Monday, March 11, 2013
Tigo yampeleka nchini China Mshindi wa Promosheni ya Ascend Y200 Bw.Christian Mkama.
Mshindi
wa droo ya Ascend Y200 ya mwaka jana bw. Christian Evarist Mkama
akiongea na waandishi wa habari uwanja wa ndege wa kimataifa JK
Nyerere kabla ya safari kuelekea nchini China.
Mshindi
wa droo ya Ascend Y200 ya mwaka jana bw. Christian Evarist Mkama akiwa
na mama mzazi Bi. Eva Christian Amuko na mjomba wake bw. Fortunatus
Christian Amuko uwanja wa ndege JK Nyerere kabla ya safari kuelekea
nchini China.
Tigo
Tanzania imempeleka Bw. Christian Evarist Mkama nchini China ambaye ni
mmoja kati ya washindi wawili wa droo ya kwanza ya Ascend Y200 ambayo
ilifanyika mwaka jana tarehe 19 Desemba.
Kwa
kuwa mshindi wa droo hii amejishindia tiketi ya bure ya kwenda na
kurudi nchini China pamoja na kulipiwa gharama zote za safari,chakula na
dola 200 kwa siku za matumizi.
Akiwa
nchini china mshindi huyu atakaa siku nne na atatembezwa na kuonyeshwa
sehemu mbalimbali za mji wa Guangzhou, na kupelekwa kwenye sehemu za
utalii ya mlima Lotus.
Promosheni
ya AscendY200 ilizinduliwa mwaka jana 2012 mwezi wa kumi(oktoba) kwa
jumla kutakuwa na droo tano za Ascend Y200 na kila droo itakuwa na
washindi wawili kwa jumla ya washindi kumi watapatikana kwenye droo
hizi.
Kushiriki
kwenye shindano hili mteja wa Tigo inambidi awe amenunua simu ya Ascend
Y200 kwenye maduka ya Tigo yaliyosajiliwa na kujisajili kwenye
kifurushi cha A-Smart package.
GHASIA ZAIBUKA KENYA
Polisi wa
kutuliza ghasia, wamelazimika kutumia mabomu ya machozi nchini Kenya,
mji wa Kisumu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya
urais ambayo mgombea wao, Raila Odinga alishindwa katika uchaguzi
uliofanyika nchini humo.
Vurugu hizo ziliibuka, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais
yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.
DOKEZO
Mahakama Kuu ya Kenya ndicho chombo pekee chenye uwezo wa kutengua
matokeo ya urais yaliyotangazwa IEBC.
Jopo la
majaji watano ndilo litakalosikiliza rufaa ya mgombea wa Cord, Raila
Odinga; nao ni Jaji Mkuu, Dk. Willy Mutunga ambaye ni Rais wa Mahakama
hiyo, wengine ni Majaji Dk. Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Philip Tunoi,
Jackton Boma Ojwang na Mohamed Ibrahim.
Source: Mwananchi,
Jumatatu, Marchi 11, 2013
MAAFISA WA POLISI MBEYA WASIMAMISHWA KAZI KWA UPOTEVU WA DAWA ZA KULEVYA
Sehemu ya mbele ya gari ikiwa
imefunguliwa kwa uchunguzi
zaidi
Picha
chini :Askari polisi akilinda sehemu ya madawa ya kulevya
yaliyotolewa kwenye gari hiyo
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zimesema kuwa Waziri
wa mambo ya
ndani Dr. Emmanuel Nchimbi amewasimamisha kazi badhi ya maofisa wa
polisi kwa
upotevu wa madawa ya kulevya uliotokea mwaka jana 2012 mkoani Mbeya
katika
mazingira ya kutatanisha.
Baadhi ya maofisa hao ni kamanda wa kikosi cha
upelelezi mkoani Mbeya
(RCO) Elis Mwita, naibu RCO Jacob Kiangi na mkuu wa kikosi cha FFU
Charles
Kinyongo.
