MSANII wa filamu za Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’ ameonesha kukerwa na
wanaume ambao hawana hela lakini wamekuwa wakijifanya
wanajua kupenda sana huku wakiwa na wivu kupitiliza. Akiongea na mwandishi wetu , Kabula alisema anajua kupenda ni suala la msingi lakini anawashangaa wale wanaokuwa na wivu wa kupindukia na wakati mwingine kutoa vipigo kwa wapenzi wao wakati wao ni wanaume wasio na kitu. “Unajua nawashangaa sana wanaume wa aina hiyo, wanakuwa na wivu kupitiliza lakini hawawasaidii chochote wapenzi wao kifedha zaidi ya kuonesha wana wivu na wakipishana kidogo tu kipigo kinatembea, mimi wananikera sana,” alisema Kabula. |
Saturday, July 06, 2013
JINI KABULA .... "MWANAUME ASIYE NA PESA HAPASWI KUWA NA WIVU KWA MPENZI WAKE"
MOYES ASEMA: ROONEY HAUZWI, ATAENDELEA KUWA MCHEZA WA UNITED - KUHUSU RONALDO ASHINDWA KUKATAA WALA KUKUBALI KUTAKA KUMSAJILI MOYES ASEMA: ROONEY HAUZWI, ATAENDELEA KUWA MCHEZA WA UNITED - KUHUSU RONALDO ASHINDWA KUKATAA WALA KUKUBALI KUTAKA KUMSAJILI
Kocha wa
Manchester United David Moyes leo hii amethibitisha kwamba mshambuliaji
wa klabu hiyo Wayne Rooney hayupo sokoni na ataendelea kuicheza klabu
hiyo kwa mingi ijayo.
Akizungumza kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na klabu hiyo akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, Moyes alisema: "Nimeongea na Wayne Rooney. Wayne yupo nyuma ya mabao 40 kumfikia Sir Bobby na Denis Law. Wayne hauzwi - ni mchezaji wa Manchester United - na ataendelea kubakia kuwa mchezaji wa Manchester United. Nimekuwa na mikutano nae kadhaa. Amerudi kwenye hali nzuri na anafanya vizuri mazoezini. Tunajaribu kufanya kila kitu kumrudisha Wayne Rooney kuwa kama alivyokuwa zamani - Wayne Rooney ambaye tunamjua.
"Vyovyote vilivyotokea kabla, tunafanya kazi pamoja sasa. Macho yake yanaonyesha ni mtu mwenye furaha, ni lazima niseme Wayne hauzwi. Kuliwahi kuwepo mkutano wa siri baina ya Rooney na Sir Alex. Mie naendelea mbele sasa, sijui nini kilizungumzwa kwenye mkutano huo. Ninachofikiria sasa ni kusonga mbele na kufanya kazi ya kumrudisha Wayne Rooney kwenye ubora wake. "

Alipoulizwa kuhusu Cristiano Ronaldo, Moyes alijibu: "Sitomzungumzia
yeye moja kwa moja na wachezaji wengine wa vilabu vingine. Lakini hii
klabu siku zote imekuwa ikivutiwa na wachezaji bora duniani."
Pia Moyes alithibitisha kwamba winga mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace - Wilfred Zaha ambaye amekuwa akiwindwa na vilabu vingi kujiunga navyo kwa mkopo - Moyes amesema mchezaji huyo ataungana na Manchester United kwenye tour ya pre-season, kama ilivyo kwa wachezaji wengine.
Wakati huo huo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wapya, Moyes amesema angependa kusajili wachezaji mapema lakini mambo yamekuwa yakichelewa kutokana na makocha ambao ndio wanaothibitisha uuzwaji wa wachezaji wengi wamekuwa likizo au ndio wanaingia kwenye vilabu vyao vipya.

Chanzo: Shaffih Dauda Blog
Friday, July 05, 2013
MAHAKAMA YAELEKEZA MAZISHI YA MANDELA, YAAMURU MIILI YA WANAWE IFUKULIWE IKAZIKWE ATAKAPOZIKWA
HATIMAYE vita iliyokuwa ikipiganwa ndani ya familia
ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kuhusu mahali
panapostahili kuwa eneo la kuzikia miili ya wanafamilia hiyo imefikia
mwisho, baada ya Mahakama Kuu ya Mthatha iliyoko Jimbo la Eastern Cape,
kutoa hukumu inayoelekeza yawe katika makazi ya Mandela yaliyoko
kijijini Qunu.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Jaji Lusindiso Pakade wa Mahakama Kuu
ya Eastern Cape, aliyekuwa akisikiliza shauri lililofunguliwa mahakamani
hapo na mtoto mkubwa wa kike wa Mandela, Makaziwe, aliyekuwa akipinga
hatua ya Mandla ambaye alichukua uamuzi wa kufukua miili ya watoto
watatu wa Mandela akiwamo baba yake mzazi, kutoka katika makaburi ya
familia yaliyoko Qunu na kwenda kuizika katika makazi yake ya kichifu
yaliyoko Mzove.
