Wednesday, March 27, 2013
Dk Slaa awatuhumu Usalama wa Taifa

Dar es Salaam.
Kwa ufupi
“Chadema
ni chama makini na hakiwezi kuyumbishwa na mtu yoyote wala idara
yoyote inayotumiwa na baadhi ya watu ili kutaka kukizohofisha,” alisema
Dk Slaa ambaye mara kwa mara amekuwa akilalamika kuchezewa rafu.
Dar es Salaam. Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa
ameanza kuisakama Idara ya Usalama wa Taifa kuwa wanatumia mbinu
mbalimbali kuwahujumu na kwamba mbinu zinazofanywa na idara hiyo ni
kueneza propaganda walizodai za uongo dhidi yao.
Akizungumza jana makao makuu cha chama hicho jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema: “Tumezibaini mbinu zinazofanywa na Usalama wa Taifa kwa kutumiwa na CCM kueneza propaganda za uongo dhidi yao kwa lengo la kukichafua chama, lakini haziwezi kufanikiwa kwani tayari tumegundua mbinu zao.
ROSE NDAUKA: KAJALA AJIPANGE KUTIMIZA NDOTO ZAKE
Habari na saluti5
NYOTA
wa filamu, Rose Ndauka amemzungumzia msanii mwenzie wa filamu, Kajala
Masanja aliyeponea chupuchupu kwenda jela miaka mitano na kusema kuwa,
anachoamini ni kwamba sasa Kajala atajipanga na kuyafanya maisha yake
yaende kama alivyokusudia hatimaye kutimiza ndoto zake.Saluti5
ilizungumza na Rose ili kupata maoni yake juu ya kuachiwa huru kwa
Kajala aliyekuwa jela kwa muda mrefu, ambapo alisema kuwa kikubwa ni
kushukuru mungu kwa kuweza kwake kurudi tena uraini, lakini pia sasa ni
wakati wa kuzijenga upya ndoto zake.
“Binafsi, siwezi kujua
kwa sasa Kajala mwenyewe amepanga kitu gani juu ya maisha yake, lakini
ninaamini atafanya yale anayayowaza katika akili yake, hususan
kuhusiana na kuendeleza mipango yake ya kimaisha,” alisema Rose.
JK: afunga rasmi mafunzo ya JKT ya muda mfupi kwa wabunge RUVU JKT
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti
cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum
Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi
mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.(Picha na Freddy
Maro)

Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.
RAIS KIKWETE AKAGUA MIRADI YA UZALISHAJI JKT RUVU
Mwakilishi
wa Wabunge waliomaliza mafunzo maalumu ya muda mfupi ya Jeshi la
Kujenga Taifa(JKT)katika kambi ya RUVU Ester Bulaya akikabidhi risala
kwa niaba ya wenzake kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
leo mchana.
Wabunge
waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita
kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mris
Wabunge
waliomaliza mafunzo ya muda mfupi ya Jeshi la kujenga Taifa wakipita
kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho kikwete
wakati wa gwaride maalumu la kumaliza mafunzo hayo huko kambi ya RUVU
leo.
Wabunge
walihudhuria mafunzo ya muda mfupi Ruvu JKT wakionesha walijifunza kwa
Tuesday, March 26, 2013
SANAMU YA KANUMBA KUWEKWA BAGAMOYO, SOMA STORY HAPA
![]() |
| Of course Steven Kanumba had so much fans
kwenye hii tasnia ya filamu za
Bongo and he could defenetely take ‘Bongomovie’ somewhere far na ndio
maana anakumbukwa kutokana na ku-inspire wengi. Taarifa zisizokuwa rasmi kitaani kwasasa ni kwamba kwenye maazimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha the late steven kanumba mwaka huu huenda ikatengezwa sanamu yenye sura yake na kuwekwa kwenye mji wa kihistoria wa bagamoyo Mkoani Pwani. Muigizaji Stevene Kanumba alifariki mwezi April mwaka jana 2012 nyumbani kwake Sinza Vatkan dar es salaam akiwa na umri wa miaka 28 baada ya majibizano na mpenzi wake Elizabeth Michael ‘lulu’ ambae pia ni muigizaji. |
MCHORO WA KUMUUA ASKOFU MOKIWA