WAKATI WABUNGE WAKITESA, MADEREVA WAO WALIA NA NJAA KALI
WAKATI wananchi wengi,
wakikabiliwa na ugumu wa maisha, madereva wa wabunge nao wameibua kilio
chao
wakilalamikia ukali wa maisha. Madereva hao, walilazimika kumwandikia
barua
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila wakilalamikia haki zao kukaliwa na
wabunge. MTANZANIA imefanikiwa kunasa barua hiyo ya Julai, 2012 ambayo
imesainiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Wabunge, Juvenille
Joseph.
Pamoja
na mambo mengine,
barua hiyo inaishutumu Ofisi ya Bunge kushindwa kusimamia maslahi yao,
hali
inayowafanya waishi kwa shida.
Katika
barua hiyo,
madereva hao walilamikia suala la ukosefu wa mikataba ya kazi, huku
wakitaka
posho na mishahara yao itenganishwe kutoka katika akaunti za
wabunge.
“Mheshimiwa
Katibu wa
Bunge, sisi ni madereva wa waheshimiwa wabunge, tunaleta kwako hoja zetu
ili
ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kina katika ofisi yako.
“Kwa
kipindi chote,
madereva wa wabunge hatukuwa na mikataba ya ajira zaidi ya makubaliano
ya mdomo
baina ya dereva na mbunge.
“Ndiyo
maana kunakuwa na unyanyasaji mkubwa kwa
baadhi ya waheshimiwa wabunge dhidi ya madereva wao.
“Tunaomba
ofisi yako
izingatie kuwa kazi ya ubunge ni ya kipindi cha miaka mitano, bila
mkataba ni
vigumu kujua suala la haki za kikazi.
“Hivyo
basi, tunaomba
ofisi yako isimamie kuhakikisha kuwa wabunge wote wanatoa mikataba ya
ajira kwa
madereva wao,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
WALIOSEMA MHE. LOWASSA ALIKUWA HAPENDWI NA MWALIMU NYERERE NA AELEWANI NA FAMILIA YAKE WAUMBUKA
Ni baada ya kualikwa kuongoza harambee ya kuchangia miradi ya maendeleo Wilayani Butiama
Mke wa
Baba wa Taifa,Mama
Maria Nyerere na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh.
Edward
Lowassa wakiwasili kwenye hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za
ujenzi wa
miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri
Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa
wiki
kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Bodi ya
Mradi
huo,Dkt. Patrick Mugoya.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh.
Edward Lowassa akizungumza machache kabla ya kuanza harambee ya
kuchangisha
fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa
Mara
chini ya usimamizi wa Padri Wojciech Adam (hayupo pichani) wa kanisa Katoliki la Kiabakari lililopo
wilayani
humo,Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena
Jijini Dar
es Salaam.
Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere akizungumza machache wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za
ujenzi wa
miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri
Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa
wiki
kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.ambapo Mgeni Rasmi katika
harambee
hiyo,alikuwa ni Waziri Mkuu
Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la
Kiabakari
akitoa historia fupi ya mradi huo toka kuanza kwake mpaka walipofikia
wakati
wa hafla ya harambee ya
kuchangisha
fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa
Mara,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar
es
Salaam.ambapo Mgeni Rasmi katika harambee hiyo,alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh.
Edward Lowassa.
Mbunge
wa Jimbo la Musoma
Vijijini,Mh. Nimrod Mkono akizungumza machache wakati wa kukabidhi
mchango wake
na kuahidi kuendelea kuchangia ili kuhakikisha ujenzi wa miradi ya
maendeleo
katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara inafanikiwa huku akisikilizwa kwa
makini
na Mgeni Rasmi wa Harambee hiyo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo
la
Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria
Nyerere.
Mbunge
wa Jimbo la Musoma
Vijijini,Mh. Nimrod Mkono akikabidhi mchango wake kwa Mke wa Baba wa
Taifa,Mama
Maria Nyerere huku akisaidiwa na Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo,Waziri
Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Waziri
Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimkaribisha Brigedia
Jenerali,Zoma Kongo kukabidhi mchango wake kwa Mama Maria Nyerere kwa
ajili ya
kufanikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa
wa
Mara.
