Tuesday, March 26, 2013

UAMSHO WASOMEWA KESI UPYA

Na Salma Said Zanzibar
KESI ya jinai inayowakabili viongozi wa Dini wa Jumuiya ya Uwamsho na Mihadhara imeanza kusomwa upya jana katika mahakama Kuu ya Zanzibar.

Kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2012 ilisomwa mbele ya Jaji Fatma Hamid Mahmoud na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Bw. Ramadhan Nassib, ambae aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Farid Hadi (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47)
mkaazi wa Makadara na Azan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini mkoa wa Mjini wa Magharibi Unguja.
Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe na Abdallah Said (48) mkaazi wa Misufini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Washitakiwa wote kwa pamoja walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kuharibu mali, Uchochezi, Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la ttatu ni kula njama ya kufanya kosa huku kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne Azan Khalid ambae anadaiwa kufanya vitendo
vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa Amani.
Makosa yote hayo yandaiawa kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 katika maeneo tofauti ambapo washitakiwa hao walipotakiwa kujibu tuhuma zao walizikana.
Mara baada ya kuwasomea mashtaka yao hayo Mwenesdha Mashtaka wa Serikali Bw. Nassib alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo tayari umeshakamilika lakini hata hivyo aliiomba mahakama hiyo kufanya subra ya kuweza kuamuwa maamuzi yoyote kutokana na upande huo wa mashtaka kukata rufaa kitendo ambacho alisema kwamba iwapo mahakama hiyo  itaendelea na kesi hiyo kunaweza mahakama ya rufaa ikatoa maamuzi ambayo yataweza kuathiri maamuzi ya mahakama hiyo.
Kwa upande wa mawakili wa watetezi uliokuwa ukiongozwa na Bw. Taufik Salum uliiomba mahakama hiyo kuwapatia dhamana washitakiwa wake haohasa ikiangaliwa kuwa tayari washitakiwa hao wameshakaa ndani kwa muda mrefu.
“Mhe Jaji tumefurahi kuona kwamba kwa mara ya kwanza upande wa mashtaka unatamka kuwa upelelezi umekamilika lakini isiwe sababu ya kuendelea kubakia rumande wateja wetu kwa vile muda wa kukaa kwako umekuwa mwingi na kupelekea haki yao ya msingi ya dhamana kunyimwa”,
alisema Bw. Salum.
Hata hivyo Jaji Mahmoud alisema kuwa atayachukuwa maombi ya pande yote mbili na kuyapitia kwa umakini ili baadae aweze kutoa maamuzi yaliyosahihi kutokana na kuwa ni mgeni wa kesi hiyo na jalada lake amelipokea kwa muda mchache ambao haukpata nafasi ya kuipitia.
“Nayachukuwa maombi yote mawili nitayatafakari kwa kina na kuja kutoa maamuzi unaofaa”, alisema.
Hata hivyo Jaji huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 27 mwaka huu.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...