Tundu ambaye ni
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amesema kuwa maelezo
yaliyotolewa kwamba alijificha chooni kwa muda wa saa mbili si kweli,
kwani hawezi kufanya hivyo.
“Jamani mimi na umri wangu huu nawezaje kuwakimbia waandishi wa
habari? Siku zote mimi nafanya kazi na waandishi wa habari,” alisema
Lissu na kuongeza:
“Ofisi yangu pale Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam ina choo ndani,
nikiwa ofisini kama mtu yupo nje wala hawezi kujua kama mimi nipo
chooni. Nadhani hizo taarifa za kusema nilijifungia chooni ni za
upotoshaji.
“Halafu haiwezekani mimi nikimbie suala la Rwakatare kwa sababu
tayari nilishalitolea maelezo. Mpaka sasa, mimi kama mmoja wa mawakili
wanaomtetea, nina maswali yangu kwa jeshi la polisi, kwani ile video
haioneshi uhalifu wowote ambao umetendeka.
“Ni kweli niliweka miadi ya kuzungumza na waandishi lakini nilisahau.
Nakumbuka jioni kabisa ya siku hiyo, nilipokea SMS ya mwandishi,
akiniambia alikaa sana Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam mpaka
akachoka, kwa hiyo alishindwa kuniona.”
Wikiendi iliyopita, iliripotiwa na mitandao mbalimbali pamoja na
gazeti moja la kila siku kwamba Lissu alijificha chooni kwa saa mbili
kukwepa kuonana na waandishi wa habari, waliotaka ufafanuzi wake kuhusu
kile kinachoendelea juu ya kesi inayomkabili Rwakatare ambaye ni
Kiongozi Mstaafu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
SOURCE GLOBAL PUBLISHER