Mke wa
Baba wa Taifa,Mama
Maria Nyerere akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha
fedha za
ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa
Mara,iliyofanyika
mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mhariri
Mtendaji wa Kampuni
ya Free Media,Ansbert Ngurumo ampa mkono Mama Maria Nyerere mara baada
ya kutoa
ahadi yake ya kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya
Butiama
mkoa wa Mara.
Waziri
Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimkabidhi picha Boss
Mkuu wa
Mgahawa wa BreakPoint mara baada ya kununua kwenye mnada aliouendesha
yeye
mwenyewe.Katikati ni Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere.
Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la
Kiabakari
akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod
Mkono.
Rais wa Bodi ya Mradi huo,Dkt. Patrick
Mugoya
akizungumza machache kwenye hafla hiyo.
Meza
kuu.
Mke wa
Baba wa Taifa,Mama
Maria Nyerere (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh.
Edward Lowassa (kulia) wakiwa kwenye hafla ya kuchangisha fedha za
ujenzi wa
miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri
Wojciech Adam (katikati) wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika
mwishoni
mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Wadau
Mbali mbali
waliohudhulia hafla hiyo.
NA ISSA
MICHUZI
MATUKIO
Sunday, March 10, 2013
Waziri Acharukia Skendo ya Jack Chuzi Kujiuza
BAADA
ya hivi karibuni msanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’
kunaswa akipelekwa kuuzwa kwa mwanaume, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makalla anadaiwa kuicharukia skendo hiyo
ambapo juzikati alimvaa Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon
Mwakifwamba na kumuuliza juu ya tukio hilo la aibu.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya
shirikisho hilo kililitonya Ijumaa kuwa, Mhe. Makalla alimvaa
Mwakifwamba kwenye mkutano na wasanii uliofanyika ndani ya Hoteli ya
Kibadamu, Ubungo jijini Dar.
“Mhe. Makalla ndiye aliyekuwa
mgeni rasmi, akiwa pale alimuuliza Mwakifwamba kuhusu hatua walizochukua
kwa Jack Chuzi baada ya kuandikwa habari kuwa alinaswa akienda kuuzwa.
“Mwakifwamba alijitetea kuwa,
wanalishugulikia na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Michael
Sangu ‘Mike’ akasisitiza kuwa, wako katika mchakato wa kulitolea uamuzi
tukio hilo lililofanywa na Jack ,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi
paparazi wetu alimtafuta Mwakifwamba lakini hakuweza kupatikana mara
moja ila Mike alipoulizwa juu taarifa za Mhe. Makalla kucharukia ishu ya
Jack alisema:
“Ni kweli waziri aliuliza kuhusu
hatua tulizozichukua kuhusu suala la Jack kujiuza ambapo nilimjibu kuwa
tuko kwenye mchakato wa kulitolea uamuzi na kwa sasa tumeunda kamati
maalum, ikimaliza uchunguzi wake ndiyo tutatoa jibu kuwa tumemchukulia
hatua gani.”
Source:Global Publisher
MZEE MANDELA APELEKWA TENA HOSPITALINI AFRIKA YA KUSINI.
RAIS Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela amepelekea hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Taarifa kutoka kwa afisa ya Rais wa Afrika Kusini zimesema kuwa uchunguzi huu ni wa kawaida tu.
Kwa
muujibu wa tovuti ya Urais wa Afrika Kusini, Madaktari wanaomfanyia
uchunguzi Mzee Mandela wamesema hakuna haja ya kuwa na tahariku.
Kwa muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ni swala la kutia wasiwasi.
Mandela
mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kwa siku 18 mwezi wa
Desemba mwaka jana kutokana na kutatizwa na mapafu pamoja vijiwe ndani
ya kibofu chake cha mikojo.
Taarifa
iliyoandikwa kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma zimeeleza kuwa
Mzee Mandela alipelekwa katika Hospitali ya Mjini Pretoria kwa uchunguzi
wa kawaida wa ki-afya.
Taarifa hiyo imeendelea kusima kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutikana na matatizo yanayoambatana na Umri wake mpevu.
