Chama cha
Mapinduzi (CCM) leo kimefanya mkutano wake wa hadhara katika Kata ya
Goba nje
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mkutano huo ambao ulijaza umati wa watu
wakiwamo wanachama wa chama hicho ulihutubiwa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi Taifa,
Nape Nnauye.
Sunday, February 17, 2013
RAIS KIKWETE AZIFARIJI FAMILIA ZA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA GARI UBENA ZOMOZI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji ndugu, jamaa na
marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kwa ajali ya gari
maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari
11, 2013 iliyoua watu wanane papohapo, wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II
lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.

Sehemu ya mabaki ya gari hilo lililopata ajali na kuua
watu wanane.
Sehemu ya mabaki ya magari hayo yaliyopata ajali na
kuua watu wanane.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji ndugu, jamaa na
marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kwa ajali ya gari
maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari
11, 2013 iliyoua watu wanane papohapo, wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II
lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
MANCHESTER CITY WAIBUKIA KOMBE LA FA
Manchester City 4 Leeds 0
At the
double: Sergio Aguero scored twice as Manchester City cruised into the
sixth round
Three and
easy: Carlos Tevez (left) celebrates with Sergio Aguero and David Silva
after scoring Manchester City's third goal against Leeds United (below)
It was just
the fillip manager Roberto Mancini needed, with City 12 points behind
Manchester United in the title race and amid fresh speculation over his
position.
Celebration:
Sergio Aguero (left) and David Silva mark the second goal
Under-fire
Warnock also made a goalkeeping change, replacing Paddy Kenny with Jamie
Ashdown, and brought back former Liverpool man El-Hadji Diouf, Rodolph
Austin and Aidan White, but to no effect.
Early lead:
Yaya Toure celebrates with his teammates Sergio Aguero, James Milner
and Carlos Tevez after giving City a 1-0 lead on five minutes
Composure:
Yaya Toure rounds Leeds goalkeeper Jamie Ashdown to slot home Manchester
City's first goal after five minutes
Aerial
battle: Matija Nastasic (left) challenges Aidan White in the air
He's behind
you! El-Hadji Diouf tries to rob Kolo Toure of the ball during the
first-half
On the
turn: James Milner tries to find a route past Leeds player Stephen
Warnock
Nice to
meet you! The FA Cup mascot makes the acquaintance of Man City manager
Roberto Mancini
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MWAMINI MALEMI ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA NYUZI ZA MKONGE CHA JESHI LA MAGEREZA, KIHONDA MKOANI MOROGORO.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Malimi Malemi (wa pili kutoka kushoto) akiangalia nyuzi za mkonge ambazo
zimeanikwa kwa ajili ya kukaushwa maji kabla ya kuingizwa kiwandani kwa
ajili ya
kuzilainisha na kuzisafisha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna
Jenerali John Minja.
Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Nyuzi za Mkonge cha
Gereza Kihonda lililopo mkoani Morogoro, Fidelis Muhaya akimuonyesha
majani ya
mkonge ambayo yamevunwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi,
Malimi Malemi (Kushoto). Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa
Programu ya
Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta.
Naibu Katibu Mkuu,
Mwamini Malemi (katikati) akizishika nyuzi za mkonge
zilizokamilika
ambazo zipo tayari kwa ajili ya matumizi mbalimbali nchini.
Naibu Katibu Mkuu,
Mwamini Malemi (katikati) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna
Jenerali John Minja (kushoto) pamoja na wageni wengine wakionyeshwa
pamoja na
kufafanuliwa zaidi na Msimamizi wa kiwanda hicho Fidelis Muhaya jinsi
inavyofanya kazi mashine ya kubana mkonge kwa ajili ya kupunguzwa
ukubwa.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (wa pili kutoka
kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John
Minja
(kulia) pamoja na wageni waliotembelea kiwanda hicho wakiangalia mashine
ya
kubana mkonge kwa ajili ya kupunguza ukubwa kabla ya
kusafirishwa. PICHA
ZOTE
NA KITENGO CHA
MAWASILIANO YA
SERIKALI
WIZARA YA MAMBO
YA NDANI YA
NCHI.
Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya kuuwawa kwa Padri Evaristitus Mushi
Padri Evaristitus Mushi
Padri Evaristitus Mushi wa KANISA la katoliki,Parokia ya ST.Joseph,Shangani,Unguja ameuwawa leo mnamo saa moja asubuhi katika eneo la Beit-EL-Ras karibu na kanisa la Katoliki.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Mohamed Aboud imeeleza kuwa kutokana na tukeo hilo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatambua wale wote waliohuka na tukio hilo kwa ajili ya kuwachukulia hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria.
