Friday, July 05, 2013

RCC MBEYA YAPENDEKEZA WILAYA YA CHUNYA KUWA MAKAO MAKUU YA MKOA MPYA WA SONGWE


   
Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo akifurahia jambo.
Na Gordon Kalulunga
WILAYA ya Chunya mkoani Mbeya ambayo kwa sasa imepitishwa na kikao maalum cha kamati ya ushauri ya mkoa(RCC) kuwa iwe makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe, ina historia ndefu na inastahili kuwa makao makuu ya mkoa. Historia inaonesha kuwa wilaya hiyo ndiyo wilaya kubwa kuliko zote nchini Tanzania.
Wilaya hiyo ina kilomita za mraba zipatazo 29,219 tarafa 4, kata 30 vijiji 73 na idadi ndogo ya watu wapatao 290,478.
Chunya ilianzishwa kwenye miaka ya 1948 na wakati huo ikiwa kama makao makuu ya wilaya ya Mbeya.

Wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya za zamani au za mwanzo na zenye historia kubwa na ya pekee nchini.
 
Upekee wake unaazia kuwa ni wilaya ambayo imesahaulika kimaendeleo.
Enzi za ukoloni wakati nchi ikijulikana kwa jina la Tanganyika, waingereza walichagua wilaya ya Chunya kuwa makao makuu ya jeshi la polisi katika eneo la mgodi wa Saza(mine).
George Chanda anasema kuwa, sababu kubwa ya kuchagua eneo la mgodi wa Saza au Saza Mine kuwa makao makuu ya polisi katika koloni la Tanganyika ni kilinda maslahi ya dhahabu.
 


Sehemu nyingine za machimbo ya dhahabu katika wilaya hizo zilikuwa zinasimamiwa na wakoloni ni maeneo ya Chunya mjini, matundasi na Makongorosi.
Wilaya ya chunya imepata umaarufu wa kuwa eneo la kwanza hapa nchini kuleta wachimbaji madini katika maeneo ya Saza na Matundasi kutoka nchi za Northern Rhodesi kwa sasa Zambia na South Africa yaani Afrika kusini.
Enzi za ukoloni kabila wa wawemba kutoka Zambia na makaburu(Boers) kutoka Afrika kusini, ndiyo watu waliokuwa wakifanya kjazi za migodini kwasababu walikuwa ndiyo wataalamu.
Utaalam wao unaelezwa kuwa ulitokana na sababu kwamba nchi zao zilikuwa na migodi mingi ya shaba, dhahabu, Almasi na maka ya mawe.
Hadi leo hii ukienda Matundasi, Chunya mjini na Sazza utawakuta Wawemba wengi ambao zama hizo walitoka Zambia na kwa sasa wamebaikia kuwa walowezi.
Sifa za mkoa mpya wa Songwe(Chunya)
Marais wa zamani wa Afrika kusini Frederick deKlerk na Pietha Botha wote walizaliwa katika eneo la mgodi wa Saza wilayani Chunya kati ya miaka 1938 na kuendelea.
Viongozi hao mashuhuri baadaye walisoma shule katika sekondari ya Iyunga iliyopo Jijini Mbeya, ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kwa jina la Mbeya European School(shule ya wazungu) kati ya miaka ya 50.
Rais wa Zamani wa Namibia Sam Nujoma na akina Thabo Mbeki, wamewahi kuishi Matundasi katika kambi ya wapigania uhuru iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Tumbu.
Ijulikane pia kuwa wilaya hiyo ya Chunya, ndiyo wilaya ya kwanza kuwa na kiwanja cha ndege na huduma za benki Tanzania lakini mpaka sasa ni wilaya ya kwanza kwa mkoa wa Mbeya wananchi kukosa huduma za kijamii.
Kupitia makala hii, tunakipongeza kikao cha RCC cha mkoa wa Mbeya kupendekeza mkoa mpya jina la Songwe ambapo makao makuu ya mkoa huo yatakuwa eneo la Mkwajuni.
Mkoa huo utakuwa na wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba na lengo zaidi ni kusogeza huduma kwa wananchi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...