Mzee
Mandela alifudumu kama rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 to 1999
na ndiye rais wa kwanza mweusi kuwahi kuitawala nchi hiyo.
Kutokana
na juhudi zake za kupigania demokraisa na kupambana na sera za ubaguzi
wa rangi nchini humo, Mzee Mandela anatambulika kama Baba wa Taifa
nchini Afrika Kusini.
Tangu mwaka 2004 Mzee Nelson Mandela amekuwa hajitokeza hadharani au kushiriki katika shughuli za umma.
Kamati ya Utendaji CHADEMA Wilaya ya Tarime yavunjwa
Baada ya kikao cha ndani
kati ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani, kubaini
udhaifu wa kiuongozi ulioruhusu kuzuka kwa makundi yaliyokuwa yakidhoofisha
utendaji kazi na uhai wa chama wilayani hapa, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,
Freeman Mbowe amevunja uongozi wa wilaya hiyo (kwa maana ya Kamati ya
Utendaji).
Uamuzi huo uliofanyika
leo mchana, ulipokelewa kwa mikono miwili na wajumbe wa kikao
hicho.
Baada ya kikao hicho cha
Kamati ya Utendaji na madiwani wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, Mwenyekiti Mbowe
alikutana na wanachama na wadau wa chama wa Tarime, kwenye kikao cha ndani,
ambapo kwa kauli moja waliupokea kwa furaha uamuzi huo wa kuvunjwa kwa uongozi
huo, huku wakiomba nafasi hizo za uongozi zijazwe mapema kwa ajili ya kuendelea
kukiimarisha chama.
Uongozi wa chama katika
ngazi za kata hadi misingi utaendelea kufanya kazi kama
kawaida.
Kwa hatua hiyo, uchaguzi
wa kupata uongozi wa Kamati ya Utendaji ya muda, utafanyika ndani ya mwezi mmoja
ukisimamiwa na ngazi ya juu
Mwenyekiti Mbowe
amewataka watu wa Tarime kutopoteza ari yao ya dhati katika kukisimamia na
kukipigania CHADEMA katika kuendesha mapambano ya ukombozi wa pili wa nchi,
ambayo ilikuwa ni mfano wa kuigwa wa wanaChadema nchi nzima, kiasi cha watu
kusalimiana..."mambo...kama
Tarime..."
MAMA PINDA AHIMIZA AKINAMAMA KUWA WAZI NA WAAMINIFU
MKE wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda
amewataka akinamama wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali kuwa waaminifu
kwa wenza wao na wanafamilia wao ili waweze kupata ushirikiano kutoka kwao.
Alisema mbali ya majukumu mengi
yanayowakabili, akinamama wanapaswa kuwa karibu na familia zao kwani ndiyo
msingi mkuu wa Taifa. “Hatuna budi kutoa malezi mema kwa wenza wetu na watoto
wetu. Tunapofanikiwa katika shughuli zetu, tusiache kuwa waaminifu kwa wana-familia wetu (akinababa na watoto
wetu); tuwaheshimu na kuwaenzi kwa kuwashirikisha kazi tunazofanya ili tuweze
kupata ushirikiano wao na baraka zao,” alisema.
Mama Pinda ametoa kauli hiyo jana usiku
(Jumamosi, Machi 10, 2013) wakati akizungumza na wanawake wajasiriamali
walioshiriki Maonyesho Maalum ya Batik (Batik Gala Night) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani kwenye ukumbi wa Hellenic Club, Upanga jijini Dar es Salaam.
Maonyesho hayo yaliandaliwa na Kamati
ya Tamasha la Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (MOWE) kwa kushirikiana na Ofisi ya Shirika la Kazi
Duniani hapa nchini (ILO) yalikuwa na nia ya kuamsha chachu ya kuendeleza kazi za akinamama
wanaofanya maonyesho kila mwaka yaliyopangwa kufanyika Oktoba, mwaka huu kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Alisema akinamama wanapaswa kuungana
kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze kuunganisha ujuzi, stadi walizonazo
na kushirikishana uzoefu. Alisema hawana budi kuhakikisha kuwa bidhaa
wanazozalisha zinakuwa na ubora wa kiwango cha juu ili waweze kukabiliana na
ushindani kwenye soko.