Aboud amesema kuwa wakati uchunguzi huo unaendelra, Serikali inawaomba wananachi wote kuwa watulivu na kuliachia Jeshi hilo la Polisi kutekeleza wajibu wake .
Aidha Serikali imetoa mkono wa pole kwa familia na wanafamilia wa marehemu pamoja na waumini wa kanisa hilo kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA FREEMAN MBOWE AONGEA NA VIONGOZI WA CHAMA KUTOKA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI
Mwenyekiti wa chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema Freeman Mbowe akiwa anaongea na viongozi
wa chama kutoka katika mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni arusha
,kilimanjaro ,manyara pamoja na tanga kuhusiana na sera ya majimbo leo
jijini Arusha
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na
maendeleo chadema Freeman Mbowe akiwasili katika ukumbi wa bugaloo kwa
ajili ya kuongea na viongozi wa vyama mbambali kwa jili ya kupanga
mkakati wa chama chao
mwenyekiti wa muda wa chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema kanda ya kaskazini ambaye pia ni mbunge
wa karatu akiwakaribisha viongozi mbalimbali wa kanda ya kaskazini
katika kikao cha viongozi wa chama hicho kanda kikao ambacho kinajadili
seraya majimbo
picha juu na chini wajumbe ambao ni
viongozi walioudhuria mkutano huo
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida
mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA),Freeman
Mbowe amesema kuwa mauji ya Viongozi wa
dini ambayo yametokea,katika mkoa wa Geita, na Zanzibar ni
matokeo ya CCM,na hivyo kama
wataandelea kuendesha nchi kwa msingi hiyo bado nchi itakabiliwa na mauji makubwa sana
Mboye aliyasema hayo mapema leo wakati akizindua kanda ya kaskazini
kwa chama hicho ambayo itaweza kuhudumia mikoa ya kanda ya kaskazini
katika shuguli za kichama na za kijamii
Alisema kuwa hapo awali Chadema kilishasema kuwa CCM isipuuzie
matatizo ya ubaguaji wa dini lakini chama hicho hakikusikia na badala
yake kiliendelea kujiendesha kwa misingi ya kubaguana kidini hali
ambayo sasa inanyima watu uhuru wa kuabudu na kufanya mambo yao
Alisistiza kuwa kama CCM bado iliendelea kufanya ubaguzo wa dini kwa
misingi kuwa inakomoa Chadema lakini hawakujua na kutambua kuwa hali
hiyo inafanya mauaji ya kila siku ambayo sasa yameanza Geita lakini
Leo yameelekea Zanzibar mara baada ya Padre kuuliwa wakati akielekea
Kanisani kusalisha misa
“Leo kila mahali unasikia mauji ya dini lakini mimi nilishawaambia CCM
kuwa hiii sio hali ya kuendelea kuangalia lakini walujua kuwa ni
siasa na wao walifanya hivi kwa malengo ya kuwa wanatukomoa sisi
Chadema kwa kugawa Taifa katika Imani ya kidini sasa wamelikoriga
wanatakiwa kulinywa’aliongeza Mbowe
Katika hatua Nyingine Mbowe alisema kuwa wao kama Chadema wanalaani
Mauji ambayo yanatokea kila siku ndani ya Tanzania na kwa hali hiyo
hawataweza kuwagawa wananchi katika misingi ya kidini kwa kuwa wote
wapo sawa na kama Nchi itaendeshwa hivyo ni wazi kuwa damu ambazo
hazina hatia zitamwagika kila mara.
“Chadema tunaalani kwa kweli haya mauji na kwetu Muislamu, Mkristo
wote ni wa moja na kamwe kiongozi ambaye ataonesha ubaguzi dhidi ya
wakristo na waislamu ni wazi kuwa tutamkimbia hatuwezi kuingiza
jitiada za CCM ndani ya chama chetu,na kuweka utaratibu wa kumwaga
damu ambazo hazina hatia kabisa’aliongeza Mbowe
Akiongelea suala la kanda ya kaskazini ndani ya chama hicho alisema
kuwa hiyo ni moja ya mikakati ambayo imewekwa na mbali na hilo pia
kupitia viongozi wa kanda ya kaskazini wataweza kujiwekea nafasi nzuri
sana ya kuchukua Nchi ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2015 hivyo
kufanya Nchi iwe huru zaidi kuliko ilivyo kwa sasa
Mbowe aliongeza kuwa kanda ya kaskazini pia itaweza kuwa chachu ya
Maendeleo kwa kuwa itaweza kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo
zinawakabili kwa kuwa sasa kazi za maendeleo zitafanywa chini ya mikoa
minnne tofauti na hapo awali ambapo kila mkoa ulikuwa unajitegemea kwa
shuguli za kichama na za kichama.

