Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula
anatarajia kufunga ndoa kesho katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini, mjini Njombe.
Hatua hiyo ya Mzee Mangula kuoa inakuja baada ya aliyekuwa mke wake kufariki dunia mwaka 2004, kutokana na ugonjwa wa saratani.
Msemaji wa familia ya Mzee Mangula ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) tawi la Njombe, Dk Lechion Kilimike alilieleza Mwananchi kuwa ndoa hiyo itaongozwa na Askofu Mstaafu wa Kanisa hilo, Solomon Swalo.
Mzee Mangula anafunga ndoa na Mkuu wa Sekondari ya Philip Mangula, iliyopo wilayani Wanging’ombe, mkoani Njombe, Yolanda Kaberege.