“Napenda
kusisitiza, suala la ubora wa bidhaa tunazozizalisha kwa kuzingatia viwango vya
Kitaifa na kimataifa ili bidhaa zetu ziweze kupata uhakika wa soko. Hili
litafanikiwa pia endapo tutazingatia pia ubora wa vifungashio tunavyotumia
kwenye bidhaa zetu. Endapo, tutazingatia viwango, vifungashio na kutumia
kiandishi-anuani (barcodes), sioni ni kwa nini bidhaa zetu zisiende hadi masoko
ya mbali huko ughaibuni,” alisema.
Aliwataka
akinamama wajipange vizuri kwa ajili ya Maonyesho makubwa ya kitaifa (MOWE) yatakayofanyika
Oktoba mwaka huu ambayo yatajumuisha washiriki kutoka mikoa yote hapa nchini.
Mapema,
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi hapa nchini (ILO Tanzania), Bw. Alexio Musindo, alisema anawapongeza
akinamama wajasiriamali chini ya kamati ya MOWE kwani kupitia mafunzo
yanayodhaminiwa na Ofisi yake, akianamama hao wameweza kujiamini zaidi na
kuthubutu kushiriki maonyesho mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Alisema jamii haina budi kuwekeza zaidi
kwa wasichana kwa kuwapa fursa za kujiendesha kibiashara pamoja na ujuzi
(skills) ili waweze kujiajiri kwani wanakumbana na vikwazo vingi wanapotafuta
ajira ikiwemo, unyanyasaji na unyanyapaa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
Taarifa kutoka South Africa, kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania
1. Kibanda
leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura
baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu
mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.
2. Upasuaji
huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na
jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda
pia aliumizwa taya lake la kushoto.
3. Kuhusu
jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema
wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya
kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo
iliharibiwa kwa majeraha.
4. Wakati
akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa
kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na
kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni
matokeo ya unyama aliyofayiwa.
5. Jana
Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao
wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia
hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa
tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa
mahakamani.
Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.
--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556
Rais Kikwete amtumia salamu za pongezi Rais Mteule wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia salamu za pongezi nyingi Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya,
Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.
Katika
salamu hizo zilizotumwa leo, Jumamosi, Machi 9, 2013, saa chache baada
ya kuthibitishwa rasmi kuwa Mheshimiwa Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu
wa Kenya uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Jumatatu, Machi 4, 2013, Rais
Kikwete amemwambia Mheshimiwa Uhuru Kenyatta:
“Mpendwa
Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kupokea taarifa ya
ushindi wako wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu, kwa
niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba
yangu binafsi kukupogenza kwa dhati ya moyo wangu kwa mafanikio haya
makubwa ya kuchaguliwa kwako.”
Ameongeza Rais Kikwete: “
Ushindi huu ni ushahidi na ishara ya wazi kabisa ya imani na matumaini
ambayo wananchi wa Kenya waliyonayo katika uongozi wako. Huu ni utambuzi
wa kazi yako maridadi na mchango wako mkubwa ambao umeutoa katika
nafasi mbali mbali za uongozi katika siku za nyuma katika jitihada zako
za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ustawi wa nchi yako na
wananchi wake.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati
unajiandaa kuchukua madaraka ya juu zaidi katika nchi yako, napenda
kukuhakikishia msimamo wangu binafsi pamoja na ule wa Serikali yangu wa
kuunga mkono Serikali yako. Ni imani yangu kubwa kwamba pamoja tutaweza
kuendelea kusukuma mbele zaidi maendeleo ya nchi zetu – Kenya na
Tanzania na pia utengamano wa Afrika Mashariki kwa manufaa ya nchi zetu
na wananchi wake.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
9 Machi, 2013
KIMENUKA TENA MISRI HAKUKALIKI A BAADA YA HUKUMU YA KIFO KWA MASHABIKI 21 WA SOKA KUTOLEWA.
