Kwa ufupi
SERIKALI ya
Malawi imesema ina wasiwasi kuhusu hatma ya mgogoro wa mpaka wa Ziwa
Nyasa na kwamba hali hiyo inatokana na Tanzania kuvunja sehemu ya
makubaliano ya usuluhishi.
SERIKALI ya
Malawi imesema ina wasiwasi kuhusu hatma ya mgogoro wa mpaka wa Ziwa
Nyasa na kwamba hali hiyo inatokana na Tanzania kuvunja sehemu ya
makubaliano ya usuluhishi.
Kauli hiyo
inakuja wakati jopo lo viongozi wastaafu kutoka nchi wanachama wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(Sadc), likijiandaa kuwasilisha
ripoti yake baadaye mwezi huu.
Jopo hilo
linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano, litakabidhi
ripoti hiyo kwa viongozi wakuu wa nchi zote mbili.
Waziri wa
Mambo ya Nchi za Nje wa Malawi, Ephraim Chiume, ameituhumu Tanzania
kwamba imeanza kuzungumzia utatuzi wa mgogoro huo wakati ikijua kuwa
mzozo huo uko katika hatua ya upatanishi maalumu.
Waziri
Chiume aliikosoa kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwa ufumbuzi
wa mgogoro wa mpaka baina ya mataifa hayo mawili, unakaribia kupatikana.
Alisema
kitendo cha Membe kuzungumzia maendeleo ya mgogoro huo kinapingana na
makubaliano ya pamoja yaliyowasilishwa kwa Chissano na kwamba hatua
hiyo inavunja moyo.
Waziri
Chiume aliliambia gazeti la Nyasa Times kuwa pande zote mbili
zilipokutana Nombemba 17 mwaka jana jijini Dar es Salaam, zilikubaliana
kuzungumzia mgogoro huo ili kuepuka kuingilia juhudi za
upatanishi. Alisema hata hivyo, hivi karibuni ya Serikali ya Tanzania
imekiuka sehemu ya makubaliano hayo.
“Tanzania wamevunja makubaliano, na sisi tunasisitiza kuwa Ziwa Nyasa ni la Malawi,” alisema waziri.
Baadhi ya
wachambuzi wa mambo, wamesema kauli huyo inaashiria kuwa huenda pande
hizo mbili zikashindwa kukubaliana na mapandekezo yatakayowasilishwa na
mpatanishi wa mzozo huo.
Mpatanishi huyo mwezi huu anatazamiwa kukutana na Rais Jakaya Kikwete na yule wa Malawi, Joyce Banda.
Hata hivyo,
alivyotafutwa ili kuzungumzia malalamiko hayo, waziri Membe
kupatikana, lakini Naibu wake Mahadhi Maalimu, alisema: “Ninachosema
mimi kwanza hizo taarifa sijazipata na kama zipo basi Serikali
itawasiliana kupitia mikondo sahihi. Serikali haiwezi kujibizana kupitia
magazeti”
Hivi
karibuni Serikali ya Tanzania na Malawi zilipeleka barua ya pamoja
kwenye Jukwaa la Marais wa Wastaafu wa Nchi za Kusini mwa Afrika
linaloongozwa Chissano, zikiomba zipatanishwe katika mzozo huo.
Hatua hiyo ilikuja baada ya majadiliano ya pande zote mbili kushindwa kuzaa matunda.
Kama sehemu
ya kuepusha mgongano wa kimaslahi, jopo hilo la wasuluhishi
halikuwahusisha viongozi wastaafu wa Tanzania Alhaji Ali Hassani Mwinyi
na Benjamin Mkapa.
Hali kadhalika Bakiri Muluzi wa Malawi.
Hata hivyo,
duru za kidiplomasia mjini Lilongwe zinasema Serikali ya Malawi
imejiandaa kwenda katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa(ICJ) kama
upatanishi huo utashindwa kuzaa matunda.
Gazeti la
Daily Times limewanukuu maofisa wa Serikali wakisema kuwa karata ya
mwisho kwa Malawi itakuwa ni kwenda katika mahakama hiyo.
Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/#ixzz2Mc2j8Jzo