Saturday, July 06, 2013

SOMALIA YALIKOSOA JESHI LA KENYA KISMAYO



Wanajeshi wa Kenya walisaidia Somalia kufurusha wapiganaji wa Al shabaab kutoka Mogadishu
Kufichuliwa kimakosa kwa barua ya siri ya kidiplomasia kumefichua mgawanyiko mkubwa kati ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi na nchi za kiafrika pamoja na kikosi cha kulinda amani cha Kenya kinachohudumu Somalia.
Katika barua hiyo,iliyoonekana na BBC, Somalia inakishutumu kikosi cha Kenya kwa kushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigano ya hivi karibuni kati ya makundi tofauti yaliyosababisha vifo vya watu 65.
Taarifa zinazohusiana
Kenya ina kikosi Kusini mwa Somalia karibu na mpaka wake kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani.

Somalia imekuwa katika vita kwa miongo kadhaa sasa lakini matumaini yalikuwa kwamba kikosi cha Umoja wa Afrika wakiwemo wanajeshi wa Kenya wataleta tofauti kubwa katika nchi hiyo.

Lakini barua hii kutoka wizara ya mashauri ya kigeni kwa Umoja huo wa Afrika inawashutumu walinda amani wa Kenya kuegemea upande mmoja katika eneo hilo la kusini mwa Somalia.

Barua hiyo inasema kikosi cha Kenya kinapendelea kundi moja dhidi ya makundi mengine na kilimkamata afisa mmoja mkuu wa jeshi la Somalia na kilitumia silaha nzito katika maeneo yalio na raia.

Kile kilichotajwa katika barua hiyo kuwa ni kutowajibika kwa kikosi cha Kenya kunasemekana kusababisha kuzuka mapigano hivi karibuni katika mji wa Kusini ulio karibu na bandari ya Kismayo.

Watu 65 waliuawa huku wengine 155 wakijeruhiwa.

Barua hii ya kidiplomasia imefichuliwa tu lakini Kenya haijatamka chochote kuihusu. Lakini Jeshi la Kenya awali lilisitiza kwamba haliegemei upande wowote na jukumu lake Somalia ni kuleta amani.

Tuhuma hizo za serikali ya Somalia huenda zikathibitisha wasiwasi katika eneo hilo kwamba wakati kenya ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani lakini pia kina ajenda yake.

Wanadiplomasia katika eneo hilo wanasema inajaribu kuunda jimbo ndani ya Somalia linaloendeshwa na wanasiasa wa Somalia ambao inaweza kuwadhibiti.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...