MCHORO uliosanifiwa na watu ambao inaaminika walitaka kumuua Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa ni hatari.
Askofu
Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa.
Taarifa za kila upande,
zinathibitisha kwamba mchoro huo ulisanifiwa kitaalam na kwamba
kilichomwokoa Mokiwa ni Mungu.
Imebainika kuwa kingine kilichonusuru maisha ya Mokiwa ni muundo wa nyumba yake, kwani baada ya majambazi kumshambulia kwa mapanga mlinzi wake, iliwawia vigumu kuifikia nyumba ambayo kiongozi huyo wa kiroho alikuwemo.
Imebainika kuwa kingine kilichonusuru maisha ya Mokiwa ni muundo wa nyumba yake, kwani baada ya majambazi kumshambulia kwa mapanga mlinzi wake, iliwawia vigumu kuifikia nyumba ambayo kiongozi huyo wa kiroho alikuwemo.
MCHORO WENYEWE
Uchunguzi unaonesha kwamba uvamizi nyumbani kwa Mokiwa, Mbezi kwa Yusuf, Dar es Salaam, Machi 9, mwaka huu haukuwa wa bahati mbaya kwani uliandaliwa mapema.
Pikipiki ambayo namba zake hazikunakiliwa, inatajwa kuhusika na upangaji wa uvamizi huo kwani siku ya tukio ilikaribia nyumba ya Mokiwa takriban mara tatu.
Uchunguzi unaonesha kwamba uvamizi nyumbani kwa Mokiwa, Mbezi kwa Yusuf, Dar es Salaam, Machi 9, mwaka huu haukuwa wa bahati mbaya kwani uliandaliwa mapema.
Pikipiki ambayo namba zake hazikunakiliwa, inatajwa kuhusika na upangaji wa uvamizi huo kwani siku ya tukio ilikaribia nyumba ya Mokiwa takriban mara tatu.
WANAFUNZI 10,000 WALIOKATA RUFAA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE-2012 WAMEFELI TENA
Wakati tume ya kuchunguza
matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea na kazi,
imebainika kuwa wanafunzi waliokata rufaa kutaka mitihani yao
isahihishwe upya wamefeli zaidi baada ya
kusahihishiwa.Kwa mujibu wa
taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa,
wanafunzi waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama
matokeo hayakubadilisha madaraja waliyopata awali.Habari zinaeleza kuwa,
wanafunzi waliokata rufaa NECTA kutaka mitihani yao isahihishwe upya ni
takribani 10,000 na kwamba baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine
wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo vya habari kutoka ndani
ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa mitihani kwa wanafunzi waliokata rufaa
ilianza kusahihishwa Machi 12 na kuhitimishwa Machi 15, mwaka huu na
kwamba wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi kadhaa kukata rufaa,
NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika masomo yote na kuanza
kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa umakini,
kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango cha kufeli kimeongezeka,”
alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye aliomba jina lake lisiandikwe
gazetini kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa baraza hilo.
ABOMOLEWA NYUMBA NA KUCHOMEWA VYOMBO VYA NDANI AKIDHANIWA MSHIRIKINA ILEMI MBEYA
| Wananchi wenye hasira kali wakibomoa nyumba ya mama Atupele Kalile akidhaniwa kuwa mchawi maeneo ya ilemi Mbeya |
| Wengine wameshaingia ndani na kuanza kutoa vyombo nje tayari kwa kuvichoma |
| Mtoto wa mama Atupele akijaribu kuokoa vitu vya mama yake visichomwe moto na wanakijiji |
| Vyombo vinazidi kutolewa ndani ilivichomwe moto |
| Wamefyeka shamba lake lote la mahindi |
| Wengine wanapongezana kwa kazi waliofanya |
WABUNGE ZITTO, AZAN WAMALIZA MAFUNZO YAO YA JKT KAMBI YA MGAMBO 835KJ LEO

Mbunge wa
Kigoma CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo
wakemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo
835KJ kilichopo Mkoani Tanga.
Pichani juu
ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha
chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake Iddi Azan, Abdallah
haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.

