Saturday, February 16, 2013
IBF Yachukua nafasi ya Katikati Barani Afrika.
Upimaji uzito katika mapambano mawili ya IBF yanayofanyika katika majiji ya Johannesburg na Tunis umefanyika vizuri leo.
Mapambano haya yaliyopewa jina la “Barabara ya kutoka Cape Town mpaka Cairo kwa IBF” kutokana na majiji haya kukaa moja kusini na lingine kaskazini mwa Afrika, yanafanyika wakati IBF ikijipambanua vyema katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Kusini mwa Afrika, leo imeshughudia mabaondia mawili wanaopambania ubingwa wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25 wakipima uzito mbele ya mashirika mbalimbali ya habari ya ndani na nje ya Afrika ya Kusini.
Illunga Makabu kutoka Jamhuri ay Watu wa Kongo (DRC) alipima uzito kumkabili Gogota Gorgiladze wa Georgia. Upimaji huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa ulio katika hotel ya nyota tano ya Emperors Palace iliyoko katika jiji la Johannesburg!
Rodney Berman mtu anayeheshimika kwa kuwa promota wa kwanza kuandaa pambano la IBF la dunia katika bara la Afrika mwaka 1990, ndiye anayepromoti pambano hili!
Tayari wadau na mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwamo Namibia, Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania wameshawasili nchini Afrika ya Kusini tayari kuangalia mpambano huo. Wengine walibaki Afrika ya Kusini wakati wa mashindano ya kombe la Afrika yaliyomalizika wiki iliyoita.
Msimamazi mkuu wa mpambano huu ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi aliyesimama pichani na mabondia Gogita Gorgiladze (kushoto) na Ilunga Makabu (kulia)
Kaskazini mwa Afrika,
Bondia ambaye ameshajizolea sifa kemkem Ayoub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium atapigana na bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana kugombea ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Light Middle.
Mpambano huo uliopewa jina la “Uzuri wa Jasmine” kutokana na jina hilo kutumika katika mapinduzi yaliyomwondoa Rais wa zamani wa Tunisia Ben Ali unafanyika wakati Ayoub Nefzi akijiandaa kugombea mkanda wa juu wa IBF wa mabara mwezi wa tatu nchini Belgium.
Mabondia wote wawili wanatagemea kuonyesha moto mkali katika mpambano ambao tayari mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi za Nigeria, Ghana, Libya, Misri, Algeria tayari wameshawasili nchini Tunisia kuangalia mpambano huo!
Tunisia inasifika kama nchi iliyowahi kutoa viongozi wengi wa mchezo wa ngumi katika bara la Afrika.
Fastjet yatoa mafunzo kwa Mtanzania wa Kwanza Mmaasai kuongoza ndege aina ya Airbus.
William Zelothe Stepehen
akiwa ndani ya ndege aina ya Airbus A319.
William Zelothe Stepehen
akiwa na marubani wa ndege ya Fastjet.
William Zelothe Stepehen ni
Mtanzania wa Kwanza Mmaasai aliyepewa ithibati ya kuiongoza ndege aina
ya Airbus A319 punde tu baada ya kupokea mafunzo ya urubani
yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet. Alipata mafunzo hayo
nchini Uingereza kwa muda wa takriban miezi miwili na amerudi nchini
Tanzania hivi karibuni. William alikulia Olosipe jijini Arusha ambapo ni
nyumbani kwa wazazi wake.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JESHI
LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
15 Februari
2013
Meli
vita tatu (3) kutoka Jeshi la Wanamaji la Urusi zijulikanazo “MARSHAL
SHAPOSHNIKOV”, “ALATAU” na “IRKUT” zikiongozwa na Rear Admiral Vladimir
Vdovenko, watawasili nchini tarehe 16 February 2013 na kuondoka tarehe
20
Februari 2013 katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufanya ziara
ya
kirafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi.
Waandishi
wa Habari mnakaribishwa kufanya ‘coverage’
ya tukio hilo
Siku ya
Jumatatu, tarehe 18 February 2013 saa 1.00
hadi saa 3.00 usiku.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao
Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP
9203, Simu: 0764 742161
Email:
ulinzimagazine@yahoo.co.uk
K U M B
U K U M B U
MMJ/JB/
Feb 13
DP
ADMN
Kufanya mahusiano na uongozi wa
Bandari
1.