Mashabiki
wa soka wa klabu ya Al-Ahly katika jiji la Cairo nchini Misri wamezua
balaa katika jiji hilo ikiwa ni pamoja na kuichoma moto ofisi ya
shirikisho la soka nchini humo kufuatia mahakama jijini Cairo kutoa
hukumu ya kifo kwa mashabi 21 wa soka.
Mapema
asubuhi ya leo mahakama ya Cairo imethibitisha hukumu ya vifo hivyo
kufuatia kuuwawa kwa mashabiki 74 na wengine zaidi ya 1,000 kujeruhiwa
baada ya mchezo uliopigwa mwezi januari baina ya Al Masri ya Port Side
na Al-Ahly.
Hukumu ya kifo iliyotolewa mwezi Januari imethibitishwa hii leo na mahakama mjiniCairo na kupokelewa kwa hasira nchini humo.
Wale waliohukumiwa kifo wengi wao ni mashabiki wa Al Masry ya Port Said ambao buila shaka sasa watakuwa wanaelekea kunyongwa.
Vurugu kubwa zimeibuka katika mji wa Suez Canal city.
Itakumbukwa watu 40 walifariki dunia mara baada ya hukumu hiyo kutangazwa kwa mara ya kwanza January 26, na wengi wao waliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Itakumbukwa watu 40 walifariki dunia mara baada ya hukumu hiyo kutangazwa kwa mara ya kwanza January 26, na wengi wao waliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Mashabiki
wengi wa Al Masry katika mji wa Port Said, wanadhani kuwa mamlaka
imeipendelea klabu ya Al-Ahly, kwa kuwa ni klabu kubwa nchini Misri.
Filimbi ya
mwisho ilipo pulizwa katika mchezo baina ya Al-Masry na Al-Ahly February
1 mwaka jana ulipelekea kuzuka kwa vurugu kubwa na watu 130,000
kujeruhiwa vibaya na vitu vyenye ncha kali kama visu, vyuma, kuwasha
moto pamoja kuwavamia wachezaji wa Al-Ahly na mashabiki wao karibu.
Hasira kutoka kwa mashabiki wa Al-Ahly wakionyesha hasira zao.
Moshi mkubwa ukitoka kutoka katika ofisi za shirikisho la soka la nchini Misri
Fans protesting
wapingaji wa hukumu iliyotolewa katika mji wa Port Said katika picha hii leo.
Watu wamekusanyika kusikiliza hukumu.
Saturday, March 09, 2013
KICHEKESHO TOKA KENYA ...MAJUKUMU YA RAIS MPYA
WAKENYA TUNATAKA PRESIDENT IKO NATIMIZA MABO HAYA:-
1. Introduce petrol ya satchet kwa watu wa vitz
na probox..(no offense)
2. Wapunguze bei ya mutura na mahindi choma
juu wanatumia gas kuchoma.
3. Siku za mwizi ziongezwe from 40 to 70 juu
kumekauka.
4. Bei ya iphone ireduce juu mtu alishaa bite
hiyo apple.
5. Tissue paper itolewe hiyo second sheet.
(inakuwanga ya nini by the way?)
6. Ile light huwanga "at the end of the tunnel"
izimwe to save energy.
7. Ma subscribers wa Safcom wote warudishiwe
hiyo "bob" ikokwa jina la Collymore. Huyo
jamaa anakula bob kwa kila subscriber, siyo poa,
inafaa abaki tu Collymore.
8. Miguna Miguna anyanganywe jina moja
wapatie wenye hawana majina kama Nameless.
9.Gava ifungue Mr. Broke coz hatuwezani na Mr.
Price
10. Bei ya doughnut ibaki vilevile but wapunguze au wazibe ile
shimo
11. Bei ya soda ipunguzwe coz haikuwangi imejaa
ama wajaze
12. The road to success ikuwe super highway ndio
wasee wafike haraka
13. Atoe remix ya national anthem iwe na beats za Heart & Soul riddim.
14. Wapunguze fare ya kwenda S.africa kwa ndege juu ni mteremko ndege haitumii mafuta
Subscribe to:
Posts (Atom)