TAMKO LA RAIS KIKWETE KUHUSU MAUWAJI YA PADRI ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.
Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushin a kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”
Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu
TARIFA MPYA KUHUSU KIFO CHA PADRI ZANZIBAR LEO
Taarifa imeripoti kuwa Padre Mushi aliuawa na watu walipolisimamisha gari la Padre huyo alipokuwa akielekea katika kanisa la Mtakatifu Theresia lililoko eneo la Mtoni, na alipopunguza mwendo ili awasikilize, ndipo alipopigwa risasi kichwani na kusababisha gari alilokuwamo kukosa uelekeo na kuigonga nyumba iliyokuwa jirani. Watu walioshuhudia tukio hilo walimchukua Padre Mushi ili kumwahisha hospitalini katika jitihada za kuokoa uhai wake, lakini alifariki dunia. Waliomwua Padre Mushi bado hawajakamatwa.
-----------------------
Akina mama wakilia kwa uchungu kuomboleza kifo
cha ghafla cha kupigwa risasi Padre Evaristus Mushi kilichotokea leo
asubuhi muda mfupi kabla ya kuanza Misa ya Jumapili kwenye kanisa la
Kigango cha Mtoni, Zanzibar. (Picha na Martin Kabemba via Lukwangule
blog)
Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara Miwili huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.
Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.
Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.
Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.
Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.
Wakizungumza kuhusu hilo, raia wamesema hawana imani na Polisi wala Madaktari na hawatarajii jipya zaidi ya ripoti kuwa suala hili ni la uhalifu kwa kuwa tukio kama hili liliwahi kutokea mwishoni mwa mwaka jana kwa Padre Ambrose kupigwa risasi na taarifa zilisema lilikuwa ni tukio la kihalifu na kwamba risasi hazikutumika jambo ambalo halikuwa kweli kwani Padre Ambrose alikutikana na risasi alipohamishiwa katika hospitali ya Taifa, Muhimbili.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali fuatilia vyombo mbalimbali vya habari.
SIMBA IMESHADUNGWA MSHALE 1-0 NA LIBOLO FC YA ANGOLA,
Mchezaji
wa timu ya Simba ya Tanzania Shomari Kapombe kulia akichuana vikali na
Maieco Antonio mchezaji wa timu ya Libolo FC kutoka nchini Angola
wakati wa mchezo wa Klabu Bingwa Afrika ( CAF) kati ya timu hizo
uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Timu ya Libolo
FC ya Angola inaongoza goli 1-0 dhidi ya Simba ya Tanzania ni kipindi
cha pili na mpira bado unaendelea.
Waamuzi
wa mchezo huo wakiwaongoza wachezaji wa timu ya Simba na Libolo ya
Angola wakati timu hizo zikiingia uwanjani tayari kwa kumenyana katika
mchezo huo.
Wachezaji
wa Simba ya Tanzania na Libolo FC ya Angola wakisalimiana kabla ya
kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
TAARIFA YA INSPEKTA JENERALI WA POLISI SAID A. MWEMA KWA UMMA KUHUSU TUKIO LA KUUWAWA KWA PADRE EVARISTI MUSHI ZANZIBAR TAREHE 17 FEBRUARI, 2013
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema
akitoa taarifa ya jeshi hilo mbele ya waandishi wa habari katika makao
makuu ya jeshi hilo leo mchana.
Nimelazimika nizungumze nanyi kuhusu
tukio la kuuwawa kwa Padre Evaristi Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar
lililotokea leo asubuhi tarehe 17 Februari, 2013 eneo la Mtoni mkoa wa
Mjini Magharibi, ambapo watu wasiofahamika walimpiga risasi Padre huyo
alipokuwa anaenda kusalisha ibada katika kanisa la Betras. Baada ya
tukio hilo kutokea alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo
baadae alifariki dunia. Tukio hili ni baya na la kusikitisha.
2 Kufuatia kutokea kwa tukio hilo na
kujirudiarudia kwa vitendo vya kuwashambulia na kuwadhuru viongozi wa
dini na uchomaji wa nyumba za ibada, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na
vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumeanza uchunguzi wa kina wa
kuwatafuta wanaohusika na matukio hayo.
3Hivyo, nimetuma timu ya wataalam
waliobobea kwenye masuala ya upelelezi na oparesheni kutoka Makao Makuu
ya Polisi, kwenda kushirikiana na timu ya wataalam iliyoko Zanzibar.
Hadi sasa watu watatu wananshikiliwa kwa mahojiano.
Jeshi la Polisi limeimarisha doria
maeneo yote hapa nchini na tunafuatilia mienendo na kuakamata watu wote
wanaochochea, kufadhili, kuhamasisha na kushiriki katika vitendo vya
uhalifu, vurugu na fujo.
