Monday, March 18, 2013

HARUSI YA 2FACE YAZUA MANENO, GAVANA ATOA ZAWADI YA GARI

MWIMBAJI nyota wa African pop, Tuface Innocent maarufu kama 2face Idibia na mpenzi wake wa muda mrefu, Annie Macauley wamefunga ndoa ya kimila mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibua mjadala mzito baada ya kuzawadiwa gari aina ya Prado Jeep na gavana wa Jimbo la Akwa Ibom, Dk. Godswill Akpabio.
Mbali na zawadi hiyo, gavana huyo pia ameahidi kugharamia wanafamilia 20 wa Annie anayetoka katika jimbo hilo, ambao hawana uwezo wa kwenda Dubai ambako wawili hao watafunga ndoa rasmi baadae mwezi huu
Kamishina wa mawasiliano wa jimbo hilo, Aniekan Umana, alithibitisha Alhamisi wiki hii kwamba gavana Akpabio ameamua kumsaidia Annie Idibia, hivyo familia yake na marafiki wa karibu ambao ni raia wa Akwa Ibom wasioweza kumudu gharama ya safari ya Dubai watakuwa pamoja nae kwenye sherehe hizo.

Wakati watu wakihoji sababu ya gavana huyo kuingia gharama kwa ajili ya harusi hiyo, Umana alisema kwenye taarifa ya ofisi ya jimbo kuwa, wenza hao wamefanikiwa kukusanya pamoja mastaa na watu kibao maarufu, jambo ambalo ni zuri kwa uchumi wa jimbo lake.
“Harusi ya Annie na Tuface kuletwa Akwa Ibom ni jambo zuri kwa uchumi wa jimbo, na hili lisingeliweza kutokea hata kwa matangazo ya naira milioni 3,” alisema Umana akirejea jumla ya fedha zinazotarajiwa kutumika kukata tiketi kwa familia na rafiki wa Annie kutoka Dubai.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...