Jaji Pakade katika hukumu yake ya juzi, alikiita kitendo cha Mandla
kufukua miili hiyo kutoka kaburini na kwenda kuizika upya bila ridhaa ya
wanafamilia, kuwa hakikubaliki hivyo miili hiyo ifukuliwe na kurudishwa
ilipozikwa awali.
UHUSUIANO WA IRAN NA ZIMBABWE WAPONGEZWA
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ali Akbar Salehi amekutana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mjini Harare ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu njia za kustawisha uhusiano wa pande mbili. Katika mkutano huo, Salehi amemkabidhi Mugabe salamu za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na rais-mteule Hassan Rohani. Kwa upande wake Rais Mugabe ameashiria safari zake nchini Iran na kusema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia aliwahi kutembelea Zimbabwe wakati akiwa rais. Mapema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alikutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Zimbabwe Simbarashe Mumbengegwi ampabo wawili hao wamepongeza uhusiano baina ya nchi zao.
Katika mkutano huo Salehi alisema Iran na Zimbabwe ziko katika mashinikizo na vikwazo haramu na hivyo nchi hizi mbili zinapaswa kuwa na ubunifu katika kukabiliana na mzingoro wa maadui. Naye Mumbengegwi alisema Iran, kama mwenyekiti wa mzunguko wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM imeinua itibari ya harakati hiyo. Aidha amepongeza misimamo imara ya Iran na Zimbabwe pamoja na kuwepo mashinikizo ya kila aina dhidi yao.
RAIS WA MPITO AAPISHWA NCHINI MISRI
Jaji mkuu wa mahakama ya juu
zaidi ya kikatiba ameapishwa nchini Misri kuwa rais wa muda baada ya
jeshi kumng'oa mamlakani rais aliyechaguliwa na raia kwa njia ya
kidemokrasia na kushinda kwa wingi wa kura, Mohammed Morsi.
Viongozi duniani wamepokea kwa tahadhari matukio
yanayojiri huko Misri. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Guido
Westerwelle, amewaambia waandishi kwamba anaangalia kwa umakini hatua
iliyochukuliwa na jeshi la Misri.Mfalme Abdalla wa Saudia ametuma ujumbe wa hongera kwa kaimu rais wa Misri akisema kwamba uteuzi wake unajiri katika wakati muhimu.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.
RCC MBEYA YAPENDEKEZA WILAYA YA CHUNYA KUWA MAKAO MAKUU YA MKOA MPYA WA SONGWE
Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo akifurahia jambo.
Na Gordon Kalulunga
WILAYA ya Chunya mkoani Mbeya ambayo kwa sasa imepitishwa na kikao maalum cha kamati ya ushauri ya mkoa(RCC) kuwa iwe makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe, ina historia ndefu na inastahili kuwa makao makuu ya mkoa. Historia inaonesha kuwa wilaya hiyo ndiyo wilaya kubwa kuliko zote nchini Tanzania.
Wilaya hiyo ina kilomita za mraba zipatazo 29,219 tarafa 4, kata 30 vijiji 73 na idadi ndogo ya watu wapatao 290,478.
Chunya ilianzishwa kwenye miaka ya 1948 na wakati huo ikiwa kama makao makuu ya wilaya ya Mbeya.
Wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya za zamani au za mwanzo na zenye historia kubwa na ya pekee nchini.
Upekee wake unaazia kuwa ni wilaya ambayo imesahaulika kimaendeleo.
Enzi za ukoloni wakati nchi ikijulikana kwa jina la Tanganyika, waingereza walichagua wilaya ya Chunya kuwa makao makuu ya jeshi la polisi katika eneo la mgodi wa Saza(mine).
George Chanda anasema kuwa, sababu kubwa ya kuchagua eneo la mgodi wa Saza au Saza Mine kuwa makao makuu ya polisi katika koloni la Tanganyika ni kilinda maslahi ya dhahabu.