Tukiwa katika kipindi hiki, nawaomba
wananchi wote hapa nchini kuwa watulivu wakati suala hili
linaposhughulikiwa kuhakikisha kwamba wahalifu hao wanakamatwa na sheria
inachukua mkondo wake.
Naomba nitumie fursa hii pia,
kuwasiliana na wananchi wenzangu wenye taarifa zitakazosaidia wahalifu
hao kukamatwa kutupa ushirikiano kupitia namba zetu maalum za simu
zifuatazo 0754785557 au 0782417247 na namba za makamanda wa mikoa na
vikosi, ili kuhakikisha kwamba amani, usalama na utulivu vinadumishwa
hapa nchini.
Nawashukuru wananchi wote ambao
wamekuwa wakitupa ushirikiano.
AHSANTENI SANA.
BAADHI YA FAMILIA ZA KOSA MAHALI PA KUISHI BAADA YA NYUMBA ZAO KUEZULIWA NA UPEPO MKALI
BAADHI ya wakazi wa maeneo ya Mafisa mkoani hapa wamekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha leo jioni,
Mbali na kuezua nyumba hizo pia upepo huo uliangusha miti mirefu,taa za barabarani na mabango marefu ya matangazo ya makampuni ya simu ya vodacom na tigo
Miongoni mwa mabango hayo ni bango kubwa la vodacom ambalo liliwekwa eneo la stendi ya mabasi ya Msamvu katikati ya geti kuu la kutokea mabasi eneo ambalo pia madereva wa boda boda huegesha pikipiki zao chini ya bango hilo.
" Ni mungu tu ametunusulu na kifo wakati bango hili linaanguka sisi tulikuwa hapa chini tukisubiri abiria kwa bahati tuliwahi kustuka,na kukimbia mwenzetu mmoja kwenye heka heka ya kukimbia aliiacha pikipiki yake ambayo aliangukiwa na bango hili na kuhalibika vibaya"alisema mmoja wa mabareva hao wa boda boda aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Samwel
Hii ni mara ya pili kwa bango la kampuni hizo kuanguka ambapo mara ya kwanza takribani miaka miwili iliyopita bango la tigo lililowekwa katikati ya stendi ya daladala lilianguka na kuharibu daladala mbili ambazo kwa bahati zilikuwa hazina watu ingawa zenyewe zilihalibika vibaya baada ya kuanguliwa na bango hilo.
Pia upepo huo uliovuma jana kutoka upande wa kaskazini ya mji wa Morogoro uliezua nyumba za watu na kuangusha miti mirefu ambapo hadi mtandao huu unakwenda hewani takribani nyumba 15 ziliezuliwa mapaa hali iliyosababisha wakazi wa nyumba hizo kukosa mahali pa kuishi.
BREAKING NEWZZZ!!!!! PADRI APIGWA RISASI HADI KUFA ASUBUHI HII HUKO ZANZIBAR
Taarifa zilipatika sasa hivi ni kuwa Paroko wa
Kanisa la Katoliki Minara Mirefu Zanzibar, Evarist Mushi amefariki dunia
baada ya kupigwa risasi saa 1.00 asubuhi na kufariki kabla hajafika
hospitali ya Minazi Mirefu. Paroko huyu amepigwa risasi akishuka katika
gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00 leo.
Kwa siku za hivi karibuni
kumekuwako na vitisho vya wazi wazi dhidi ya wakristu huko visiwani
Zanzibar ambapo inaelezwa kuwa jeshi la polisi halijafanya juhudi yoyote
kuzuia tishio hili. Kumekuwapo na vipeperushi vinavyodai kuwa kupigwa
risasi kwa padre Ambrose sio mwisho wa mapambano.
Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar.
Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar.
R .I.P
SOURCE WAPO RADIO
SOURCE WAPO RADIO
Saturday, February 16, 2013
MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO, AZAM YAIFUNGA EL NASIR 3-1
Kiungo wa timu ya Azam FC, Bolou Kipre (kushoto)
akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa El-Nasir FC ya Sudan ya
Kusini, Abdallmelik Sebit katika mchezo wa Kombe la Shirikisho
uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Azam FC
wakishangilia bao la pili la timu yao lililofungwa na Kipre Tchetche
(katikati) wakati ilipoibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya El Nasir ya
Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Jabir Aziz akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa El Nasir FC ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe
la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Mshambuliaji wa
Azam FC, Brian Umomy akiwatoka walinzi wa timu ya El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Jacob Osuru na Abdallmelik Sebit katika mchezo wa kombe
la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Kikosi cha el Nasir ya Sudan ya Kusini
Kikosi cha Azam FC
Mashabiki wa Azam
Subscribe to:
Posts (Atom)