani aliyemfanyia unyama huo ambapo licha ya kuwa msichana huyo ni tahira alieleza kwa shida kuwa alikamatwa kwa nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye alimtaka ampelekee maji ya kuoga chumbani kwake.

Saturday, July 06, 2013

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA JOYCE KIRIA BAADA YA KUSHAULIWA AMWAMBIE MUMEWE AACHANE NA SIASA

My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.


Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama).

 
Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"

Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.

DIAMOND ASABABISHA KIFO CHA MTOTO MWANANYAMALA...!!!


Vilio  na  simanzi  vilitanda Jumatano iliyopita Mwananyamala Kisiwani, jijini Dar kufuatia mtoto wa mwaka mmoja, Rahim Rajab kufariki dunia kwa kuangukiwa na watu watatu, akiwemo baba yake mzazi, Rajab Said..

Tukio la watu hao kumwangukia mtoto huyo lilitokea Jumatatu iliyopita na lilisababishwa na ugomvi mkubwa wa CD yenye nyimbo za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ulioibuka ndani ya chumba cha kulala kati ya mama wa marehemu na mpangaji mwenzake aitwaye Aisha.

Akizungumza kwa machungu kuelezea tukio hilo, mama mzazi wa marehemu Rahim, Habiba Ally alikiri kuwa kisa cha kifo cha mwanaye ni CD tu.Akasema: 

" Kwa kweli hakuna kingine zaidi ya CD, naamini hivyo kwa kuwa mimi sikuwa na ugomvi wowote na Aisha. Tulikuwa tunaishi kawaida tu ukiacha mikwaruzo ya hapa na pale.”

MAGAZETI YA BONGOLEO TAREHE 6 JULAI, 2013

.
.
.

SOMALIA YALIKOSOA JESHI LA KENYA KISMAYO



Wanajeshi wa Kenya walisaidia Somalia kufurusha wapiganaji wa Al shabaab kutoka Mogadishu
Kufichuliwa kimakosa kwa barua ya siri ya kidiplomasia kumefichua mgawanyiko mkubwa kati ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi na nchi za kiafrika pamoja na kikosi cha kulinda amani cha Kenya kinachohudumu Somalia.
Katika barua hiyo,iliyoonekana na BBC, Somalia inakishutumu kikosi cha Kenya kwa kushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigano ya hivi karibuni kati ya makundi tofauti yaliyosababisha vifo vya watu 65.
Taarifa zinazohusiana
Kenya ina kikosi Kusini mwa Somalia karibu na mpaka wake kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani.

Somalia imekuwa katika vita kwa miongo kadhaa sasa lakini matumaini yalikuwa kwamba kikosi cha Umoja wa Afrika wakiwemo wanajeshi wa Kenya wataleta tofauti kubwa katika nchi hiyo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...