Aidha Zitto
Kabwe amesema anafuraha iliyo pitiliza kumaliza mafunzo hayo na ameweka
historia ya kubwa katika maisha yake hii leo. Anapasha zaidi katika
wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3 akiwa
amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1 akiwa amesimama. NA FATHER KIDEVU
UAMSHO WASOMEWA KESI UPYA

Na Salma
Said Zanzibar
KESI ya
jinai inayowakabili viongozi wa Dini wa Jumuiya ya Uwamsho na Mihadhara
imeanza kusomwa upya jana katika mahakama Kuu ya Zanzibar.
Kesi hiyo namba 9
ya mwaka 2012 ilisomwa mbele ya Jaji Fatma Hamid Mahmoud na Mwendesha
Mashtaka wa Serikali Bw. Ramadhan Nassib, ambae aliwataja washitakiwa
hao kuwa ni Farid Hadi (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52)
mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47)
mkaazi wa Makadara
na Azan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini mkoa wa Mjini wa Magharibi
Unguja.
Wengine ni Suleiman
Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi
wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib
Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe na Abdallah Said (48) mkaazi wa
Misufini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Washitakiwa wote
kwa pamoja walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kuharibu mali, Uchochezi,
Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la ttatu ni kula njama ya kufanya
kosa huku kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne Azan Khalid ambae
anadaiwa kufanya vitendo
vinavyoweza
kusababisha uvunjifu wa Amani.
Makosa yote hayo
yandaiawa kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 katika maeneo tofauti
ambapo washitakiwa hao walipotakiwa kujibu tuhuma zao walizikana.
Mara baada ya
kuwasomea mashtaka yao hayo Mwenesdha Mashtaka wa Serikali Bw. Nassib
alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo tayari umeshakamilika lakini hata
hivyo aliiomba mahakama hiyo kufanya subra ya kuweza kuamuwa maamuzi
yoyote kutokana na upande huo wa mashtaka kukata rufaa kitendo ambacho
alisema kwamba iwapo mahakama hiyo itaendelea na kesi hiyo kunaweza
mahakama ya rufaa ikatoa maamuzi ambayo yataweza kuathiri maamuzi ya
mahakama hiyo.
Kwa upande wa
mawakili wa watetezi uliokuwa ukiongozwa na Bw. Taufik Salum uliiomba
mahakama hiyo kuwapatia dhamana washitakiwa wake haohasa ikiangaliwa
kuwa tayari washitakiwa hao wameshakaa ndani kwa muda mrefu.
“Mhe Jaji
tumefurahi kuona kwamba kwa mara ya kwanza upande wa mashtaka unatamka
kuwa upelelezi umekamilika lakini isiwe sababu ya kuendelea kubakia
rumande wateja wetu kwa vile muda wa kukaa kwako umekuwa mwingi na
kupelekea haki yao ya msingi ya dhamana kunyimwa”,
alisema Bw. Salum.
Hata hivyo Jaji
Mahmoud alisema kuwa atayachukuwa maombi ya pande yote mbili na
kuyapitia kwa umakini ili baadae aweze kutoa maamuzi yaliyosahihi
kutokana na kuwa ni mgeni wa kesi hiyo na jalada lake amelipokea kwa
muda mchache ambao haukpata nafasi ya kuipitia.
“Nayachukuwa maombi
yote mawili nitayatafakari kwa kina na kuja kutoa maamuzi unaofaa”,
alisema.
Hata hivyo Jaji
huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 27 mwaka huu.
HABARI KUHUSU KUVUNJIKA KWA KUNDI LA P. SQUARE...!!!
![]() |
| Kumekuwa na uvumi kuhusu wasanii wanaoliunda
kundi la muziki la PSquare kutengana kiasi cha mashabiki wao kubaki
wameduwaa. Hata hivyo Peter na Paul Okoye wameweka wazi kuwa huwa wanaingia kwenye mitafaruku hadi kufikia hatua ya kupigana makonde huku kila mmoja akitishia kutengana lakini wakadai kwamba kama ni kutengana ambae angeweza kuwatenganisha ni mama yao pekee. Wawili hao wamesema kuwa mama yao aliwalea na kuwaonyesha upendo na mapenzi na kama ingetokea kuwa siku moja itatokea PSquare watatengana basi yatakuwa ni maamuzi ya wazi na kama mmoja wao ataamua kustaafu muziki basi haimaanishi kuwa wataacha kusaidiana. |
Tanzania yaahidiwa misaada bila masharti