Kurugenzi ya Habari imefanya zoezi la kuwaita waandishi wa Habari kutoka
vyombo
vya habari vifuatavyo TBC, ITV, CLOUDS TV, MLIMANI TV, STAR TV, na
CHANEL
TEN.
2.
Uongozi wa Bandari hauruhusu Waandishi wa Habari kuingia kufanya
“coverage”
kwenye eneo hilo bila taarifa rasmi.
3.
Inaombwa mahusiano yafanyike na bandari kuhusiana na mapokezi ya
waandishi wa
habari watakao hudhuria siku hiyo ili kukwepa usumbufu kwa waandishi
hao.
(KM
Mgawe)
Col
DIPR
NEY WA MITEGO APATA AJALI MBAYA YA GARI
ajali hiyo ilitokea maeneo ya mataa ya St Peters, alipokuwa akitokea masaki kuelekea moroko, na baada ya mataa yake kumruhusu kupita, alikutana na Lori lililokuwa likitokea Mjini kuelekea Moroko pia, likiwa halina taa na kumvaa kwa nyuma na kupelekea gari lake kuingia mtaroni na kuharibika vibaya
ndinga aliyokuwa nayo Ney ni aina ya Altezza, ina thamani ya shilingi millioni 14, kama angekuwa amelipia bima katika kiwango cha Comprehensive, yaani bima kubwa, angerudishiwa gari ndinga mpya, akini kwa bahati mbaya alilipa bima ya kawaida
Friday, February 15, 2013
MKONO WA ALBINO WAPATIKANA SUMBAWANGA
MKuu wa
Mkoa wa Rukwa , Stella Manyanya wa tatu
kulia akibubujikwa na machozi jana usiku baada ya ya Kaimu Kamanda
wa
Polisi Mkoa , Peter Ngusa (kulia) akiwa ameushikilia mkono
ulionyofolewa
hivi karibuni kutoka kwa mwanamke mwenye ulemavu wa
ngozi (hayupo pichani) na kufukiwa poroni
kijijini
Miangalua wilayani Sumbawanga akiuonesha hadharani mbele ya majengo
ya Hospitali ya Mkoa mjini hapa , watatu kushoto ni Mganga Mkuu wa
Mkoa , Dk
John Gurisha
Mmoja wa askari akifungua
majani ya mgomba yaliyoufunga mkono ulionyofolewa hivi karibuni
kutoka kwa
mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi (hayupo pichani) na kufukiwa poroni
kijijini
Miangalua wilayani Sumbawanga ambao akiuonesha hadharani mbele ya
majengo
ya Hospitali ya Mkoa mjini hapa jana usiku jana Februari
14.
JAJI MKUU WA KENYA, MHE. MUTUNGA AKUTANA NA WAJUMBE TUME YA KATIBA
Jaji
Mkuu wa Kenya, Mhe.
Willy Mutunga (katikati) akibadishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko
ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume, Dkt. Sengondo
Mvungi
nje ya ukumbi wa Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa
mkutano
kati yake na Wajumbe wa Tume leo Ijumaa (Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga
alikutana
na Wajumbe ili kubadilishana mawazo na uzoefu katika uandishi wa Katiba
Mpya.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko
ya
Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (kushoto) akibadilishana
mawazo
na Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga nje ya ofisi za Tume Jijini
Dar es
Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume
leo
(Ijumaa Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga amekutana na Wajumbe wa Tume
kubadilishana
mawazo na uzoefu wake kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko
ya Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akimwonyesha nakala ya
Kitabu Jaji
Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) nje ya ofisi za Tume mara
baada ya
kumalizika kwa mkutano kati yake na wajumbe wa Tume baina yao
uliofanyika
katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa Feb. 15, 2013).
Mhe.
