Sunday, February 17, 2013

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MWAMINI MALEMI ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA NYUZI ZA MKONGE CHA JESHI LA MAGEREZA, KIHONDA MKOANI MOROGORO.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Malimi Malemi (wa pili kutoka kushoto) akiangalia nyuzi za mkonge ambazo zimeanikwa kwa ajili ya kukaushwa maji kabla ya kuingizwa kiwandani kwa ajili ya kuzilainisha na kuzisafisha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja.
Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Nyuzi za Mkonge cha Gereza Kihonda lililopo mkoani Morogoro, Fidelis Muhaya akimuonyesha majani ya mkonge ambayo yamevunwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Malimi Malemi (Kushoto). Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (katikati) akizishika nyuzi za mkonge zilizokamilika ambazo zipo tayari kwa ajili ya matumizi mbalimbali nchini.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (katikati) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) pamoja na wageni wengine wakionyeshwa pamoja na kufafanuliwa zaidi na Msimamizi wa kiwanda hicho Fidelis Muhaya jinsi inavyofanya kazi mashine ya kubana mkonge kwa ajili ya kupunguzwa ukubwa.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na wageni waliotembelea kiwanda hicho wakiangalia mashine ya kubana mkonge kwa ajili ya kupunguza ukubwa kabla ya kusafirishwa. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...