Meya wa Mji Mkuu wa Kampala nchini Uganda akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa tuhumza za kusababisha vurugu.
Kampala, Uganda. Watu wawili wameuawa kwa risasi nchini Uganda juzi, wakiwa katika mkusanyiko kwenye eneo la soko la Kisekka.
Meya wa mji mkuu wa Uganda, Kampala, Erias Lukwago, pia alizirai baada ya kupigwa na polisi hao waliofyatua risasi za mipira kuutawanya umati wa wafuasi wake.
Akiwa kitandani, Meya huyo amesema baada ya kupata kipigo hicho alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitalini.
“Bomu ambalo lilinifanya nipoteze fahamu lilirushwa katika gari langu na kuingia ndani,” amesema.
Meya huyo ni mpinzani wa rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, alieleza kwamba maofisa wa polisi walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake wakimtuhumu kwa kuchochea ghasia.