Mtungi amekutana na Wajumbe wa Tume kuzungumzia uzoefu wake kuhusu
uandishi na
utekelezaji wa Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph
Warioba. (PICHA NA TUME YA
KATIBA)
JESHI LA POLISI WALIVYOWEKA ULINZI MKALI KUFUATIA MAANDAMANO YA WAFUASI WA SHEKH PONDA
Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya jengo la Sukari lililopo mkabala na Makutano ya Barabara za Ohio na Sokoine Driver Posta jijini Dar es salaam jengo hilo ndmo zilimo ofisi za mwendesha mashtaka wa Serikal Dk.Eliezer Feleshi, Ulinzi huo umeimarishwa kutokana na tishio la wafuasi wa Shekh Ponda kutishia kuandamana kwenda kwa Mwendesha Mashtaka huyokushinikiza Shekh Ponda aachiwe huru.
Baadhi
ya wafuasi hao wa
Shekh Ponda wamekamatwa katika maeneo mbalimbali wakati wakijaribu
kuingia
katika eneo la Posta ambapo ulinzi mkali uliimarishwa huku polisi
wakitumia
Magari, Pikipiki, Mbwahuku makachero wakizunguka kila
mahali.
Baadhi
ya Barabara
zilifungwa ili kuweka eneo hilo katika hali ya usalama zaidi na
kuhakikisha
linzdhibitiwa na kulidwa kirahisi.
Askari Polisi wakifanya doria kwa
kutumia pikipiki kam wanavyoonekana wakiranda katika mitaa mbalimbali
Posta
jijini Dar es salaam.
Baadhi ya
waumini wa Dini ya Kiislamu
wakirushwa kichura leo Katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es
Salaam
walipokamatwa kwa tuhuma za kuandamana kushinikiza Sheikh Ponda aachiwe
kwa
dhamana.
Askari Kanzu akiwa amemkamata muumini wa Dini ya Kiislamu katika pilikapilika za kudhibiti maandamano ya kushinikiza Mahakama imuachie kwa dhamana Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda, Dar es Salaam
Askari Kanzu akiwa amemkamata muumini wa Dini ya Kiislamu katika pilikapilika za kudhibiti maandamano ya kushinikiza Mahakama imuachie kwa dhamana Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda, Dar es Salaam
Lady Gaga Cancels World Tour For Hip Surgery.
Lady
Gaga has cancelled the remainder of her world tour after discovering
she needs surgery for a hip injury.
The
announcement was made on Wednesday, one day after the pop superstar
lamented having to delay some of her forthcoming North America concerts.
A
news release said Gaga, 26, has a tear in the labrum in her right hip
that would require surgery followed by a recovery period.
The
labrum is a layer of muscle that helps holds the ball-shaped hip joint
in place.
NCCR – Mageuzi yapinga hatua zozote za kutaka kuzuia matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni.
Chama
cha NCCR – Mageuzi kimesema kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya Katibu wa Bunge kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa
kuzuia kurusha matangazo moja kwa moja na badala yake kuyafanyia kwanza
uhariri kabla ya kuwafikia walaji.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa chama
hicho Faustin Sungura NCCR – Mageuzi inapinga kwa nguvu zote, hatua
zozote zinazotaka kuchukuliwa na mamlaka yeyote za kuzuia matangazo ya
moja kwa moja kutoka bungeni.
Amesema
wanapinga hatua hizo kwa sababu, hoja na sababu za kutekeleza azma hiyo
kama zilivyotolewa na Katibu wa Bunge ni hoja dhaifu na hasi.
Amesema
mawazo ya Katibu wa bunge yanakinzana na Ibara ya 18(d) ya katiba ya
nchi.(Picha na Maktaba).
Nigerian singer Susan ‘Goldie’ Harvey has died in Lagos.
Nigerian pop singer Susan Oluwabimpe Harvey,
popularly known as “Goldie”, has died after a sudden illness.
Her record label said Miss Harvey, 31, had
complained of a severe headache shortly after returning to Nigeria from
the US where she had attended the music industry’s Grammy Awards.
The star was rushed to a hospital in Lagos,
where she was pronounced dead.
Goldie had won several industry awards and
appeared in last year’s celebrity Big Brother Africa TV show.
Pope appoints Ernst von Freyberg new Vatican bank head.