Rais Xi Jinping wa China ameahidi
kuendelea kuipiga jeki Afrika ili kukabiliana na changamoto za
kimaendeleo, huku akisema kuwa suala la utoaji misaada yenye masharti
magumu siyo ajenda ya Serikali yake. Jinping akitumia jukwaa la Tanzania
kutambulisha sera yake kwa nchi za Afrika alisema kwamba bara hilo
limepiga hatua kubwa kimaendeleo na kwamba nchi yake itaimarisha
uhusiano uliopo kwa manufaa ya pande zote mbili.
Alisisitiza kwamba ushirikiano wenye tija ni ule
unaozingatia “majadiliano na maridhiano” na kwamba Serikali yake
imetenga kiasi cha Dola za Marekani 20 bilioni kufadhilia miradi
mbalimbali ya maendeleo Afrika.
“China haitakuwa tayari kutoa masharti kwa
taifa lolote… Tunataka kutoa fursa zinazofanana,” alisema Rais, ambaye
alishika rasmi wadhifa huo Machi 14, mwaka huu. Alisema China
haitaingilia masuala ya ndani ya nchi, huku akisisitiza kwamba shabaha
ya nchi yake ni kuendelea kupalilia ushirikiano mwema uliodumu kwa
miongo kadhaa na siyo kujihusisha na migogoro.
Baadhi
ya wachunguzi wa mambo wanadai kuwa, kauli ya kiongozi hiyo ni kama
ujumbe wa onyo kwa baadhi ya nchi za Magharibi ambazo zinalalamikiwa
kuendesha sera zinazominya ustawi wa Afrika.
Mhadhiri katika
Chuo cha Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa (CFR), Dk Ahmed Mtengwa
alisema: “Ni hotuba inayofungua njia kwa Afrika..., amezungumzia
ushirikiano unaolingana yaani `win win situation’ (kila upande
ufaidike), hivyo kwangu ninayaona matumaini.”Rais Jinping,
aliyekuwa katika ziara ya siku mbili nchini na juzi usiku alisaini
mikataba 17 inayohusu sekta za kilimo, afya na miundombinu.
Mkataba
wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ni kati ya miradi mikubwa
iliyomo kwenye makubaliano hayo na ujenzi wake utafanywa na Kampuni ya
Merchants Holding ya China na utakwenda sanjari na ujenzi wa barabara
inayounganisha bandari hiyo.
Pia katika
bandari hiyo itaunganishwa na Reli ya Kati na na ile ya Mamlaka ya Reli
ya Tanzania na Zambia (Tazara) ili kurahisisha usafiri wa mizigo ndani
na nje ya nchi. Mikataba mingine itahusiana na uboreshaji wa sekta ya
viwanda, kilimo hasa kile cha tumbaku ikiwamo kuwatafutia soko wakulima
kutoka Mikoa ya Tabora na Ruvuma ili waweze kuuza zao hilo katika soko
la China pamoja na kulipatia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zana
za kufanyia kazi.
Rais huyo, ambaye Tanzania ndiyo nchi
ya kwanza barani Afrika kuitembelea, alizindua na kukabidhi rasmi Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere kilichoko jijini
Dar es Salaam ambalo ni jengo la ghorofa tatu na lenye kumbi nne za
mikutano zenye uwezo wa kuchukua watu 1,800 kwa wakati mmoja.
Ujenzi wa kituo
hicho uligharimu Dola za Marekani 29.7 milioni zilizotolewa na Serikali
ya China kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Rais huyo
alisifu ushirikiano wa muda mrefu baina ya taifa lake na Tanzania na
kusisitiza kuwa nchi hizo zitaendelea kusaidiana kama sehemu ya kuenzi
misingi iliyowekwa na waasisi wa mataifa haya mawili, Mwalimu Julius
Nyerere na Mao Tse Tung.
Rais
Jinping aliondoka jana jioni kwenda Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa
tano wa Wakuu wa Nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi ikiwamo Brazil, Urusi,
India, China na Afrika ya Kusini (BRICS).
Chanzo -
Mwananchi
Subscribe to:
Comments (Atom)










