Friday, July 05, 2013

UHUSUIANO WA IRAN NA ZIMBABWE WAPONGEZWA

 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ali Akbar Salehi amekutana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mjini Harare ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu njia za kustawisha uhusiano wa pande mbili. Katika mkutano huo, Salehi amemkabidhi Mugabe salamu za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na rais-mteule Hassan Rohani. Kwa upande wake Rais Mugabe ameashiria safari zake nchini Iran na kusema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia aliwahi kutembelea Zimbabwe wakati akiwa rais. Mapema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alikutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Zimbabwe Simbarashe Mumbengegwi ampabo wawili hao wamepongeza uhusiano baina ya nchi zao.
  Katika mkutano huo Salehi alisema Iran na Zimbabwe ziko katika mashinikizo na vikwazo haramu na hivyo nchi hizi mbili zinapaswa kuwa na ubunifu katika kukabiliana na mzingoro wa maadui. Naye Mumbengegwi alisema Iran, kama mwenyekiti wa mzunguko wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM imeinua itibari ya harakati hiyo. Aidha amepongeza misimamo imara ya Iran na Zimbabwe pamoja na kuwepo mashinikizo ya kila aina dhidi yao.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...