Pope Benedict XVI has appointed German lawyer
Ernst von Freyberg to head the Vatican’s embattled bank.
Mr Freyburg’s selection is one of the last
major appointments of the Pope’s tenure in office.
The bank, officially known as the Institute
for Works of Religion, has been dogged by scandal in recent years.
The pontiff, 85, shocked the world’s biggest
Christian Church on Monday when he announced his resignation.
AFYA YA MATUMAINI YATENGAMAA
SHIRIKISHO la filamu nchini(TAFF) limesema, limefurahishwa na taarifa iliyotolewa na madaktari wa hospitali ya Amana kuwa afya ya msanii wa vichekesho Bi.Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’iposhwari na wamemruhusu kurudi nyumbani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Rais wa Shirikisho hilo la filamu nchini(TAFF) Simon Mwakifamba alisema kuwa wao kama shirikisho wamepokea kwa furaha taarifa hiyo.
"Tunajisikia poa kwa afya ya msanii huyo kurejea kuwa nzuri, baada ya kuwa ameruhusiwa na madaktariwa hospitali hiyo ya Amana kwa kuwa amerudi nyumbani kwao Kiwalani jijini Dar es Salaam,"alisema Mwakifamba.
Afya ya msanii huyo ilibadilika na alianza kuumwa alipokuwa ameenda nchini Msumbiji na alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
MKUU WA MKOA WA RUKWA AAHIDI KUWACHUKULIA HATUA KALI WALANGUZI WA NISHATI YA MAFUTA MKOANI HUMO
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza
katika kikao cha baraza la ushauri la watumiaji wa nishati na maji
nchini na wadau wake walipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za baraza hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pongezi kwa kazi
nzuri wanayofanya na kuahidi kuwachukulia hatua walanguzi wa nishati ya
mafuta pamoja na wale wanasimamia kwa kushindwa kufanya kazi yao vizuri.
Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri watumiaji wa
maji na nishati nchini Eng. Profesa Katima akizungumza katika kikao
hicho ambapo alisema kazi kubwa ya baraza hilo ni kutetea na kulinda
haki za watumiaji wa maji na nishati ambayo ni maji safi na maji taka,
umeme, petroli na gesi asilia.
Baadhi ya wadau wa mkutano huo ambao ni
vyombo vya ulinzi na usalama, Tanesco, EWURA Mkoa wa Rukwa, wawakilishi
wa sheli za mafuta na shirika la Maji safi na Maji taka Mkoa wa Rukwa
(SUWASA)
Wawakilishi wa baraza hilo Mkoani Rukwa
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba -Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Rukwa)
WAZIRI WA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO ATEMBELEWA NA BRITISH COUNCIL OFISINI KWAKE
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (Mb)
akisalimiana na Mkurugenzi wa British Council nchini Sally Robinson
(kulia) leo Ofisini kwa Waziri,alipokwenda kumtembelea na kufanya
mazungumzo mbalimbali kuhusu tasnia ya ubunifu wa Sanaa na Utamaduni
pamoja na jinsi ya kuwajengea uwezo katika fani mbalimbali za sanaa na
ujasiria mali.
Picha ya pamoja
Waziri
wa Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara
(Mb)akizungumza na Mkurugenzi wa British Council nchini(kulia) Sally
Robinson leo alipomtembelea Ofisis kwake jijini Dar es Salaam na
kuzungumza masuala mbalimbali ya tasnia ya Utamaduni,
Rais Jakaya Kikwete Asaini Kitabu Cha Maombolezo na Kutoa Heshima za Mwisho Kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT)
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia
saini
kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini
Kati la
Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT)jana, Alhamisi, kwenye
Kanisa
Kuu la KKKT mjini Arusha kabla ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili
wa
Askofu.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa
heshima
zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya
Kaskazini Kati
la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT)Jana, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini
Arusha.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiifariji familia ya Askofu
Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati nyumbani kwa Askofu mara
baada ya
kuwa ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa
Kuu la
KKKT mjini Arusha jana, Alhamisi, Februari 14, 2013. Picha zote na
Freddy
Maro-IKULU
Subscribe to:
Posts (Atom)