
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwa kupitia simu ambayo namba 0752960276 na unaosomeka: “Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi.”
Alisema baada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa “nimekupata nimekuelewa nipo tayari kwa lolote.”Hata hivyo, Mulongo amekana kumtumia Lema ujumbe huo... “Nimepata hizi taarifa wewe ni kama mtu wa nane kuniuliza. Sijatuma huo ujumbe na siwezi kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”
















Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu
alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada
ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.