Thursday, July 04, 2013
FBI WAKAGUA OFISI YA KOVA KWA MBWA...!!!
Ofisa mmoja wa Usalama wa Marekani (FBI), akiwa na
mbwa jana aliingia Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na
kufanya ukaguzi.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya msafara wa
magari ya Marekani kupita yakitokea Ikulu kwenda Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere kumlaki Rais Barack Obama.
Polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema ofisa huyo
aliingia na mbwa hadi maeneo ya mapokezi, lakini muda mfupi
walitoka.
“Walikwenda moja kwa moja mapokezi wakafanya ukaguzi,
kisha wakatoka nje ya jengo na kama hiyo haitoshi, ofisa huyo akiwa na mbwa
alikwenda sehemu ya kuegesha magari yenye kesi na yale ya kawaida na kuanza
kufanya ukaguzi, baada ya hapo waliondoka,” alisema polisi huyo na
kuongeza:
“Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale, lakini hili la
kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo tunaaminika kwa
usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo
Kikuu.”
Hata hivyo, usalama kwenye vituo vingi ikiwamo Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusu Nyerere, vilikuwa chini ya usimamizi na
uangalizi wa makachero wa Marekani.
Na Mwananchi.
Na Mwananchi.
HATIMAYE SWANSEA CITY YAKAMILISHA USAJILI WA JONJO SHELVEY
Kiungo Mpya wa timu ya Swansea City ya Uingereza Jonjo Shelvey
Hatimaye
klabu ya Swansea City imekamilisha zoezi la Kumsajili kiungo wa zamani
wa liverpool Jonjo Shelvey kwa dau la Pauni Milioni 5. Jonjo Shelvey
amesajiliwa na timu ya swansea akitokea timu ya liverpool.
Kinda
huyo mpya wa Swansea Mwenye umri wa Miaka 21 ameweka saini yake na
kukubali kufunga ndoa ya miaka minne baada ya kukubali masharti yake
binafsi na kufuzu kwa vipimo vya afya na hatimaye atakuwa kwenye dimba
la libert kwa miaka minne.
Safari
ya Jonjo katika Soka ilianza pale alipokuwa akiichezea timu ya Charlton
kabla hajaamia liverpool kwa dau la Pauni Milioni 1.7 mnamo mwaka 2010.
Baada
ya kumaliza kutia saini katika mkataba wake wa miaka minne na timu ya
Swansea Jonjo Shelvey aliandika katika Ukurasa wake wa twitter kuwa
"napenda kuwashukuru kila mmoja na mashabiki wote wa liverpool kwa
msaada wake na pia nitawamiss kweli hakika hii ni daraja la kwanza"
"Nitakumbuka
sana Jiji pamoja na klabu.Hallaa kwa kila mmoja hapa, Asante sana. Huu
ni muda sasa wakuanza ukurasa mpya katika maisha yangu ya Wales. Asante"
MGAMBO WAMUUA MKULIMA KWA KUMPIGA FIMBO YA KICHWA MBEYA...!!!
Watu wawili ambao ni askari mgambo, wamekimbilia kusikojulikana bado,
wanatafutwa na polisi baada ya kumpiga kwa fimbo kichwani na kumwua mkulima
aliyetambulika kwa jina la Gigwa Malegi (55, Msukuma) na mkazi wa kijiji cha
Iyonyo.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Barakael Masaki inasema kuwa mauaji hayo yalitokea tarehe Mosi Julai, 2013 majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Totowe wilayani Chunya, Mbeya.
Taarifa hiyo imewataja watuhumiwa kuwa ni Focus Fabian na Charles (jina la pili halijafahamika bado).
Imeelezwa kuwa chanzo cha kupigwa na kuuawa marehemu kinatokana na kukutwa akilisha mifugo (ng'ombe) kaitka eneo oevu kandoni mwa ziwa Rukwa.
Kamanda Masaki ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake amewasihi watatue matatizo yao kwa mazungumzo na kwa kufuata sheria.
Ametoa wito kwa watuhumiwa kujisalimisha mikononi mwa askari mara moja ama yeyote mwenye taarifa za watuhumiwa, azitoe mara moja katika mamlaka husika ili hatua za kisheria zichukuliwe.

