Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimemtupia lawama nzito Makamo wa Kwanza wa Rais
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuanza kwenda kinyume na
makubaliano yaliounda Serikali ya Umoaja wa Kitaifa mwaka 2009.
Akihutubia mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM waliohuidhuria mkutano wa hadhara uloiofanyika Jumba la Vigae huko Jang’ombe mjini Ungujajana(3.3.13),
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema
Maalim Seif ameanza kufanya vikao vya siri vinavyotishia kuvuruga amani
na umoja wa kitaifa Visiwani humu.
Vuia ambaye ni kati ya wajumbe waasisi
walioshiriki katika mchakato wa mazungumzo ya upatanishi wa kisiasa
Zanazibar, amesema kama angeliijua mapema dhamira ya Maalim Seif katika
mazungumzo ya kundwa kwa Serikali iliyopo, angekuwa radhi kujitoa na
kutokuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya muafaka.
Amesema kwamba hivi karibuni kiongozi
huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, ameitisha kikao maalum cha vijana wa
chama chake na kusema, ikiwa chama chake kitawaamrisha vijana, nchi
haitatawalika na ikibidi litote tugawane mbao.
No comments:
Post a Comment