RAIS WA MISRI ATIMULIWA NA JESHI LA NCHI HIYO
jeshi nchini Misri limemuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo Mohamed Morsi na imemteuwa kiongozi wa muda wa nchi baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali.
Akihutubia kwa njia ya televisheni jumatano jioni, mkuu wa jeshi, Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema katiba ya Misri imesitishwa kwa muda na mkuu wa mahakama ya katiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa muda nchini humo.
Sisi alitangaza kwamba jeshi linaangalia watu wa Misri kufuatana na maandamano makubwa ya upinzani yakidai kuwa Rais Mohamed Morsi ajiuzulu.
Kufuatia hotuba ya kwenye televisheni Bwana Morsi alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter, akiita hatua ya jeshi ni “mapinduzi kamili”. Aliwasihi wa-misri wote kukataa hatua ya jeshi lakini pia aliwataka kuwa na amani.
Kiongozi mpya wa muda nchini Misri, Adli Mansour ana umri wa miaka 68 ni mkuu wa sheria katika mahakama ya juu ya katiba. Ataapishwa alhamisi.
Kama sehemu ya mwongozo mpya unaoungwa mkono na jeshi kwa nchi, sisi aliutaka uchaguzi wa urais na wabunge, jopo kutathmini katiba na kamati ya mashauriano kitaifa. Alisema mwongozo ulikubaliwa na makundi kadhaa ya kisiasa.
Wednesday, July 03, 2013
MJUKUU WA MANDELA AFIKISHWA MAHAKAMANI....!!!
Jamaa za familia ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela,
wamewasilisha kesi ya uhalifu dhidi ya mjukuu wa Mandela,Mandla Mandela.
Msemaji
wa polisi, Mzukisi Fatyela aliambia BBC kuwa maafisa wa usalama
watachunguza tuhuma dhidi ya Mandla za kufukua makaburi kinyume na
sheria
Mwendesha mashtaka wa umma, kisha ataamua ikiwa amshtaki Mandla au la.
Inahusisha
maiti za watoto watatu wa Mandela ambao inaaminika walifukuliwa na
Mandla kutoka makaburi ya familia miaka miwili iliyopita.
Katika
kesi nyingine, jamaa kumi na sita wa familia ya Mandela, wanataka
kurejesha miili hiyo katika kijiji cha Qunu, ambako Mandela, ambaye
anaumwa sana hospitalini anataka kuzikwa akifa.
Kesi hiyo
inayosikilizwa katika mahakama kuu ya Mthatha, katika mkoa wa Mashariki
iliakhirishwa hapo jana kuanza kusikilizwa leo.
Wiki
jana, mahakama ilitoa amri ya muda kwa maiti za watatu hao kuhamishwa
kutoka nyumbani kwa Mandla katika kijiji cha Mvezo hadi Qunu, umbali wa
kilomiya 22.
Lakini Mandla Mandela, ambaye alitawazwa kama kiongozi wa kijamii na babu yake, sasa anapinga vikali amri hiyo.
SIFA ZA GARI YA OBAMA INAWEZA KWENDA 97KM TU KWA SAA AT MAXIMUM ..... YA JK IPO JUU KWA SPEED
Walioona msafara wa obama wataona namna msafara ulipita kwa speed ya kawaida sana tofauti na ile speed tuliyozoea anapopita JK, our president normally huwa ana cruise at an average of 120kmh.
Ile speed ikanifanya nitafute habari zaidi, niliyoyaona yamenishangaza, kumbeMaximum speed ya limo ya obama ni 60mph tu, sawasawa na kilimita kama 97 kwa saa. hii gari haina ujanja wa kwenda hata 100km kwa saa, hata boda boda inaweza kwenda speed kuliko hii gari
- ina uzito unaokadiria kukaribia tani 9
- matumizi ya mafuta ni 8mpg, kwa
lugha ingine inahitahi lita 35.31 ili kutembea kilomita 100, hii ni sawa
na lita 1 kwa kila kilomita 2.8
- vioo vyote havifunguki isipokua pale kwa dereva kwa mbele. gari iko 100% sealed
- Vioo vya dirishani vina thickness ya inchi 5 wakati milango ni nchi 8.
- kutokana na unene wa madirisha
na milango, obama hawezi kusikia chochote kinachoendelea nnje, spika
zimewekwa ili kunasa sauti za nje
- gari ina night vision kamera zinazomuwezesha dereva kuendesha usiku bila hata kuwasha taa
Subscribe to:
Posts (Atom)